Mgomo mkubwa wa wahadhiri Ustawi wa Jamii

Tuyuku

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
3,292
1,919
Taasisi ya Ustawi wa Jamii ipo katika hali mbaya sana kutokana na menejimenti mbovu na uongozi mbovu wa serikali ya wanafunzi.

Wahadhiri wa Taasisi hiyo wapo katika mgomo toka Jumatatu wakishinikiza kukutana na waziri mkuu Pinda kutokana na mamlaka zingine kushindwa kutatua matatizo yao sugu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko juu ya uongozi mbovu wa chuo hicho chini ya mapacha watatu. Mapacha hao ni kaimu mkuu wa chuo bwana Madihi, mkurugenzi wa mafunzo bwana Mchovu na mkuu wa utawala na fedha mama Mbonimipango. Mapacha hao watatu wanakiendesha chuo kama taasisi yao binafsi kwa kukithiri kwa ufisadi. Jambo linalohuzunisha zaidi ni kuwa mapacha hao watatu wote kwa pamoja hawana sifa za kuiongoza taasisi hiyo. Wote hawana PhD kama inavyotakiwa kwa taasisi inayotoa shahada. Jamambo linalosikitisha zaidi wanafanya kila jitihada ili shahada iondolewe hapo chuoni ili wao waendelee kuwepo hapo kwa maslahi binafsi.

Taasisi imevurugika kiasi cha kuwa kama chuo cha watu watatu. Wanajivunia kubebwa na katibu mkuu wa wizara ya afya Blandina Nyoni na mwenyekiti wa tume ya mipango ya rais ambaye ni mume wa huyo mama. Huyo mama ni mharibifu sana kwani alishaharibu sana TBC kabla ya kwenda Ustawi wa Jamii.

Tatizo jingine hao mapacha watatu wamemnunua rais wa serikali ya wanafunzi Gelard Simbaya. Rais huyo amehongwa kiwanja akaahidiwa kujengewa na nyumba, alihongwa kwenda kufanya field Ulaya, na ameahidiwa gari ilimradi atetee maslahi yao. Hali hiyo imepelekea uchaguzi wa serikali mpya ya wanafunzi hadi sasa haujafanyika miezi miwili zaidi ya tarehe iliyopaswa kufanyika kwani uongozi wa taasisi unahofu anaweza kuja rais ambaye hatokubaliana nao.

Ubazazi huo wa mapacha watatu umekuwa ukitimua timua ovyo wahadhiri jambo lililowafanya wahadhiri waliobaki kuamua kugoma wakishinikiza kuletwa kwa menejimenti yenye sifa inayozingatia uadilifu na utawala wa sheria.

Kiujumla hali ni mbaya sana ndani ya taasisi hiyo. Wito kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za makusudi ili kuwaokoa wanafunzi ambao ni sehemu ya wapiga kura wao.
 
kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.... Ivo malalamiko hayaasaidii cha msingi jitaidi kamba yako iwe ndefu
 
INASIKITISHA SANA.. tanzania bila CCM INAWEZEKANA! investigation kama hizi zinapaswa ziende kufanyika katika taasisi mbali mbali kwani viongozi ambao hawana na wala hawategemei kumiliki digrii za PhD wameendelea kuongoza na kuwafanya wafanyakazi wao vile wao na CCM inataka!
 
Haya ndio mambo ya nchi hii. hakuna la kutegemea kama wana kifua nyuma yao lakini yote yana mwisho.
 
huyo mchomvu si huwa anarekodi vipindi vya afya ya jamii ITV?

masikini TZ, yaani kwa sababu management haina sifa wanataka chuo cha umma kishushwe hadhi ili sifa zao zitoshe kuendelea na nyadhifa zao? hii nadhani ni mpya kabisa duniani!!
 
Mgomo mkubwa watangazwa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuushinikiza Ungozi wa Taasisi kutimiza madai ya wanafunzi hao ikiwa ni kufundishwa na walimu ambao hata hivyo nao wapo kwenye mgomo na kubwa zaidi kujiuzulu kwa menejimenti ya Taasisi.
 
Wizara ya Afya mko wapi//Dr.Haji Mponda bado uko Ifakara unakula pelege na kitoga nini?
 
Mheshimiwa LEMA unasikia hayo??? Hebu tembelea chuo hicho uwape dozi hao vijana!!! namna ya kulinda maslahi yao!
 
Nchi hii kila mtu ni mjuaji,na haya matatizo yanasababishwa na serikali.kwa nini haitatui matatizn ya managementi nyingi za vyuo?au ndo wizarani wanawekana na kupeana vyeo?
 
kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.... Ivo malalamiko hayaasaidii cha msingi jitaidi kamba yako iwe ndefu

Tatizo ni kwamba MBUZI wengine wanakata kamba na kula kwenye vihamba vyetu......
 
Ivi apa napo wanatoa digrii?mbna ukiwa majuu ata katka orodha ya TCU hakpo?msaada tafadhali
 
Bodi ya magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam imekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo wa wahadhiri wa taasisi hiyo.

Madai ya wahadhiri na wanafunzi ni kutaka uongozi wa taasisi uondoke kwa kuwa hauna sifa zinazotakikana kwa mujibu wa sheria ya Nacte. Hali ilikuwa mbaya sana chuoni hapo lakini wanachuo wamekuwa wastaarabu na kuondoka kwa majonzi wakiwa hawajui hatma yao.

Serikali ya Tanzania inapaswa kulaumiwa kwa mgogoro katika taasisi hiyo kwa kuwa kuna katibu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii anaufuga mgogoro huu kwa maslahi binafsi.

Yana mwisho haya
 
Mi mwenyewe nimejua tu ipo siku hata kuna siku kumbe GERALD amehaidiwa mengi ila wana paka lini lile jengo halikamiliki jamani kile chuo au english medium da
 
garald kasaliti huku akijiita document na akasahau wapo watu mafile na wapo kimya,ndio chuo kimefungwa nawaomba wana taasisi wa ustawi hata chuo kikifunguliwa wahakikishe mapacha watatu wanaondoka kabla ya kurudi chuoni huu ni upuuzi,hapa watu wanafikiri kwa tumbo badala ya kichwa haswaa mchomvu akitaka nyazifa kubwa wakati elimu yake ni ndogo!!!!!!!!!!!!11pumbavu!!!!!
 
Duh chuo kimekuwa kama kariakoo kwakweli tunamkumbuka sana mama tf ngalula km inawezekana ata arudishwe kwa mkataba wa mwaka m1 tu atunyooshee chuo hali ni mbaya sana duuh
 
jamani kwani solution pekee katika hali kama hizi huwa ni kufunga vyuo tu? mbona wanaingiza wanafunzi na wazazi/walezi katika gharama zisizo za lazima?

poleni wadau

Mungu yupo atasikia sala zetu
 
Ivi apa napo wanatoa digrii?mbna ukiwa majuu ata katka orodha ya TCU hakpo?msaada tafadhali
Si vyuo vyote vinavyotoa Degree viko chini ya TCU.TCU ni umoja wa vyuo vikuu tu; hizi Taasisi kama IFM, NMA-kigamboni, CBE, NIT na ISW-Ustawi zote zinatoa Degree na zinatambulika ziko chini ya NACTE.kama kweli we mtu wa kuruka Majuu, tembelea GOOGLE, u-search High Learning Institutions in Tanzania, ISW-Ustawi utakiona kaka, ni Chuo kinachoongoza Tanzania na ukanda wa East Africa na Central kutoa wataalamu 'Pure' wa mambo ya sayansi ya jamii-social workers, mahusiano kazini-industrial relationists-wataalamu wa sheria za kazi.
 
Back
Top Bottom