Mgombea CCM aanguka jukwaani akiruka kichurachura!

Mgombea CCM aanguka jukwaani akiruka kichurachura!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,528
Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Tunduru Kaskazini, Injinia Ramo Makani, alianguka jukwaani wakati wa kampeni. Alikuwa anaruka kichurachura kuwathibitishia wapiga kura yuko fiti kiafya ndipo 'aibu' hiyo ilipomkuta.
View attachment 294680
Mgombea ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Tunduru Kaskazini,Mhandisi Ramo Makani alianguka jukwaani wakati akijaribu kuruka kichura chura.

Tukio hilo lilitokea katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za mgombea huyo, uliofanyika kwenye viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.

Inasadikiwa kuwa alikusudia kunogesha staili ya mgombea urais wa tiketi ya CCM,Dr. John Magufuli ya kupiga Push Up..
Ingawa tukio hilo lilionekana kumfedhehesha,mgombea huyo alijikakamua kuinuka huku akisaidiwa na walinzi wake na kuendelea kunadai sera zake.

Alisema kuwa katika kipindi kilichopita alitekeleza ilani ya chama chake kwa kusimamia ujuenzi wa barabara ya Namtumbo-Tunduru hadi wilayani Nanyumbu inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

Nitasimamia kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kuwa mradi wa kusambaza umeme vijijini unaanza'' alisema.

Chanzo:
Majira

My take: Acheni Mungu aitwe Mungu!

UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu kwa wapiga kura. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.

Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na Tume haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.
 
Wazee wa push ups wameacha Sera sasa wameshika ajenda ya afya zao na sio afya za watanzania wanaokosa Huduma kwenye vituo vyetu vya tiba
 
Eeeeeehh... safi sana Hizo ni sifa za kijinga
 
UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu kwa wapiga kura. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.

Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na Tume haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.

Kweli tupu mana wengi wanajua kuna chama kinaitwa ukawa
 
Siasa za Tanzania na maajabu yake!
""eti kugufurika""wapi imewahi tokea duniani?te te te!
 
UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu kwa wapiga kura. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.

Vinginevyo, kama wadau walivyosema, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na Tume haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.

mbona umetoka nje ya THREAD hii mkuu.

Anzisha yako na siyo kudandia gari moshi kwa mbele.
 
POLE KAMANDA; PUSH UP KAMA KAWAIDA
11.jpg
 
Push up tunapiga ila sijaona tukiahidi kuboresha michezo!

Ni vizuri tulitazame kundi la vijana wa michezo kwa kuwa tukipata mchezaji mmoja kama Diego Costa ataifanyia makuu nchi na jamii inayomzunguka
 
Heeh! Kumbe huu ulimbukeni umeenea mpaka huko majimboni.

MAGUFULIKA NDIO HABARI YA MJINI...sasa hivi hadi kwenye harusi....maharusi WANAMAGUFULIKA..... Kuanzia November 2015....sehemu za kazi kabla ya kuanza kazi ... KUMAGUFULIKA baada ya kabla kwenda Nyumbani watu watakuwa wanamagufulika tena!!
 
Hapo juu naona wanahamu ya kuchafua Boxer
 
Back
Top Bottom