Hatua yoyote ile ya kugoma kutoa huduma kwa WATANZANIA wasio na hatia haitakubalika. Kwa sasa watanzania tutalaani na kupinga action yoyote kwa madaktari wanayokusudia kuchukua. Hatua hiyo ni kama uhaini kwa kukusudia kuua raia wema wanaokamuliwa kodi kwa kusomesha na kuwalipa mishahara wataalamu. Tunaamini bado kuna nafasi ya kukaa na kupata muhafaka kupitia meza ya majadiriano bila kuilazimisha, kuisulutisha na kuiwekea mashariti ya kuidhalilisha serikali eti kwa kwa kigezo ni kada muhimu. Serikali ina utaratibu wake ambao inapaswa uheshimiwe na watu wote kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Pia tunatoa mwito kwa serikali kuheshimu taaluma za wataalamu wetu kwa kuwapatia vitendea kazi na maslahi yanayokidhi taaluma husika. Suala la kada ya afya lishughulikiwe kwa ujumla wake kwa kuzingatia wataalamu wote waliopo katika kada hiyo bila kuwabagua maana wanategemeana bila kusema Daktari ni bora zaidi, kinyume na hapo ni kuzalisha Crisis nyingine ndani ya kada ya Afya kwa kusababisha chuki kati yao na mgomo baridi utakaoleteleza kuzorotesha huduma ya Afya. Hatua kwa hatua na kwa kasi, Serikali iboreshe maslahi kwa watumishi wake, maana tukisema Sekta ya Afya ni muhimu zaidi, je Walimu wanaopigana kuondoa ujinga na kuzalisha hao wataalamu wa Afya wao si ni bora zaidi? SERIKALI ISIJIINGIZE KATIKA MTEGO WA KUONA KADA NYINGINE NI BORA ZAIDI KWA MAANA KADA ZOTE ZINATEGEMEANA! Mfanyakazi wa TRA si bora zaidi, kuliko mtaalamu wa Afya za Mazingira, Mkemia au mhandisi, Mwanajeshi si bora zaidi Kuliko Daktari, na wala Daktari si bora zaidi kuliko Mwalimu, na Wala WABUNGE si bora kuliko watu wengine. Na kinyume chake ni hivyo hivyo. Tofauti inayoweza kujitokeza, madharani ni kwa kuhamasisha wanafunzi wengi wapende masomo ya Sayansi, hivyo ili linaweza kufanyika kwa wataalamu wa sayansi kupewa motisha na hata ikibidi nje ya mishahara yao. lakini suala la mishahara lazima liwe na kanuni ya uwiano.
Changamoto ninayoitoa kwa serikali kwa siku za mbeleni na kwa hatua za haraka zaidi, pelekeni kwa wingi wataalamu wa kada ambazo zina impacts za moja kwa moja kwenye maisha ya binadamu katika vyombo vya usalama kama vile jeshini, usalama wa Taifa, police na vinginevyo kwa ajili ya emergency wakati wa dharula. Lakini pia maslahi ya wataalamu wetu lazima yaboreshwe.
Nasilisha kwa maslahi ya Taifa
Baki hivyohivyo na maoni yako wala husibadilike na hayo maoni yako ungepeleka wizarani ingekuwa vizuri kwani sie tumejaribu imeshindikana, mgomo wetu upo pale pale hadi hapo JK atakapojua wajibu wake! Hii sio siasa na wala hakuna maandamano.