Mgomo Jambo Plastics! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo Jambo Plastics!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, May 6, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,554
  Likes Received: 18,239
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kumetokea mgomo wa wafanyakazi kiwanda cha Jambo Plastics, Nyerere Rd. Wafanyakazi wameifungia nje menejimenti ya kiwanda, na kutanda lango kuu huku wamebeba mabango mbalimbali waliandika malalamiko yao.

  Miongoni mwa malalamiko hayo, ni kuajiriwa mpaka kipindi cha miaka 10 kama vibarua tuu, bila NSSF, moja ya bango linamtaka Kikwete afukuze kazi waziri wa kazi, huku bango jingine likimtaka Magufuli ndio awe waziri wa kazi.

  My Take!.
  Huu ndio mtindo wa uendeshaji viwanda kwa wawekezaji uchwala ambapo haki za msingi za mfanyakazi ni favours!. Kitakachofuatia hapo ni defender za FFU labda na maji ya upupu!.
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hivi ni lini serikali itaacha kuwaandekeza hawa wawekezaji aka waddekezwaji hasa hawa jamaa zetu wenye asili ya kihindi ni wanyojaji sana .
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nchi ya kitu kidogo...tuwakatae wawekezaji uchwara! wanaojali maslahi yao kuliko uhai wa watu...haiwezekani wakae kwenye ardhi yetu,watutumikishe,tuwalambe miguu na mwishowe tuambulie majeraha ya maisha km tunavyoshuhudia sasa!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hadi kieleweke mwaka huu...halafu hawa watu wanaofanya kazi viwandani huwa wanaonewa sana...nadhani wengi ni hawajui hako zao za msingi na most of them hawana option ya kuishi dar...just ni ajira tu na wengi wao wa chini ya form 4,wanabanwa,wananyonywa all relative staffs. Naona wanaanza kujielewa by the way!!
   
Loading...