Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abuu Jumaa amesema, mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni Rais aliyeletwa na Mwenyezi Mungu akieleza kuwa hilo linathibitishwa na namna alivyofanya mambo mengi makubwa ya kimaendelea katika kipindi cha muda mfupi aliokuwa madarakani
Abuu Jumaa amezungumza hayo akiwa kwenye jimbo la Mkuranga, mkoani Pwani aliposhiriki kwenye kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM Abdalah Ulega
"CCM itashinda, na itashinda kwa sababu tunaye Rais mzalendo, tunaye Rais jasiri, tunaye Rais mwenye kuthubutu, tunaye Rais mwenye huruma, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana nchi hii, kila mahali ukienda huwezi kukuta kijiji au kitongoji kuna kitu kimefanyika" -Abuu Jumaa
Amesema sambamba na kuanzisha miradi mingi mipya ya maendeleo katika kipindi cha muda mfupi aliokuwa madarakani, lakini pia Dkt. Samia Suluhu Hassan haikutelekeza miradi yote aliyoachiwa na mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, miradi ambayo kwa uhalisia imegharimu fedha nyingi lakini ameitekeleza kwa kasi.