Mgombea CCM aliyempiga OCD naye akamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea CCM aliyempiga OCD naye akamatwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 25, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Gazeti la kila siku la Mwananchi limeripoti leo ya kuwa mgombea wa ubunge wa CCM wa Maswa ambaye dereva wake aliuawa na wananchi wenye hasira na kusababisha mgombea ubunge wa Chadema Shibuda kuswekwa lupango sasa na yeye amemfuata ingawaje kwa sababu nyingine.

  Kulingana na Mwananchi ya leo, mgombea huyo amejikuta lupango kwa tuhuma za kumpiga OCD. Hili ni shitaka dogo ukililinganisha na lile linalomkabili Mheshimiwa Shibuda la mauaji na hivyo huyu wa CCM anaweza kupewa mdhamana lakini Shibuda ni vigumu kuupata msamaha kutokana na mashitaka yanayomkabili.

  Hii inawezekana kabisa ni janja ya nyani- kwa maoni yangu- kwa sababu kama polisi wetu wangekuwa si mashabiki wa CCM mgombea huyu wa CCM ndiye alipaswa kuwa mshitakiwa wa kwanza kwa kumtuma dereva wake kwenda kuchochea vurugu dhidi ya wapenzi wa Chadema. Kwa mapolisi kutomshtaki huyu mgombea wa CCM kwa tuhuma za mauaji wa dereva hata kama siyo ya kukusudia yaani - manslaughter- yaashiria Mheshimiwa Shibuda hawezi kutendewa ubinadamu na ingefaa aachiliwe huru mara moja kwa matatizo ya kiufundi yaitwayo "misjoinder of the accused."

  Hata hivyo , tunaelewa ni kwa nini Mheshimiwa Shibuda yupo lupango ni kwa sababu za kisiasa tu na baada ya uchaguzi tusishangae kesi hiyo ya mauaji ikapoteza mwelekeo....:Lengo la JK na CCM yake ni kumzuia Mheshimiwa Shibuda kuendelea na kujiimarisha na kampeni zake kwa kumshikilia kwa tuhuma ambazo wahusika wote polisi inawajua lakini haitaki kuwashughulikia kwa minajili ya kupoteza lengo.

  Swali la kuwauliza polisi na hususani IGP na DPP hivi inakuwaje mmliki wa gari lililokwenda kuanzisha vurugu asikamatwe kwa tuhuma za kumtuma dereva wake na gari yake kwenda kuleta vurugu kwenye shughuli za watu wengine? Hivi polisi watueleze wanaubia gani na serikali ya JK na CCM yake pale wanapoacha kushughulika na watuhumiwa halisi na kumkamata Mheshimiwa Shibuda ambaye hata hivyo hata hakuwepo kwenye eneo la tukio?
   
 2. j

  janusqm1 Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inakuaje kisheria, is that mean shibuda will not be in a campaign rally until the ellection day? If it happens he win the ellection, will his candidacy be elligible? Wadau nisaidieni.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kwa nini Shibuda anaendelea kushikiliwa wakati inafahamika kuwa hakuwepo kwenye eneo la tukio? Kwa nini afikishwi mahakamani? Hii si njama ya kumpotezea muda wa kufanya kampeni katika saa hizi za lala salama?
   
 4. T

  Tata JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Hizo ndio mbinu za ziada za chama dola - CCM kinapoona kuwa hali yake siyo nzuri.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mgombea CCM aliyempiga OCD akamatwa


  na Stella Ibengwe, Maswa


  JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mgombea ubunge katika Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Simon Kisena, kwa kosa la kumpiga ngwala Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru.

  Habari zinasema Kisena alimpiga ngwala ODC Nduguru baada ya kushindwa kuelewana katika mahojiano baada ya mgombea huyo kupata taarifa za dereva wake kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, alisema Kisena alifanya kitendo hicho Oktoba 21, mwaka huu kufuatia vurugu zilizowahusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Steven Kwirasa (26).

  Alisema Kisena alikamatwa jana mchana na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa moja kwa moja mahabusu.

  Kukamatwa kwa mgombea huyo kunaongeza idadi ya watu wanaoshikiliwa kufikia 14, akiwamo mgombea ubunge wa CHADEMA, John Shibuda na wengine 12 kwa kile kilichodaiwa kuhusika kwenye tukio hilo.

  Inadaiwa wakati Shibuda akiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kizungu, gari lake liliondoka kwa ajili ya kuelekea kijiji kingine kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mkutano mwingine.

  Alisema katika tukio hilo, dereva wa mgombea ubunge wa CCM, Steven Kwilasa (26) aliyekuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 917 BBH alishambuliwa kwa mawe na kipigo hadi kifo.

  Alisema kutokana na hali hiyo, wafuasi wanne wa CCM walijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, ambapo mgombea wa CCM hakuwa eneo la tukio hilo.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alisema jeshi hilo limeunda tume ya maofisa wanne kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha vurugu hizo.

  Alisema mara baada ya uchunguzi huo, uamuzi wa kumpa dhamana Shibuda ndipo utatolewa, lakini kwa sasa hana namna zaidi ya kuendelea kushikiliwa.

  “Ni kweli niko Maswa kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi wa tukio hili… tumeunda tume ya maofisa wanne kwa ajili ya kuchunguza suala hili, tutatoa majibu pindi kazi hii ikikamilika,” alisema DCI Manumba.


  Chanzo: T Daima
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nauliza: Hivi kosa la kumpiga polisi adhabu yake ni nini mtu akipatikana na hatia chini ya Kanani ya Adhabu? Sina hakika mimi, lakini nadhani ni kifungo tu bila ya faini. Kama ni hivyo, unless kina Makamba/Manumba/ridhwani watamuokoa, huyo mgombea wa CCM sasa ni finished politically.

  Labda compromise moja tu inaweza kumuokoa huyu, kwamba wote wawili -- yeye na Shibuda waachiliwe mara moja. In fact kosa la Shibuda silioni, hakuwepo eneo la tukio, labda wa-prove kwamba aliwatuma wafuasi wake wakamwuue huyo dereva.
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Habari nilizozipata ni kuwa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Maswa Magharibi bwana Robert Kisena ameachiwa huru kwa dhamana (Mwananchi, 25 Octoba 2010,u.k 1 & 4).
  Kinachoniumiza kichwa hapa ni suala la Shibuda,kwa nini mbaka leo wanaendelea kumshikilia,anakosa gani?.Taarifa tulizozipata ni kumba wakati tukio la mauaji,lilipotokea yeye alikuwa anaendelea na mkutano wa kampeni,hivyo hakuwepo eneo la tukio,kwa lugha raisi hakutekeleza mauaji,sasa kwa nini wanaendelea kumshikilia?huu ni uonezi na anashikiliwa ili kumzoofisha kisiasa!!!!!!!!!!!!!
   
 8. o

  omuhabhe Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila mpenda amani na muumini wa sheria za nchi yetu ataungana nami kulaani kitendo hicho kilichofanywa na mgombea ubunge huko Maswa na kutolewa majibu kuwa jambo hilo ni la binafsi zaidi kati ya mgombea na OCD.

  Je nini fundisho kwa wengine wakati huu wa kuelekea uchaguzi na kupata matokeo yake kwa wapiga
  kura, kama kila mtu atakuwa na wazo la kushambulia vyombo vya dola na kupata baraka za majibu kama ya Maswa itakuwaje?

  Bw Membe unalisemeaje hilo maake kwa Bw Shimbo ulizungumza saaana, tunasubiri busara zako.
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi si mwanasheria, lakini nasikia ni kosa kubwa kumdhuru polisi akiwa amevaa sare zile, vijana wa zamani tunasema 'unadharau crown'.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tume ya nini tena ! Kosa kumshambulia askari akiwa kazini (OCD).
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mie nauliza kosa la Shibuda ni nini hadi awekwe ndani bila dhamana??
   
 12. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kuwa mfuasi wa chama cha upinzania CHADEMA
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pongezi kwa jeshi la polisi kusimamia haki..... Pia nivyema wakakomesha hizi dharau kwani kumpiga polisi ni kuahatarisha usalama wa raia. Polisi anapoonekana ameshindwa na raia inaleta picha mbaya kwa raia wakawaida kwani wengi wetu tunategemea polisi kama watetezi wetu na wasimamizi wa mambo ya usalama wa raia kwa ujumla. Viongozi wetu wa siasa kuweni na subira...... Tusiwadharau walinzi wetu ni mbayaaaaa!
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huoni kama kuna murder kesi hapa?
   
 15. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huoni kama kuna murder kesi hapo?
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  ccm watatafuta watu wao ndio watoe ushahidi dhidi ya Shibuda
   
 17. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,074
  Likes Received: 15,729
  Trophy Points: 280
  JAMANI MIE WAGOMBEA WOTE SIJAOANA ANAYENIFAA ZAIDI YA MGOMBEA URAIS BWANA KUGA MZIRAY MAANA YEYE KAMPENI ZAKE HAZINA VURUGU WALA HAHITAJI KUJITANGAZA, NIMESHANGAA HATA HAPA JAMII FORUMS KWA WALE WANAOPIGIWA KURA HAYUPO. JAMANI NAOMBA ATAMBULIWE NA YEYE. NA KWA MTIZAMO WANGU HUU NDIE RAIS ANAYETOSHA:smile-big:
   
 18. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ipi hiyo ya kubambikiwa kama walivyotaka kumfanyia mtoto wa Mengi akawashtukia. Shibuda hakuwepo katika eneo la vurugu hizo wala hakujua kutokea kwa tukio hilo ila kachomekewa.
   
 19. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kosa ni kosa,Kisena kafanya kosa la kufanya fujo kituo cha polisi chini ya kifungu cha 89(a) (2) cha kanuni ya adhabu,pia katenda kosa la shambulio la kawaida kwa huyo OCD- common assault. Hivo hana sababu ya kutoshitakiwa hata kama ni mgombea wa CCM. Alotenda kosa ni mtu! kwa upande wa RPC alikosea sana kusema ni masuala binafsi ya ocd na kisena,kauli yake ni hatari sana kwa mstakabari wa usalama wa raia! Hili kosa lilitendeka ndani ya kituo cha polisi ambapo askari walikuwepo na ndipo silaha zinapotunzwa,fikiria askari mmoja angeamua kuchukia baada ya mkuu wake kudhalilishwa mbele yake na kuamua kuchukua silaha na kumuelekezea kisena kingetokea nn!! Kisena si mstaarabu hata kidogo,Shibuda km alikamatwa na kuachiliwa ni haki yake kisheria - Kifungu cha 64 sura ya 20 yq sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kiko wazi! zilikuwa ni tuhuma tu na haijathibitika aliamuru au alikuwepo eneo la tukio! Unajua RPC huyo ni mzee sana kachoka kwa wale wasomfahamu alishastaafu ila kaongezewa miaka 2 ya mkataba,mkoa wa shy hauwezi hata askari wanalia sana kuhusu kushindwa uongozi wake,ambaye haamini aulizie km ana ndg yake huko! Hivi OCD asipomfungulia kesi kisena unafikiri hao askari walochini ya OCD wata muheshimu kweli! I dont think so!!!!!!!!!!!
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa ushahidi upi wakati yy shibuda alikuwa Juukwaaani? anahutubia nashindwa elewa maana hapakuwa na askari wakati Shibuda anatoa hotuba? na kama askari alikuwepo kwanini hakutoa taaarifa hizo mapema kwa askari wenzake ili kuwahi hiyo ghasia? na Huwa ni askari wangapi huwa wanakuwepo kwenye mkutano na unapo waweka hao maaskari unaangalia idadi ya watu wajao kwa mkutano au askari anapangiwa tu eneo hivyo hivyo litakavyo kuwa kama lina watu wengi au wachache

   
Loading...