Mgomo wa Kutoa Unyumba Mpaka Barabara Ijengwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Kutoa Unyumba Mpaka Barabara Ijengwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtumiabusara, Jul 3, 2011.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Zaidi ya wanawake 250 wa mji mmoja nchini Kolombia wameanza mgomo wa kuwapa unyumba waume zao ili kuishinikiza serikali iifanyie marekebisho barabara inayoingia mjini humo.

  Wanawake katika mji wa Barbacoas wanaamini kwamba iwapo wataanza mgomo wa "kuibana miguu yao" kwa kuwanyima unyumba waume zao, basi waume zao watalazimika kufanya jitihada za kuishinikiza serikali yao kuijenga barabara inayoingia mjini humo ambayo iko kwenye hali mbaya sana kiasi cha kuhatarisha maisha yao.

  Kwa miaka 20, serikali iliahidi kuifanyia marekebisho ya barabara hiyo inaoingia kwenye mji wa Barbacoas ambao una jumla ya wakazi 40,000 lakini haijawahi kutimiza ahadi yake, limeripoti jarida la Wall Street Journal.

  Hivi sasa inawachukua watu masaa 10 kuweza kusafiri umbali wa kilomita 56.

  "Wanawake hawa na watu wote katika mji huu, tumechoshwa na ahadi hewa za serikali", alisema Lucelly Del Carmen Viveros, mtetezi wa haki za binadamu kwenye mji wa Barbacoas.

  "Hii ndio barabara pekee inayouunganisha mji wa Barbacoas na miji ya karibu nchini lakini ipo katika hali mbaya sana", aliongeza Viveros.

  source: nifahamishe.com
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hili tungeweza kulifanya wanawake wa Tanzania, nina hakika umeme ungekuwa historia na isitoshe ahadi zote zingetimizwa....kama kuna mwanamke anabisha hebu tujaribu tuone kama haijawa kweli
   
 3. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inawezekana ila inabidi mdhibiti sana mauzo ya sabuni na mafuta wasi - Masturbate. .na muwafukuze Gays wote...kwani wanaume wakipata second option ya kukidhi haja zao ..mtakuwa hamjafanya kitu..mbaya zaidi wanaweza kuwachukia..
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,993
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  kama ndoto zinatekelezeka basi vipofu leo wataona na viziwi kusikia..........hivi akina mama si ndiyo wanahitaji kuhudumiwa zaidi au.......................kwa hiyo mgomo wawezekana kweli kwani wakinyimwa unyumba hukimbilia kwa waganga wa kienyeji ili wajaribu kusawazisha majambos...............................khofu yao ni kuwa lazima njemba itakuwa imepata kidosho kipya ndiyo maana inaleta soooooooooooooookomoko
   
 5. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Tumewapa nafasi ya kuongoza bunge kwanza, tukidhibitisha uwezo wao itabidi tuwape na sector nzima ya umeme waisimamie wao !!!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wameharibu tayari si unaona mheshimiwa sana spika anavyoharibu?????
   
 7. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Serikali ndo iliyo na wajibu wa kujenga barabara. Hakuna uhusiano uliopo kati ya kumnyima unyumba mmeo na ujenzi wa barabara. Au hao wanaume ndo waliosababisha ubovu wa barabara? Uonevu mtupu!
   
 8. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Si mnamkumbuka yule mheshimiwa waziri aliyesema wanawake wawanyime unyumba waume zao kwa sababu fulani za kisiasa
   
 9. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Ha ha haaaa! kama ni mgomo wagome wake zao kuanzia mkuu wa wakaya mpaka balozi wa nyumba kumikumi, eti mke wangu mama Kadogo mi'nna tatizo gani??
   
 10. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  kwani magodoro yao yapo barabarani?
   
 11. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  swali la msingi Shantel, .............. kwani sie mbona hatujanyimwa kwa sababu ya UMEME hapa nilipo nawahi kwa mpemba kuchukua mshumaa teh teeh teeeh.
   
 12. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  si ndio hapo, umeme hatuna, barabara hatuna na hata kale karaha nako tupeane kwa mgao?
   
 13. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  ndiyoooooooooo ila sikumbuki kama walifanikiwa adhima yao...... sie hapa bongo we acha tu sipati picha maana mmmmhhh!
   
 14. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  hata mungu hapendi..... full kuduh!!
   
 15. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wanawake ni wanafki kama paka we umeona wapi eti mtu anajifanya msafi anaingia bafuni kuoga anafunika nywele zisipate maji sasa nini maana ya kuoga, utakuta wakiwa kwenye kikao hoo tuwanyime waume zetu chululuu akirudi ndani anamwambia bwanke eti wanataka kunichukulia mume wanataka niachane na wewe wanataka nikunyime chululuu anampa akitoka nje anawaambia wenzake mimi simpi kabisa na waume ni washenzi kaa mbwa akipewa anakula na akikutana na rafiki yake anamuuliza ebwan vipi hawa wanawake wanafanya nini tena wanataka kutunyima vikojoleo? mwanzake anamjibu ebwan t mimi nashaa wiki ya pili hii sipewi anajua haha kumbe mama fatu anamnyima bwanke anamtokea na kuanza kusaundisha ukifanya mchezo unaweza ndio usipewe moja kwa moja mskaji akawa ndio anajisevia.

  changanyani na za kwenu nyie ka a mmeanzisha vijiwe eti mtunyime ndio matataizo ya umeme yataisha wakati hata mkuu wa kaya mwenyewe jah wa kaya alisema matatizo ya nchi yalikuwepo tangu awamu ya kwanza na yeye ameyakuta na hatayamaliza na ataondoka amwachie na mwingine sasa ndio mfikirie mtatunyima mpaka lini chakachueni kwa raha zenu maana hata likiisha la umeme litakuja lingine sasa si utajikuta unakufa na nyexx zako na tukianzisha vismall hausi mtaanza tena kuingia mitaani au kwenda kwa waganga?
   
Loading...