Mgomo Baridi wa Matangazo ya Biashara

Mzalendowetu

Member
May 22, 2012
87
34
Wana JF, kwa muda mrefu kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu kutangaza katika jukwaa hili pasipo kuweka taarifa muhimu ya bidhaa husika kama bei, picha, namba za simu na specifications/taarifa zingine muhimu. Hii inapelekea usumbufu kwa pande zote 2 yaani muuzaji na mteja. Naamini kama mtu uko serious na biashara, huwezi kukosa picha za nyumba, gari, kompyuta au bidhaa nyingine yeyote unayouza au kuitangaza.
Ninashauri kuanzia sasa, tuweke mgomo kwa wale wote watakaotoa matangazo yao katika jukwaa hili bila kuweka taarifa muhimu kwa mteja/msomaji. Mgomo wenyewe ni kwamba, kwa tangazo lolote lisilojitosheleza tusijibu kabisa wala kuomba taarifa hizo.
 
Back
Top Bottom