DICTATOR
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 391
- 3
na Ali Lityawi, Kahama
Source: Tanzania Daima
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Igunda, Wilaya ya Kahama kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Malecha Kasonha (43), amefariki dunia jana majira ya saa 10:30 alfajiri katika hospitali ya serikali wilayani hapa.
Kasonha alifikwa na mauti baada ya kusumbuliwa na maradhi ya tumbo na kulazwa kwa muda wa siku tatu.
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kahama, Juma Ntahimpera, alisema mgombea huyo aliyekuwa akiwania kata hiyo mpya iliyogawanywa kutoka Kata ya Nyandekwa, alifikwa na mauti hayo alfajiri ya Ntahimpera alisema marehemu Kasonha aliugua tumbo ghafla mara baada ya uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa chama hicho, Jimbo la Kahama.
Baada ya uzinduzi huo, marehemu alijisikia tumbo kumsokota, alitutaarifu tukampeleka hospitali alilazwa hadi alipofikwa na mauti, alisema Ntahimpera.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA wa Wilaya alisema marehemu huyo aliyeacha mjane mmoja na watoto sita atazikwa kesho saa nne asubuhi katika kijiji alichozaliwa cha Bunasani, Kata ya Igunda. Katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya udiwani kwenye kata hiyo, marehemu alikuwa akichuana vikali na wagombea wawili wa vyama vya CUF na CCM.
Swali langu: Vipi wadau hapo sheria inasemaje kuhusu kuweka mgombea mbadala au utaratibu ni upi hapo? Nawaombeni ufafanuzi hapo.