Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameshapatikana

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 ameshapatikana

watu wa kulia lia hawana nafasi 2015.

Mh! Kwamba unaweza kumzuia PINDA just for a simple criticism like that?

Any ways, kila mtu anaAkili yake. Umetumia haki yako ya msingi kutoa yale uliyonayo. Twende kazi........
 

Attachments

  • 1423465374493.jpg
    1423465374493.jpg
    23.3 KB · Views: 982
Mkuu ebaeban, CCM ni chama cha watu na sio chama cha mtu au kikundi fulani cha watu, kilichopatikana sio mgombea, bali ni sifa tuu za mgombea CCM wanayemwitaji!. Huwezi kusema mgombea wa CCM ameishapatikana, kwa sababu kugombea kupitia CCM is a process, hatua ya kwanza ni kutangazwa kwa utaratibu, kisha kipenga kipulizwe!, kuna kuchukua fomu, kutafuta wadhamini, kurudisha fomu, vikao vya mchujo vifanyike, majina yaende CC huko watachujwa yabaki majina 5, yatapelekwa NEC watakata majina mawili na kubakiza matatu, yatakayokwenda Mkutano Mkuu ambao yatapigiwa kura na ndio utaibuka na jina moja la mgombea!.

So far, hakuna process yoyote iliyofanyika, hivyo hakuna mgombea yoyote wa CCM aliyepatikana!.

Kinachoendelea CCM ni mafisadi tuu fulani wa kisiasa, wenye wivu na husda dhidi mgombea kipenzi cha watu, hivyo wakaja na mgombea wao wa kuchonga, ambaye ni kweli sifa zote ulizozitaja hapo juu anazo!, tatizo la mgombea huyo ni ana jina tuu, lakini sio mwana siasa!, ni mlevi wa kupindukia na hajatulia!, kikubwa kuliko vyote ni mwepesi kama ubua, au kama unyoya wa kifaranga, ukimpuliza tuu kwa kiupepo, umemdondosha!, kama kweli CCM itampitisha huyu, na kipenzi cha watu, ule Mwamba wa Kaskazi ukasimama UKAWA, October, wapinzani wanatinga rasmi Ikulu ya magogoni!.

Walianza na zengwe la vua gamba, likashindikana!, wakaja na zengwe la kuanza kampeni mapema!, likaja zengwe la ukiukwaji maadili!, likapikwa zengwe la tunamtaka kijana!, likapikwa 2015 ni zamu ya mwanamke!, mara ni zamu ya Zanzibar, mara hivi mara vile!, yote hayo yatapita, kweli tupu ndiyo itakayosimama!.

CCM imsimamishe yoyote kwa merits na kihalali, vinginevyo hili la kuja na zengwe la wagombea wao wa kuchonga, halikubaliki, nakuhakikishia mwaka huu, CCM wakileta zengwe!, patachimbika!.

Pasco
 
Last edited by a moderator:
Mh! Kwamba unaweza kumzuia PINDA just for a simple criticism like that?

Any ways, kila mtu anaAkili yake. Umetumia haki yako ya msingi kutoa yale uliyonayo. Twende kazi........
Kiongozi anayejijua kashindwa kufanya haya ili hali ana nafasi - basi hatufai hata kidogo.
1 Mapigano ya wakulima na wafugaji
2. Mgawo usio wa haki hasa katika suala la ardhi kati ya wawekezaji vs wazawa hence kuleta migogoro kati yao.
3. Kushabikia u-chama na si utaifa - hence kuleta mgawanyiko kati ya watanzania walio wamoja tangu uhuru.
4. Vita madawa ya kulevya
5 Wizi wa mali za umma - Hasa suala la ESCROW
 
Kama hizo ndizo sifa za mwana ccm anayefaa kuwa rais basi hakuna anayefaa kutoka chama hicho. Mwaka huu jiandaeni tu kukabidhi madaraka kwa amani kabisa.
 
Tatizo watu Bado hawajui tu ila ukweli ni kwamba Rais ajae ni Pinda najua watu watabisha sana ila ukweli ndio huo,Pinda alikuwa hana mpango na Urais ila Marais wastaafu ni aliepo madarakani ndio walio mshawishi agombee ngoja Muda ufike ndio mtakumbuka maneno yangu
Sio Rais ajae sema mgombea kwa tiketi ya ccm, hayo matazamio yenu kana kwamba mnapeana nchi hii kama yenu wenyewe yatawaponza.
 
kungekuwa na mtu wa sifa hizo ndani ya ccm lazima angekuwa ameshashauri kupiga vita ufisadi,
 
Je anaupeo kwenye masuala ya uchumi wa ndani na wakimataifa.? Uchumi imara ndiyo kinga ya unyanyasaji kutoka WB,EU, IMF, US,na wafuasi wao. Mpimeni huyo kama anaupeo katika masuala hayo.
 
Mkuu ebaban, CCM ni chama cha watu na sio chama cha mtu au kikundi fulani cha watu, kilichopatikana sio mgombea, bali ni sifa tuu za mgombea CCM wanayemwitaji!. Huwezi kusema mgombea wa CCM ameishapatikana, kwa sababu kugombea kupitia CCM is a process, hatua ya kwanza ni kutangazwa kwa utaratibu, kisha kipenga kipulizwe!, kuna kuchukua fomu, kutafuta wadhamini, kurudisha fomu, vikao vya mchujo vifanyike, majina yaende CC huko watachujwa yabaki majina 5, yatapelekwa NEC watakata majina mawili na kubakiza matatu, yatakayokwenda Mkutano Mkuu ambao yatapigiwa kura na ndio utaibuka na jina moja la mgombea!.

So far, hakuna process yoyote iliyofanyika, hivyo hakuna mgombea yoyote wa CCM aliyepatikana!.

Kinachoendelea CCM ni mafisadi tuu fulani wa kisiasa, wenye wivu na husda dhidi mgombea kipenzi cha watu, hivyo wakaja na mgombea wao wa kuchonga, ambaye ni kweli sifa zote ulizozitaja hapo juu anazo!, tatizo la mgombea huyo ni ana jina tuu, lakini sio mwana siasa!, ni mlevi wa kupindukia na hajatulia!, kikubwa kuliko vyote ni mwepesi kama ubua, au kama unyoya wa kifaranga, ukimpuliza tuu kwa kiupepo, umemdondosha!, kama kweli CCM itampitisha huyu, na kipenzi cha watu, ule Mwamba wa Kaskazi ukasimama UKAWA, October, wapinzani wanatinga rasmi Ikulu ya magogoni!.

Walianza na zengwe la vua gamba, likashindikana!, wakaja na zengwe la kuanza kampeni mapema!, likaja zengwe la ukiukwaji maadili!, likapikwa zengwe la tunamtaka kijana!, likapikwa 2015 ni zamu ya mwanamke!, mara ni zamu ya Zanzibar, mara hivi mara vile!, yote hayo yatapita, kweli tupu ndiyo itakayosimama!.

CCM imsimamishe yoyote kwa merits na kihalali, vinginevyo hili la kuja na zengwe la wagombea wao wa kuchonga, halikubaliki, nakuhakikishia mwaka huu, CCM wakileta zengwe!, patachimbika!.

Pasco

Huyounayesema ni kipenzi cha watu ni nani? Na hao wanaomtukuza ni akina nani ?

Kuna watu wanaomfagilia huyo unayesema ni kipenzi cha watu ati mwamba wa kaskazinikwa manufaa yao binafi, CCM haiko teyari kumpitisha mtu ambae watu wanawekezakwake, mfano hai mbunge mmoja amefirisika kabisa hadi mali zake kupigwa mnadana CRDB banki, eti mbunge huyo kawa wakala wa
mwamba wa kaskazini nia na madhumuni amwezeshe ukwasi ambaoutamwezesha kukomboa mali zake, kufirisika kwa mbunge huyo kumetokana nakuendekeza mambo ya anasa, utampata binti mrembo LULU hivi hivi tu bila kifocha pesa?

Eti CCM imempate mgombea ambae atawawezesha watu kufikia ndoto zao,sorry.
Pasco sorry, hata kama mgombea mtarajiwa ni mwepesi ataimarishwa tu, UKAWA hawana nafasi kabisa na mgombea huyo aliyechafuka, sabuni ya kumsafishiani gharama kubwa mno.
 
Last edited by a moderator:
Pasco ninakuomba funguka zaidi. Mtaje huyo wao, wenyewe si wameogopa kumtaja?
 
Last edited by a moderator:
Ninaona CCM baada ya kuzunguka kote na kuona chama chao chote ni kichafu raundi hii wanataka kuwahadaa waTZ kwa kutaka kutuletea Jaji Augustino Ramadhani... Ila ninashukuru kuona waTZ wa sasa wameelimika na kugundua janja yao mapema... So nyie CCM hata mlete nani watu washawashitukia saa hvi UKAWA hata waweke jiwe wanachi watalichagua hilo hilo jiwe kuliko kuchagua mgombea wa CCM kwa kuwa wameshafahamu kuwa wagombea wa CCM wote ni ukoo wa panya tu
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015ameisha patikana
Mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ambae atapeperusha bendera yachama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ameisha patikana, ila bado tukumshauri na kumwomba akubali kugombea, kazi hiyo inafanywa na wanachama waChama Cha Mapinduzi wenye busara na ushauri wa kutosha.
Sifa zamgombea huyo:


  1. Anakubalika na vyama vyote,ataliunganisha taifa hili ambalo akina Lowassawamelisambalatisha na makundi yao.
  2. Ni mweledi
  3. Hana makundi
  4. Hana harufu yoyote ya ufisadi
  5. Ni mcha mungu
  6. Anakubalika sehemu zote za JMT,Tanzania bara na visiwani, anakubalika na dini zote hata wapagani
  7. Ana uzoefu wa kutosha na kupitilizawa uongozi
  8. Hajawahi kuomba wala kupokea rushwatangu azaliwe
  9. Ni kiongozi wa mfano(role model) tokakatika familia yake hadi sehemu za kazi
  10. Anakubalika kimataifa
  11. Ni kiongozi safi ambae watu wanamkubali, ndege angani wanamkubali,hata wanyama polini tembo faru watakuwa salama ndani ya uongozi wake

Chama cha mapinduzi si chama cha wapumbafu kiasi ati wawachague sijui Membe, Sijui Sitta,Sijui Ngulu Nchemba, Sijui,Wassira ambao tayari wana wakundi wapeperushe bendera yake, Chama Cha mapinduzikimefanya busara zake zote kumshauri mgombea mtarajiwa achukue form . MueleweCCM mgombea wake huyo ameombwa agombee, siyo amejipigia debe kama wengine.

Tusubiri tuone.
EE Mungu ibariki Tanzania, tuondokane na jinamizi hili.

team lowasa at work
 
tatizo watu bado hawajui tu ila ukweli ni kwamba rais ajae ni pinda najua watu watabisha sana ila ukweli ndio huo,pinda alikuwa hana mpango na urais ila marais wastaafu ni aliepo madarakani ndio walio mshawishi agombee ngoja muda ufike ndio mtakumbuka maneno yangu

huyu binti machozi urais atauwezea wapi?
 
Kiongozi anayejijua kashindwa kufanya haya ili hali ana nafasi - basi hatufai hata kidogo.
1 Mapigano ya wakulima na wafugaji
2. Mgawo usio wa haki hasa katika suala la ardhi kati ya wawekezaji vs wazawa hence kuleta migogoro kati yao.
3. Kushabikia u-chama na si utaifa - hence kuleta mgawanyiko kati ya watanzania walio wamoja tangu uhuru.
4. Vita madawa ya kulevya
5 Wizi wa mali za umma - Hasa suala la ESCROW

Kamuulize ole sendeka na wabunge juu ya namna Pinda alivoshughulikia Migogoro ya wakuli na wafugaji. Hata mauaji ya Kiteto ile juzi,hayakutokea mahala ambapo huwa yanatokea. Pinda alikwenda ku' level.


Madawa yakulevya ni janga la Dunia. Pinda hana maadili machafu yakushindwa kukabiliana na issue hiyo. Yes! kuna setbacks nyingi sana ktk jambo hili. Lakini nijambo lakushukuru kuwa,Pinda hawezi akawa miongoni mwa dealers au watu wowote wanaoweza kurudisha nyuma Vita hii.

Pinda hawezi na hajikushabikia Uchama na kuleta migogoro kisiasa. Ushahidi ni Record yake ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Hana MAKUNDI.

WIZI WA MALI YA UMMA; Naamini uko shahidi wa kwamba,Pinda si MWIZI/FISADI.

Jambo kubwa hapa ni namna anavyoweza kutoa mchango ktk kupambana na vitendo hivi. Yuko mstari wa mbele ktk jambo hilo. Unaweza ukarejea issue ya JAIRO. Hata hili la Escrow, amejitahidi mno (pamoja na kudanganywa mara kadhaa na washauri / wataalam wake.

Mkuu; kuna mambo mengi yakumsafisha Pinda. Tusubiri wakati ukiiva. Tutayaweka kwa maslah mapana ya Taifa (in case akipewa nafasi na Chama)
 
Kweli mfa maji haishiwi mnayemtegemea Jik;vim;stilwire vimeshindwa unakuja na sabuni ya kipande unategemea atang'aaa rais atatoka ukawa
and that is the story amini usiamini
 
kwa sifa ulizotaja hakuna rais kutoka misisiemu
 
Back
Top Bottom