Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameshapatikana

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameshapatikana

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameishapatikana

Mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ambae atapeperusha bendera yachama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ameisha patikana, ila bado tukumshauri na kumwomba akubali kugombea, kazi hiyo inafanywa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wenye busara na ushauri wa kutosha.
Sifa zamgombea huyo:


  1. Anakubalika na vyama vyote,ataliunganisha taifa hili ambalo akina Lowassa wamelisambaratisha na makundi yao.
  2. Ni mweledi
  3. Hana makundi
  4. Hana harufu yoyote ya ufisadi
  5. Ni mcha mungu
  6. Anakubalika sehemu zote za JMT,Tanzania bara na visiwani, anakubalika na dini zote hata wapagani
  7. Ana uzoefu wa kutosha na kupitilizawa uongozi
  8. Hajawahi kuomba wala kupokea rushwatangu azaliwe
  9. Ni kiongozi wa mfano(role model) tokakatika familia yake hadi sehemu za kazi
  10. Anakubalika kimataifa
  11. Ni kiongozi safi ambae watu wanamkubali, ndege angani wanamkubali,hata wanyama polini tembo faru watakuwa salama ndani ya uongozi wake

Chama cha mapinduzi si chama cha wapumbafu kiasi ati wawachague sijui Membe, Sijui Sitta, Sijui Ngulu Nchemba, Sijui Wassira ambao tayari wana wakundi wapeperushe bendera yake, Chama Cha Mapinduzi kimefanya busara zake zote kumshauri mgombea mtarajiwa achukue form. Muelewe CCM mgombea wake huyo ameombwa agombee, siyo amejipigia debe kama wengine.

Tusubiri tuone

EE Mungu ibariki Tanzania, tuondokane na jinamizi hili.
 
Wewe huijui CCM, iliyejipanga vizuri zaidi ndiye atakayepitishwa wengine ni wasindikizaji tu.
 
Ccm hakiwezi kuwa na mgombea mhuni mwizi na asiye mwadilifu hili lipo wazi kwa kila mtu na hata wagombea wenyewe wanajua hayo.
 
Zanzibar-ASP, Siyo kweli acha kuishi kwa mazoea bana utaumbuka mapema sana.
 
Last edited by a moderator:
Fisadi amewafisad nn?? Msiwe mnaongea bila ushahidi. Goa ushahidi watu wakusuport lakini sio Mara jinamizi Mara fisad hiyo yote ni mipasho ya kike,. We Kama unajiamini unaikweli WA unayoyaongea toa uthibitisho
 
Huyo Atakuwa Dr Salim Ahmed Salim,ndo Anakubalika Na Vyama Vyote,hana Makundi,hana Makuu,si Fisadi,hana Tamaa Ya Kwenda Ikulu,hana Udini,kwa Jinsi Baadhi Ya Waislamu Walivyo Wajinga,watadhani Kuwa Ujio Wa Dr Salim,(kama Atagombea) Ndo Mahakama Ya Kadhi Itakuwepo,hakuna Mahakama Ya Kadhi Tanzania Hata Kama Watatawala Waislam 50.
 
Wengine umewataja mtaje na huyo mpya ili kama anakidhi hivyo vigezo tumfuate na kumwomba.
Ila ana kadi ya chama?
Tukimkuta nayo awe ameikata hivi karibuni lakini kama atakuwa mwanachama mkongwe tuna maswali zaidi ya kumuuliza!TAFADHALI MTAJE!!
 
Hayo unayoyasema yaweza kuwa kweli. Kikubwa tuunganishe nguvu zetu ktk maombi bila kujali itikadi zetu za kisiasa au kidini.
 
Tatizo watu Bado hawajui tu ila ukweli ni kwamba Rais ajae ni Pinda najua watu watabisha sana ila ukweli ndio huo, Pinda alikuwa hana mpango na Urais ila Marais wastaafu ni aliepo madarakani ndio walio mshawishi agombee ngoja Muda ufike ndio mtakumbuka maneno yangu
 
Tatizo watu Bado hawajui tu ila ukweli ni kwamba Rais ajae ni Pinda najua watu watabisha sana ila ukweli ndio huo,Pinda alikuwa hana mpango na Urais ila Marais wastaafu ni aliepo madarakani ndio walio mshawishi agombee ngoja Muda ufike ndio mtakumbuka maneno yangu
Kauli zilizopinda na zisizohahika kutoka kwa Pinda ni udhaifu wa wazi unaomwondelea sifa!
Hakika hawezi kujisimamia wala kujisimamia!
 
Hamnaga mtu wa hivi aliyeko CCM,
 
Kuna Mzee & Kada mmoja ambaye yuk karibu sana n Msuya alinidukulia Story hii December mwaka jana (2014).

Sasa naweza nikaamini habari hii. Kwa umri wake,siamini kama anaweza akawa na account humu JF. Naamini ebaeban nawe umezipata habari hizi(perhaps more accurately zaid yangu).

Kwa UZI huu, naamini si mwingine. Ni PINDA.(Sorry kwa hili Wadau humu ndani). Nimesema kile ninachokiamini juu ya Thread hii).
 

Attachments

  • 1423464351023.jpg
    1423464351023.jpg
    38.7 KB · Views: 1,135
Last edited by a moderator:
ndani ya CCM ya sasa huwezi kumpata mtu mwenye sifa hii.

Ni kweli ndani ya CCM hii mtu huyo hayupo, ila uelewe kwamba mtu huyo ameombwa agombee, mtu anayeombwa anaweza kukatiwa kadi kwa madhumuni maalumu, CCM ilichaangalia hapa ni watu wote wanufaike na rais ajae, siyo kikundi cha watu.
 
Kuna Mzee & Kada mmoja ambaye yuk karibu sana n Msuya alinidukulia Story hii December mwaka jana (2014).

Sasa naweza nikaamini habari hii. Kwa umri wake,siamini kama anaweza akawa na account humu JF. Naamini #ebaeban nawe umezipata habari hizi(perhaps more accurately zaid yangu).

Kwa UZI huu, naamini si mwingine. Ni PINDA.(Sorry kwa hili Wadau humu ndani). Nimesema kile ninachokiamini juu ya Thread hii).
watu wa kulia lia hawana nafasi 2015.
 
Wengine umewataja mtaje na huyo mpya ili kama anakidhi hivyo vigezo tumfuate na kumwomba.
Ila ana kadi ya chama?
Tukimkuta nayo awe ameikata hivi karibuni lakini kama atakuwa mwanachama mkongwe tuna maswali zaidi ya kumuuliza!TAFADHALI MTAJE!!

Asante sana mkuu,amemfagilia sana lkn hamtaji!!weka jina lake atuambie hiyo kadi kaipata lini.
 
Dreamz za Mchana...angalia usije ota unataga!!! Itoshe kusema;- Yeyote mwenye kushirikiana na Jambazi na yeye pia ni Jambazi tu! Hakuna namna ya kumtenganisha...
 
Back
Top Bottom