Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

kikubwa nilichokiona hapo magufuli atawekwa tu kama pazia, mimi nasubiria hizo sababu zitakazonishtua ndio nije kuchangia kwa umakini zaidi. asante kwa tetesi.
 
Mgombea awe Bernard, awe Edward, Awe Samuel, awe John hata Harrison wote hao si suluhisho la ufukara, umasikini, ufisadi na matatizo yote tunayokabiliana nayo Watanzania...

Wote hao ni watoto wa baba mmoja wanaojivika tu mavazi tofauti, wote wapo kwa maslahi ya kutetea na kulinda sera na ilani za CCM...

Kama kutatokea mwanadamu atakayeingia kwenye fikra zetu na kubadilisha mitizamo yetu sisi Watanzania basi mtu huyo ndiye atayestahili kuwa kiongozi wa nchi...

Hawa mnaowataja kwao wao jukumu la kwanza ni kutetea chama chao (CCM), pili kutetea maslahi yao halafu tatu na mwisho ndio wanawakumbuka wananchi...

Bahati mbaya sana sisi Watanzania ni watu tusiojitambua, leo tunaweza kuonesha mahaba ya dhati kwa mtu fulani kwa shangwe na vigelegele lakini kitambo kidogo tu kijacho tutamtusi yule bwana tuliyempenda kwa roho na nafsi zetu na kumuona hafai...

Kiongozi akiwajibika kuyafanya yanayomfanya awe kiongoi wa nafasi fulani basi mtu huyo tutamuona Mungu mtu, tutapiga zumari na kupaza sauti kuwa huyu ndiye afaaye kwa kumpamba lakini tunasahau kwamba huyu katimiza tu wajibu wake na sio kwamba kafanya jambo la ziada...

Huwezi kukesha na kulisifia paa la nyumba yako kuwa limekukinga na mvua pamoja na jua, utaonekana mwehu kwa kuwa hizo ndio kazi za paa...lakini utaonekana wa maana kama paa hilo likikukinga na tufani ya kimbuka na dhoruba maana hapo limefanya kazi ya ziada.

Uwajibikaji thabiti pekee wa kina John, Edward, Bernard hauwafanyi kuwa ndio watu stahiki kwa uongozi wa nchi, uongozi wa nchi una zaidi ya kutimiza majukumu.

Hebu tujiulize hali za majimbo ya uchaguzi za hawa mabwana zikoje, wamefanya nini huko majimboni mwao, wametatua kero zipi, wamekuwa madarakani kwa nafasi za ubunge kwa muda gani...?

Ngoja niishie hapa....
 
This is a figment of your own imagination; na hiyo source yako imekwambia njozi zake tu kulingana na vested interests zake kisiasa; CCM ni taasisi kubwa yenye factions nyingi zenye interests tofauti tofauti ambazo lazima zipitie mizengwe na minyukano mingi kabla ya kufikia uamuzi! kumbuka a week in politics is a very very long time! Ukianza kuamini sasa hivi kwamba John "Pombekali" Magufuli ndie atakuwa mgombea wa CCM come 2015; that is too far fetched!!!
 
Kitabu cha siri ndani ya CCM kinasema " ni haramu kafiri (mkristo) kuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM. Mi sishangahi kuona Magufuli ndo mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM ila watambue kuwa nchi hii haina dini, kabila, wala kanda.Nchi ni yawote...
Jiulize je! Katika historia ya Tanzania kashatokea mgombea uraisi mkristo kwa tiketi ya CCM?
Waache ujinga tuijenge nchi.
una muda gan haupo dunian mana naona ww ni mgen
 
Watu hawazingatii kabisa N.B ya mtoa mada naona hoja zinapishana hapa wakati mtoa post/Thread kashauri "usome na utoke kimyakimya"

Aaah, nilikuwa nawakumbusha tu ushauri wa ndugu Pasco ngoja mi nizingatie nitoke kwa mtindo huo aki-confirm nitakuja hapa Mazima.!!

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom