Kenya 2022 Mgombea Urais Prof. George Wajackoyah ahuzunishwa kushindwa kupiga kura, vifaa vya KIEMS vina hitilafu

Kenya 2022 General Election

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,038
23,827
09 Agosti 2022
Kakamega, Kenya

MGOMBEA URAIS PROF. WAJACKOYAH ASHINDWA KUPIGA KURA, SABABU VIFAA VYA KURA KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Mgombea urais Prof. George Wajackoyah ahuzunishwa kushindwa kupiga kura, vifaa vya KIEMS vinahitilafu



Mgombea urais Prof. George Wajackoyah ambaye mapema leo alitazamia kupiga kura kama wale wenzie 3 wanaogombea urais ktk uchaguzi mkuu wa Kenya, ameshindwa kutumia nafasi hiyo ya haki ya kiraia kutokana na hitilafu ya vifaa vya kuwezesha kupiga kura.

Akiongea kwa masikitiko akiwa ameongozana na mkewe, amesema ikiwa yeye mgombea urais ameshindwa kupiga kura leo mapema asubuhi huku jitihada zikifanyika afanikiwe kufanya zoezi hilo muhimu la kidemokrasia je wale watu wa umri wake wanaweza kweli kungojea siku nzima ili kupiga kura? Katika eneo lake raia wengi wa umri wake wameamua kurudi nyumbani na labda hawatapa nafasi ya kupiga kura.

Prof. George Wajackoyah alipohojiwa atachukua hatua gani, amesema hana la kufanya bali kuamini kauli za mainjinia wataalamu kuwa ni jambo la kiufundi na yeye ni mwanasheria, hivyo anavuta subira kuona kitachofuata.


Prof. George Wajackoyah anasimama kupitia tiketi ya chama cha ROOTS Party kugombea nafasi ya kuchaguliwa na wananchi wa Kenya kuwa rais kama atafanikiwa kupata kura za kutosha.
 
09 Agosti 2022
Nairobi, Kenya

Wagombea wakuu wa uchaguzi wa urais Kenya wapiga kura​

5 hours ago​

62753746_101.jpg


Wagombea wakuu wa uchaguzi wa urais nchini Kenya wameungana na wananchi wengine wa taifa hilo la Afrika Mashariki kupiga kura na kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.​

Mgombea urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga amepiga kura asubuhi ya leo katika kituo cha Old Kibera, jijini Nairobi. Raila ambaye ni mwanasiasa mkongwe, alikuwa ameongozana na mkewe, Ida Odinga.

Kwa upande wa naibu rais wa Kenya, William Ruto mwenye umri wa miaka 55, ambaye pia ni mgombea urais kupitia muungano wa Kenya Kwanza, yeye amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Kosachei iliyoko katika eneo la Eldoret Kaskazini, kaunti ya Uasin Gishu, Bonde la Ufa
62752555_101.jpg


Raila Odinga, mgombea urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja akipiga kura
Wagombea wengine wanaowania kiti cha urais ni George Wajackoyah wa chama cha Roots na David Mwaure wa chama cha Agano.

Source : Wagombea wakuu wa uchaguzi wa urais Kenya wapiga kura | DW | 09.08.2022
 
9 Agosti 2022

UCHAGUZI MKUU KENYA 2022

Kaunti 47 na sub kaunti 295 za Kenya. Raia wa Kenya leo 9 Agosti 2022 wanaenda ktk vituo vya kura kuchagua rais atakayeiongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maseneta, gavana, wabunge na madiwani (mca).

RAMANI YA KENYA : Kaunti 47 za nchini Kenya mgawanyo kijiografia

1660060141800.png






Sub counties 295
Source : https://www.researchgate.net/figure...-295-sub-counties-numbered-The_fig1_343047955
1660060241853.png


The map of Kenya showing 47 counties (colored) and 295 sub-counties (numbered). The extents of major lakes and the Indian Ocean are shown in light blue. The names of the counties and sub-counties corresponding to the displayed numbers are presented in Additional file 1. Source: author generated map​

 
09 Agosti 2022
Nairobi, Kenya


Hakuna Kura Ya Ugavana Mombasa, Kakamega Leo​


NA WAANDISHI WETU

WAKAZI wa Kauti za Mombasa na Kakamega watalazimika kusubiri muda mrefu zaidi kabla kuchagua magavana wapya.


Hii ni baada ya karatasi za kura za nyadhifa hizo kukosekana hapo jana Jumatatu.

Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Jumatatu walikuwa mbioni kurekebisha hali hii lakini baadaye, mwenyekiti, Bw Wafula Chebukati akasema imeamuliwa chaguzi hizo ziahirishwe hadi wakati mwingine utakaotangazwa baadaye.

Vilevile, Bw Chebukati alitangaza tume IEBC imeahirisha chaguzi za ubunge Kacheliba na Pokot Kusini.

Uchaguzi wa viongozi wengine katika maeneo hayo utaendelea ilivyopangiwa.

Wakati wa kufungua makasha ya karatasi za kura, ilibainika kuwa karatasi za ugavana zilizopokewa Mombasa zilikuwa ni za uchaguzi wa Kaunti ya Kilifi.
Makasha mawili yaliyofunguliwa katika kituo cha kujumuisha kura za eneobunge la Mvita kilicho Shule ya Upili ya Alidina Visram, yalibainika kuwa na vijitabu ambavyo vilinakiliwa kuwa vya uchaguzi wa ugavana Mombasa lakini ndani, karatasi zikawa na picha za wagombeaji ugavana wa Kilifi.

Taharuki ilitanda kwa muda huku maajenti wa wagombeaji ugavana wakitaka majibu kutoka kwa IEBC.

“Naomba tuwe watulivu. Bado kuna wakati wa kulirekebisha. Ni kosa dogo ambalo linaweza kufanyiwa marekebisho,” alisema Msimamizi wa Uchaguzi wa eneobunge la Mvita, Bw Sudi Masha.

Makasha yaliyofunguliwa katika kituo cha uchaguzi kilicho Shule ya Msingi ya Mikindani, eneo bunge la Jomvu, na katika kituo cha eneo bunge la Kisauni pia yalipatikana kuwa na karatasi za ugavana za Kilifi.

Mkuu wa uchaguzi wa eneo bunge hilo, Bi Husna Hassan, alisema wakuu wa IEBC wangetoa taarifa baadaye kuhusu suala hilo.

Mkuu wa IEBC katika eneo bunge la Magarini, Kaunti ya Kilifi, Bi Aisha Abubakar, alithibitisha hawakuwa wamepokea karatasi za ugavana za kaunti hiyo asubuhi.

Hali sawa na hii ilishuhudiwa katika Kaunti za Kakamega na wadi ya Chuka/Igambang’ombe iliyo Kaunti ya Tharaka Nithi.
Katika Kaunti ya Kakamega, afisa mkuu wa uchaguzi, Bw Joseph Ayata, alithibitisha karatasi za kura za ugavana zilizopokewa zilistahili kuwa za Kaunti ya Kirinyaga.

Mkuu wa uchaguzi katika Kaunti ya Tharaka Nithi, Bw Mohamed Raka, alithibitisha karatasi za uchaguzi wa udiwani za Fafi, Kaunti ya Garissa, zilikuwa zimepatikana Chuka / Igambang’ombe.

Vilevile, Bw Raka alisema karatasi za uchaguzi wa udiwani wa Wadi ya Mugwe, Kaunti ya Tharaka Nithi, zilikuwa zimepatikana Kaunti ya Garissa.
Akizungumza mjini Mombasa, mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea binadamu la Haki Africa, Bw Hussein Khalid, aliondolea lawama a IEBC akisema upakiaji hufanywa kule ng’ambo ambapo karatasi huchapishwa na hazifunguliwi hadi zifike hapa.
Katika Kaunti ya Lamu, IEBC jana ilianza kusafirisha vifaa vya kupigia kura na makarani hadi maeneo ya msitu wa Boni na maeneo yanayopakana na Somalia kwa kutumika helikopta.

Mkuu wa IEBC katika Kaunti ya Lamu, Bw Maro Ade, alisema tume hiyo ilikuwa tayari imefikisha helikopta ambayo itakuwa ikikaa mjini Faza ili kusambaza vifaa na wahudumu hadi maeneo yaliyo na changamoto za usafiri na usalama katika kipindi chote cha uchaguzi.
Source : Hakuna kura ya ugavana Mombasa, Kakamega leo – Taifa Leo
 
Kakamega:
Ruto 3422
Raila 16

Kericho:
Ruto 1255
Raila 143

Kiambu nyeri:
Ruto 1028
Raila 344

Kisii:
Ruto 870
Raila 85
 
TAYARI WAMESHAFANYA YAO, KUNA WATU WATAFAIDIKA NA MKWAMO WA KIFAA KTK ENEOBUNGE / URAIS

What is extreme gerrymandering?

Gerrymandering describes the intentional manipulation of district boundaries to discriminate against a group of voters on the basis of their political views or race.

The term dates to 1812 when Massachusetts Governor Elbridge Gerry signed into law a redistricting plan that included a district many thought looked like a salamander, leading opponents to nickname the district after him.

But while the term has become a synonym for redistricting abuses, it actually covers a wide variety of sins, not all of which are related.
1660216058966.png

Photo and report from NYTimes source: Maps in Four States Were Ruled Illegal Gerrymanders. They’re Being Used Anyway.


For example, one form of gerrymandering involves drawing districts in order to protect incumbents. Likewise, sometimes districts are drawn to ensure a favored candidate can successfully run for office. These types of gerrymanders – which often occur through bipartisan collusion between political parties – can be harmful to democracy by pre-determining outcomes and depriving voters of a meaningful choice at the polls. READ MORE : What Is Extreme Gerrymandering?
 
09 Agosti 2022

Uchanganuzi wa uchaguzi mkuu 2022 nchini Kenya huku shughuli ya kuhesabu kwa kura ikianza.

Waliojitokeza wanatarajiwa kufikia 60%, ambayo ni idadi ndogo ya wapiga kura waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura.




Nini imesababisha 2022 kufeli kupata idadi kubwa ya watu kujitokeza kupiga kura katika historia ya chaguzi za Kenya.


Ni watu kukata tamaa ya kutokuwepo elimu ya uraia kuwapa watu imani kuwa kutakuwepo uchaguzi ulio huru, haki bila madubwasha ya vifaa vya kura kushindwa kufanya kazi au vifaa kupelekwa kusiko na baadhi ya maeneobunge, maeneokaunti kushindwa kupiga kura mapema leo n.k n.k
 
09 Agosti 2022

Mwenyekiti wa IEBC bw. Chebukati anaeleza kuwa vituo vya kura vimefungwa


Mwenyekiti wa IEBC anafafanua utaratibu unaofuata wakuwakilisha kura za urais, u-gavana, u-seneta na udiwani.

Kura zitakazotangazwa ktk vituo vya kupiga kura baada ya kuthibitishwa na waangalizi ktk vituo ndiyo zitakazo tambuliwa na kuwa hazitaweza kurekebishwa nje ya vituo hivyo.

Kura za jumla za urais zitatangazwa na makao makuu ya IEBC ndani ya siku 7 mara baada ya kukamilisha uchaguzi.

Zile za u-gavana, u-seneta, u-bunge na udiwani zitatangazwa na kubandikwa ktk kuta za matangazo za vituo 46,233 vya kupigia kura vilivyopo ktk eneochaguzi husika, ambavuo vimesambaa nchi nzima ya Jamhuri ya Kenya.
Source : Citizen TV Kenya
 
12 August 2022

LIVE / MUBASHARA

#Decision2022: Provisional results for the presidential race across the country



Source : Nation
 
Zimebaki siku chache tunzeni hii quotes mlete mrejesho.Ipo hivi duniani nzima ikiwemo serikali zote za duniani zipo chini ya nguvu za mamlaka ya watawala wa ulimwengu usioonekana, chochote kabla hakijafanyika ktk ulimwengu wa macho tayari kilishafanyika au afikiwa ktk ulimwengu usioonekana.
Uwe unataka utaki unakubali ukubali sisi sote tunaongozwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wetu ambazo zipo ktk ulimwengu wa siri.
Kama serikali tu inawatambua wazee mfano wazee wa Dar ukadhani ni wazee as wazee sababu ya mvi au umri upo nyuma upo wrong,wale ni watu wazito Sana katk ulimwengu ulionekana wapo physical kuwakilisha wakuu wa ulimwengu usioonekana.
Ni SAwa na vatican, vatican si kama vatican ni zaidi ya vatican,thus wakuu wote wa duniani bila kujali dini ni lazima wasalute kwa Pope. Raila Odinga alimshinda UHURU uchaguzi uliopita akawa ajakubaliana masharti ya wakuu wa dunia thus akachezewa mchezo akapewa UHURU, Then anaitwa akaitwa akayakubali masharti thus anachukua this time hata Kenyatta analijua hili ndo maana kaamua kuwa upande wa Raila.
Kwann kambi ya Raila itashinda.
1.Wakenya wamechoka kutawaliwa na kabila/ ukanda mmoja miaka yote, wanataka kubadilisha ladha.
2.Kambi ya Odinga ni strong Ina wagombea smart na wameshauzika miaka mingi sana yaani Odinga na Martha Karua kuliko kambi ya Ruto pia ni wanasiasa mahiri na ni wachapa Kazi wakenya wanaona watavusha na sio ile kambi ya mafisadi.
3.Kambi ya ODIMA yaani Martha na Odinga Ina makampeni meneja smart na makini Sana kuliko kambi ya Ruto.
4.Ruto anajibomboa mwenyewe kwa kauli zake za chuki na visasi na ukosefu wa nidhamu.
5.Ruto ana visasi hana utulivu wa akili yaani sio matured and civilized enough kuongoza nchi,kiburi mjuaji mapepe yaani saikolojia yake haijabalance bado kulinganisha na Odinga,pia ni dictator hofu atawaletea machafuko wa Kenya.
6.Wakuu wa duniani hawawezi ruhusu hayawani aingie ikulu, Kenya ni muhimu Sana kama base ya kucontrol East, and Central Afrika ikiwemo Ghuba ya Aden. Utulivu wa Kenya ni muhimu Sana kwa interest zao.
7.Katika ulimwengu usioonekana wao chaguo lao ni Odinga kwa maana ni rahisi kumcontrol kinyota na sio Ruto yeye hayupo kabisa kwenye radar zao.

Wiki ijayo sio mbali tunzeni post hii.RAILA AMORO ODINGA ndie next president wa Kenya.Upige kura usipige kura tayari wakubwa wa Dunia walishapanga Odinga.

Ruto is another dictator Arap Moi.
 
Ili kumtangaza mgombea wa urais kuwa mshindi,lazima;
  • Apate asilimia 50+1 ya kura zote zilizopigwa
  • Apate asilimia 25 ya kura katika Zaidi ya nusu ya kaunti zote 47 nchini.
Endapo hakuna atakayeshinda kura kuafikiwa vigezo hivyo,basi italazimu Tume ya uchaguzi kuandaa duru ya pili ya kura
Ikiwa hakuna mgombea aliyechaguliwa, uchaguzi mpya utafanyika ndani ya siku thelathini baada ya uchaguzi uliopita na katika uchaguzi huo mpya wagombea pekee watakuwa;
(a) mgombea, au wagombea, waliopata kura nyingi zaidi; na
(b) mgombea, au wagombeaji, waliopata idadi kubwa ya pili ya kura.

Source : Independent Electoral and Boundaries Commission
 
12 August 2022

LIVE / MUBASHARA

Kenya Elections 2022 Live Results Reporting.

 
12 August 2022

‘Do not panic,’ Chebukati explains difference in Presidential results across TV stations

 
12 August 2022
Nairobi, Kenya

Azimio team claims to have busted a votes-rigging racket in Nairobi



Source : Citizen TV Kenya
 
13 August 2022

Kalonzo Musyoka's speech at the Azimio elected leaders meeting​

 
13 August 2022
Nairobi, Kenya

Martha Karua: If you add Mombasa and Kakamega you will see we have strength around the country​




Speaking before the Azimio member-elected leaders , She added that Kenyans gave us opportunity to steer the nation ...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom