09 Agosti 2022
Kakamega, Kenya
MGOMBEA URAIS PROF. WAJACKOYAH ASHINDWA KUPIGA KURA, SABABU VIFAA VYA KURA KUSHINDWA KUFANYA KAZI
Mgombea urais Prof. George Wajackoyah ahuzunishwa kushindwa kupiga kura, vifaa vya KIEMS vinahitilafu
Mgombea urais Prof. George Wajackoyah ambaye mapema leo alitazamia kupiga kura kama wale wenzie 3 wanaogombea urais ktk uchaguzi mkuu wa Kenya, ameshindwa kutumia nafasi hiyo ya haki ya kiraia kutokana na hitilafu ya vifaa vya kuwezesha kupiga kura.
Akiongea kwa masikitiko akiwa ameongozana na mkewe, amesema ikiwa yeye mgombea urais ameshindwa kupiga kura leo mapema asubuhi huku jitihada zikifanyika afanikiwe kufanya zoezi hilo muhimu la kidemokrasia je wale watu wa umri wake wanaweza kweli kungojea siku nzima ili kupiga kura? Katika eneo lake raia wengi wa umri wake wameamua kurudi nyumbani na labda hawatapa nafasi ya kupiga kura.
Prof. George Wajackoyah alipohojiwa atachukua hatua gani, amesema hana la kufanya bali kuamini kauli za mainjinia wataalamu kuwa ni jambo la kiufundi na yeye ni mwanasheria, hivyo anavuta subira kuona kitachofuata.
Prof. George Wajackoyah anasimama kupitia tiketi ya chama cha ROOTS Party kugombea nafasi ya kuchaguliwa na wananchi wa Kenya kuwa rais kama atafanikiwa kupata kura za kutosha.