Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Gazeti la kila siku la Mwananchi limeripoti leo ya kuwa mgombea wa ubunge wa CCM wa Maswa ambaye dereva wake aliuawa na wananchi wenye hasira na kusababisha mgombea ubunge wa Chadema Shibuda kuswekwa lupango sasa na yeye amemfuata ingawaje kwa sababu nyingine.
Kulingana na Mwananchi ya leo, mgombea huyo amejikuta lupango kwa tuhuma za kumpiga OCD. Hili ni shitaka dogo ukililinganisha na lile linalomkabili Mheshimiwa Shibuda la mauaji na hivyo huyu wa CCM anaweza kupewa mdhamana lakini Shibuda ni vigumu kuupata msamaha kutokana na mashitaka yanayomkabili.
Hii inawezekana kabisa ni janja ya nyani- kwa maoni yangu- kwa sababu kama polisi wetu wangekuwa si mashabiki wa CCM mgombea huyu wa CCM ndiye alipaswa kuwa mshitakiwa wa kwanza kwa kumtuma dereva wake kwenda kuchochea vurugu dhidi ya wapenzi wa Chadema. Kwa mapolisi kutomshtaki huyu mgombea wa CCM kwa tuhuma za mauaji wa dereva hata kama siyo ya kukusudia yaani - manslaughter- yaashiria Mheshimiwa Shibuda hawezi kutendewa ubinadamu na ingefaa aachiliwe huru mara moja kwa matatizo ya kiufundi yaitwayo "misjoinder of the accused."
Hata hivyo , tunaelewa ni kwa nini Mheshimiwa Shibuda yupo lupango ni kwa sababu za kisiasa tu na baada ya uchaguzi tusishangae kesi hiyo ya mauaji ikapoteza mwelekeo....:Lengo la JK na CCM yake ni kumzuia Mheshimiwa Shibuda kuendelea na kujiimarisha na kampeni zake kwa kumshikilia kwa tuhuma ambazo wahusika wote polisi inawajua lakini haitaki kuwashughulikia kwa minajili ya kupoteza lengo.
Swali la kuwauliza polisi na hususani IGP na DPP hivi inakuwaje mmliki wa gari lililokwenda kuanzisha vurugu asikamatwe kwa tuhuma za kumtuma dereva wake na gari yake kwenda kuleta vurugu kwenye shughuli za watu wengine? Hivi polisi watueleze wanaubia gani na serikali ya JK na CCM yake pale wanapoacha kushughulika na watuhumiwa halisi na kumkamata Mheshimiwa Shibuda ambaye hata hivyo hata hakuwepo kwenye eneo la tukio?