Informer
Platinum Member
- Jul 29, 2006
- 1,611
- 6,717
MGOGORO mkubwa unakinyemelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuelezwa kuwa sekretarieti yake imekayakataa mapendekezo ya Tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo, ukiwamo wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu), ambayo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.
Mradi huo wa maji unaelezwa kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Karatu uliko mradi huo walihojiwa jana, lakini akasema hapakuwa na mpango wowote wa kufukuzana.
"Ninachoelewa ni kwamba waliitwa wakahojiwa na kitakachofuata ni kupewa maagizo ambayo lazima wayafuate na atakayekiuka ndiye atakayefukuzwa," alisema Mwigamba.
Baadhi ya viongozi wa Chadema Karatu waliotarajiwa kuhojiwa jana ili kupata suluhu ya mgogoro huo ni pamoja na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu, Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini, Jubiless Mnyenye.
Viongozi wakuu wa Chadema hawakupatikana jana kwa kuwa muda mwingi walikuwa katika kikao hicho ambacho kilimalizika jana, huku ikielezwa kuwa taarifa rasmi kuhusu yaliyojadiliwa itatolewa leo.
Alipoulizwa kuhusu mgogoro huo, Msemaji wa Chadema Tumaini Makene alisema agenda za kikao hicho zilikuwa wazi na ziliainishwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi.
"Hakuna zaidi ya hizo na leo (jana), ni masuala ya Katiba Mpya. Kwenye yatonakayo, masuala mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya nchi yanajadiliwa nchi nzima kwa sababu yanatokana na vikao vilivyopita si Karatu pekee. Angalia usije ukalishwa matangopori," alisema.
Kumshinikiza Rais
Habari zaidi kutoka katika kikao hicho zinaeleza kuwa kamati hiyo imeazimia kuchukua hatua ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusimamia utekelezaji wa masuala ambayo yapo katika mamlaka yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wengine ambao kimesema kinataka wawajibishwe ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.
Kamati hiyo pia imeazimia kuanzia Januari kuwa na operesheni kubwa ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), nchi nzima kushinikiza utekelezaji hatua za kinidhamu kwa watendaji hao na watuhumiwa wa ufisadi wa Fedha za Madeni ya Nje (EPA).
CHANZO: Mwananchi | Disemba 17, 2012
***************************

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UFAFANUZI WA AWALI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, Desemba 15-16, 2012, katika Hotel ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, imemaliza kikao chake Desemba 16, usiku.
Pamoja na kwamba maazimio yote ya kikao hicho yatatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Desemba 18, 2012, huu ni ufafanuzi wa awali kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazowakanganya wanachama na Watanzania kwa ujumla, zilizoandikwa
tangu jana Jumapili na Jumatatu, katika baadhi ya vyombo vya habari.
Mbali ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea taarifa ya hatua kadhaa za utekelezaji wa maazimio yatokanayo na vikao viwili
vilivyotangulia, Kamati Kuu pia ilijadili hali ya siasa nchini, mchakato wa Katiba Mpya na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).
Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya mwenendo wa chama kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambapo ilijadili pia kasoro za utendaji wa viongozi wa chama katika Wilaya ya Karatu.
Kamati Kuu ilichukua uamuzi wa kusimamisha uongozi mzima wa Wilaya ya Karatu na kuweka shughuli za utendaji wa chama chini ya uangalizi wa Kamati Kuu mpaka hapo itakapotolewa maagizo mengine baadae.
Aidha, Kamati Kuu pia ilipokea na kujadili mwenendo wa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa taasisi za kiserikali wanaotokana na
CHADEMA, hasa katika masuala ya ardhi na maji Wilayani Karatu.
Kikao pia kilibaini kuwa taarifa zinazohusu masuala hayo ya maji na ardhi ni tofauti na namna zilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Aidha kutokana na mjadala, iliazimiwa hatua kadhaa zichukuliwe, ambazo umma utaarifiwa katika tamko la Kamati Kuu litakalotolewa
kupitia waandishi wa habari.
Imetolewa leo, Desemba 17, 2012,
Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari
CHADEMA