Mkuu Mungi,
Hayo ni mawazo ya watu wa Kiboriloni wanayompa huyu kijana baada ya kuona aibu inayompata. Fikiri, watu wanaokusanywa kwenye mikutano yake yoote wanabebwa na hiace kutoka mbali kata za Pasua, Bomambuzi na mjini kati. Wanaletwa kwa makubaliano kwamba watapewa buku 10 kila mkutano. Kwa taarifa yako, mgombea huyo ameweka mawakala wake wananunua kadi za wapiga kura kwa buku 10 kwa mapatano kuwa zitarudishwa J3 asubuhi ili kupunguza idadi za CDM. Kata hii ni motoooo.
Ndiyo maana watu wanamwambia ajitoe tuu. Mh. Mwanri kafika hapa na uswahili wake woote, anafurahi kuona watu mbele yake, sijui kama anajua kuwa si wakazi wa kata husika. Tuombe Mungu, kesho saa 12 jioni tunaanza kujiandaa kumtawaza diwani wetu. CCM hawajafanya lolote hapa tangu miaka 37 iliyopita, leo wanagawa mahindi na nyama Poleni ccm