October 28 CCM hawachomoiMgombea Ubunge wa Chadema Jimbo la Bukene Lumola Stephen Kahumbi amepokea taarifa za vitisho vya kutekwa na kunyang'anywa Fomu za Uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Katika taarifa yake kwa Umma Lumola amesema tayari ameshawasilisha taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.
Lumola ameonya kwamba atatumia njia yoyote kujilinda ili fomu zake zisiporwe na akasema Yuko tayari kufa kuliko wampore fomu hizo.
WITO
Kutokana na Mara kadhaa wagombea wa Upinzani kufanyiwa hujuma za kutekwa na kuporwa fomu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Kanda zake zote 10 wanapaswa kuandaa taratibu za kuwalinda wagombea wao wote wa Ubunge na Udiwani Kati ya leo mpaka siku ya Jumanne siku ya kurejesha fomu.