droidwallmail
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 275
- 63
UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu kwa wapiga kura. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.
Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na Tume haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.
lakini kwanini vile kura zinahesabiwa mannualy na sio mashine tena kama zamani, na wao wanajua kuwa sio wapiga kura wote ni waelewa, kwanini wakati wanazihesabu wasiachane na hizo errors sababu wao ni binadamu na hakika wakati wa kuhesabu watajua huyu mpiga kura hapa kakosea kuweka alama lakini aliyemchagua ni fulani alafu ihesabike tu. maana mi sioni kama kuna ubaya wowote sababu anayezihesabu ni mwanadamu, sio mashine. au mnaonaje wadau?