Bb YangeYange
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 337
- 184
Mwalimu Nyerere kabla hajaaga dunia alikuwa akihangaikia usuluhishi wa mgogoro Burundi. Warundi na jumuia ya kimataifa wanatambua juhudi kubwa za Mwalimu katika utatuzi wa mgogoro huo. Taasisi ya Mwalimu Nyerere ilianzishwa mahsusi kuendeleza yale aliyoyasimamia. Cha kusikitisha ni kwamba Taasisi inayobeba jina lake haisikiki ikiendeleza ama ikisimamia kwa dhati yale ya Mwalimu ikiwemo usuluhishi. Mara moja sana hujitokeza kwenye masuala ya kisiasa. Kulikoni? Taasisi ya Mwalimu inakufa?