GE2025 Mgombea ubunge CUF Siha auawa kinyama katika ugomvi

GE2025 Mgombea ubunge CUF Siha auawa kinyama katika ugomvi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema linafanya uchunguzi tukio la kuuawa kwa Daud Mtuyehabi, aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Siha.

Tukio la kujichukulia sheria mkononi limetokea Oktoba 7, 2025 majira ya saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Kilingi, baada ya Mtuyehabi kudaiwa kumchoma kisu tumboni Abdul Mohamed, mkazi wa Kilingi, Kata ya Sanya Juu wakati akiamulia ugomvi uliozuka kati ya Mtuyehabi na Hamad Mohamed wakati wakinywa pombe, kutokana na kudaiana fedha.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia Daudi Mtuyehabi hadi kusababisha kifo," imesema taarifa.

IMG_20251008_090736_472.jpg
IMG_20251008_090736_488.jpg

 
Ugomvi kinyama ndiyo ugomvi gani huo, nimeuliza swali kutokana na heading bado sijasoma details.
 
Aisee

Sasa hv kumwagana damu ni jambo simpo sana, hapo unaweza kukuta walikuwa wanadaiana elfu 20.
 
SiHasa.... mgombea wa mbogamboga siha awe wa kwanza kuhojiwa.....
Ww huna akili na ipo siku utashindwa kubeba mimba ya mumeo na kuanza kuilaumu ccm.

Umeshaambiwa ni ugomvi wa watu wawili walikuwa wanadaiana pesa, aliyekuwa anagombea ubunge akamchoma mwenzie kisu na kumtoa utumbo nje, naye pia akauawa.

Sasa hapo huyo mgombea wa ccm anaingia vp?
 
Mbaga Jr ......

Usiwe mpumbavu wa akili....mambo huwa yanatengenezwa ! naongea hivi hicho kisa nakifahamu vyema, na sio kwa kukisoma hapa ! Niishie hapa ! Acha shobo kama mwanamke aliyeibiwa mume !
 
Mbaga Jr ......

Usiwe mpumbavu wa akili....mambo huwa yanatengenezwa ! naongea hivi hicho kisa nakifahamu vyema, na sio kwa kukisoma hapa ! Niishie hapa ! Acha shobo kama mwanamke aliyeibiwa mume !
Kwa hiyo CCM walimtuma mgombea huyo wa CUF amchome mtu kisu na kusababisha utumbo utoke nje?Ili baadaye watu wachukue sheria mkononi na kumuua huyo mgombea?Kuna siku jua litapatwa mtaisingizia CCM kwamba ndio iliyosababisha jua kupatwa.
 
Back
Top Bottom