Mgogoro wa Qatar vs Saudi Arabia

TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,369
Likes
5,151
Points
280
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,369 5,151 280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
JAMAL KHASHOGGI ATHIBITIKA KUUAWA NA SAUDI ARABIA

DANA DANA ZA UFALME WA SAUDIA NA KUJIUMA UMA KWA TRUMP

Taarifa iliyotolewa na Saudi Arabia imethibitisha kuuawa kwa Jamal ndani ya ubalozi wa Saudia

Ufalme umeunda timu ya uchunguzi ikiongozwa na crown prince MbS, waziri wa mambo ya ndani na mambo ya nje na kwamba itaanda taarifa ya nini kilitokea baada ya siku 30

Maafisa 18 wanashikiliwa na jenerali mmoja kiongozi wa intelejensia kuachiwa kazi.
Miongoni mwa maafisa hao, watano ni washirika wa MbS wa karibu sana

Hadi jana hakuna taarifa za kifo cha yoyote mingoni mwa hao wanaoshikiliwa

Haya yamejiri baada ya pressure kutoka jumuiya ya kimataifa ikifuatilia taarifa za Turkey

Turkey wamekuwa wazuri wakitoa taarifa kwa kudonoa donoa na uhakika hivyo kutompa nafasi Saudi Arabia kufanya michezo mingine, walimbana katika kona, hakutoka

Taarifa ya kuuawa Jamal imekuja kama mwiba kwa utawala wa Rais Trump.
Ni kiongozi wa taifa kubwa pekee aliyebaki akijiuma uma kana kwamba hajui afanye nini

Akiwa Intel community kali duniani, hili halikuwa tatizo la kusubiri

Alichitoka ni kununua muda ili suala lipite kimya kimya
Alifanya hivyo kwa masilahi binafsi ya biashara zake huku akisingizia biashara za nchi

Mabunge ya Marekani hayaridhishwi na hatua anazochukua Rais kinyume na thamani za taifa hilo 'values' ikizingatiwa mtafaruku wake na vyombo vya habari, huku suala zito kama hilo likifanyiwa kazi na France, Germany na UK kama viongozi wa dunia

Haijulikani Rais Trump atafanya nini baada ya Saudi Arabia kukiri kumuua Jamal ingawa mabunge ya US yanataka hatua kali

Kuna maswali yanajitokeza kuhusu tamko la Saudi Arabia......

Inaendelea
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MASWALI KWA SAUDI ARABIA

Sehemu ya II

Tulieleza huko nyuma mpango mzima ulipangwa hovyo.
Kauli ya kwanza ya afisa wa ubalozi kuwa Khashoggi alitoka ilikuwa dalili za awali za jambo baya

Swali la kwanza, alitokea wapi na saa ngapi baada ya nini na mlango gani?
Hakuna jibu baada ya kubaini uwepo wa mawasiliano kati ya Jamal na mkewe
Na kwamba, intelejensia ya Turkey ilifika uwanja wa ndege masaa machache kwa ukaguzi

Swali la pili, kwanini Saudi Arabia haikuwa na maelezo baada ya kutuhumiwa?
Jibu, walijua zipo habari zisizo na shaka juu ya walichofanya.
Ukaguzi wa ndege za Gulfstream ni ishara hamkani si shwari. Hawakuwa na majibu

Swali la tatu, kwanini walichukua muda kuongelea jambo hilo?
Walitegemea msaada wa Marekani kuyumbisha uchunguzi bila kujua taifa hilo lina rasilimali za weledi ' intellect' na si rahisi kutunga hadithi ikaeleweka
Walitumai Rais Trump angeokoa jahazi kwa mahusiano yao akiwemo Jared Kushner

Swali la nne, kwanini wametoa taarifa ya kukiri?
Hii inafuatia ziara ya SoS Pompeo aliyewaeleza lazima wachukue dhima ya tatizo akijua suala hilo ni mwiba kwa Rais Trump na litazidi kuchagiza udadisi wa masilahi yake kwa undani

Swali la tano, kwanini wameunda kamati kuchunguza tukio walilofanya wenyewe?
Ni katika kununua muda tukio lisahaulike katika siku 30, US itakuwa na mijadala ya midterm elections na matokeo yake. Hivyo, litapunguza pressure kwao na Rais Trump

Swali la sita, kwanini wamechukua hatua dhidi ya maafisa wao
Ni kutokana na jumuiya ya kimataifa kutaka iundwe tume kuchunguza.

Hilo lingewahusisha viongozi waliohusika na wangetoa siri za nani kawatuma na lini
MBS asingekuwa salama, kingdom ingelazimika kutafuta njia za kujisafisha

Njia nyepesi ni kuwaweka kizuizini wasihojiwe na mamlaka nyingine kwa hoja ya uchunguzi unaendelea. Kwa mantiki hiyo waliohusika watakuwa wamefungwa mikono na midomo

Na ili kuweza kudhibiti suala zima, MBS anayetuhumiwa kuongoza mauaji ni mkuu wa kamati

Maana yake ni kumuondoa katika watuhumiwa, kumwezesha kudhibiti habari za kichunguzi kama zitakuwepo au kumpa nafasi ya kutunga hadithi wakati muda umesonga mbele

Haiwezekani Saudi Arabia inayotuhumiwa ikajichunguza tena uchunguzi ukisimamiwa na mtuhumiwa nambari moja, crown prince MBS.

Jambo limezua maswali, siku 30 za nini ikiwa wanajua nini kimefanyika na maiti ipo wapi

Kwa fyongo inayochezwa pengine kwa ushauri wa Trump hakuna namna Saudi Arabia itakwepa kuwajibika kwa jumuiya ya kimataifa.

Ikiwa mzalishaji mkubwa wa mafuta, Saudi Arabia itasaidia sana Iran kulegezewa vikwazo na EU kurahisha upatikanaji wa mafuta na hilo litakuwa pigo kwa Rais Trump na BB Nyahu dhid ya Iran

Mwelekeo mzima wa siasa za middle east utachukua sura mpya
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
SAKATA LA KHASHOGGI NA SINTOFAHAMU US NA SAUDIA

Bandiko#23 tuliuliza Saudia ilihataji siku 30 za kuchunguza nini ikiwa ndiyo mshiriki wa tukio
Ilikuwa ni mbinu kutoka WH na Rais Trump ili kupoteza muda na suala kuisha kimya kimya

Saudia walianza kukubali wamefanya tukio hilo na kwamba Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi

Wakasema yalikuwepo ''mapigano' kati yake na watumishi wa ubalozi yaliyopelekea mauti yake
Baada ya ushahidi kutolewa, ilikuwa wazi Khashoggi asingeweza kupigana na watu 15

Saudia wakaunda timu ya uchunguzi ikiongozwa na mtuhumiwa wa kwanza MBS
Walikusudia kuwatuhumu baadhi ya watu ili kumuondoa MBS katika watuhumiwa

Saudi wakasema mauaji yalikuwa ya kukusudia 'pre mediated', watuhumiwa wanashikiliwa.
Hili lililenga kuwatuhumu wauaji na kumuondoa MBS ili mbele ya safari mambo yasawazishwe

Majuzi wakatangaza watu 5 wanaokabiliwa na tuhuma, serikali imeomba wahukumiwe kifo
Mpango ulilenga kupumbaza Dunia kuwa hatua zitachukuliwa na serikali ya MBS 'mtuhumiwa''

Yote yalifanyika kuficha ukweli unaomhusu MBS, wahusika wangeachiwa dunia ikipumbazika

Yalifanyika kwa msaada wa WH ambao MBS ni mtu muhimu,na mshirika wao kukabiliana na Iran

Kwa bahati mbaya mpango wa Saudia Arabia ulikuwa na 'wachezaji wengi' Turkey akiongoza

Turkey wana matatizo na Saudia kupitia mzozo wa Qatar kama ilivyo mwanzo wa uzi
Mauaji yamewapa 'silaha' ya kumbana Saudia kama''msaliti' wa mashariki ya kati kupitia US

Turkey wametoa msaada wa kimataifa kuhakikisha sakata halifutiki bila kibano kwa Saudia

CIA wamekusanya taarifa za uhakika wakisema Khashoggi aliuawa kwa maelekezo ya MBS

Habari hiyo si njema kwa Rais Trump anayetaka sakata la Khashoggi lijiishie kimya kimya
Rais Trump ana mawaili, akubaliane na 'tamthilia' ya Saudi Arabia au ukweli wa CIA

Huko katika Congress hali si shwari, Dems na GOP wanaungana ili Saudia iadhibiwe hasa MBS

Kwa ilipofikia mfalme wa Saudi Arabia atakuwa na kibarua cha kumwengua MBS , au Trump atakuwa na kibarua cha kushawishi serikali yake na jumuiya ya kimataifa kuhusu MBS

Tusemezane
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
542
Likes
279
Points
80
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
542 279 80
SAKATA LA KHASHOGGI NA SINTOFAHAMU US NA ...

Tusemezane
Moja ya ahadi za kampeni za Trump ilikuwa ni kupunguza / kuachana na biashara ya kujihangaisha na masuala ya mataifa mengine ("America First"). Verdict: Hakuwezi kuwa na boots on ground Saudia kutoka Marekani kutokana na suala hili tu, kama Trump atataka kuwapendeza wapiga kura wake.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Moja ya ahadi za kampeni za Trump ilikuwa ni kupunguza / kuachana na biashara ya kujihangaisha na masuala ya mataifa mengine ("America First"). Verdict: Hakuwezi kuwa na boots on ground Saudia kutoka Marekani kutokana na suala hili tu, kama Trump atataka kuwapendeza wapiga kura wake.
Mkuu Mlenge , sera ya America first ni Rais Trump kuwa 'ill informed' kwa mambo ya dunia na hata ya nyumbani

America first haiwezi kuzidi masilahi mapana ya nchi hiyo ambayo ni kutawala Dunia

Trump alipouza sera ya America First, ilipokewa na wanaoamini kuwa bila kujiingiza katika masuala ya kimataifa , Wamarekani watakuwa na maisha mazuri.

Kwa mfano, Trump alisema US inatoa misaada inayoweza kutumika kuimarisha maisha ya watu.
Takwimu zinaooonyesha misaada ni chini ya a(2%?) tena ikiwa na return katika security ya US

Majeshi ya US kule Ujerumani si kuilinda nchi hiyo, ile ni ''strategic point'' ya usalama wa US.

Majeshi ya US Korea Kusini si kuilinda Korea, ni kwa US kwa kuangalia China na North Korea. South Korea ina askari 30,000. Trump hawezi kuyaondoa , aliposema hakujua 'ill informed'

Majeshi ya US kule Japan ni kwa ajili ya US. Mgogoro wa kisiwa cha South China na kujitanua kwa China kunalazimu US wawe karibu. Trump hakujua kwa ''ignorance''

Hadi sasa, kuna majeshi ya US kule Saudi Arabia kwa masilahi yake.
US wanasaidia Saudia vita ya Yemeni na Syria katika logistic zote.Kuna boot tayari Saudia

Saudia ikiwa na holy sites, US haiwezi kuingilia kama inavyofanya kwa vinchi vingine. Huwezi kuona boot hadharani, boot zinakuwepo kwa strategy

Kutibuana na Saudia ni kuzua mtafaruku na Islam world, na hilo litawaunganisha Sunni, Shia, Ismailia. Mkakati wa divide and rule utakwama, masilahi ya US yatakuwa hatarini ikiwemo Israel

Suala la Khashoggi US inatafuta njia muafaka kukabiliana nalo, Trump ana hangaika. Vinginevyo, hilo kama halimhusu kwa America first, mbona linamsumbua sana!

Mkuu America first inaeleweka kwa wapiga kura wake wanaoamini kuzuia immigrants kutawapa kazi na si kwenda shule.

Kuna kazi milioni 7 hazina watu, bado watu wake wanaamini mtu anayeokota machungwa ni tatizo kwa US. Midterms imeonyesha jinsi wasomi na independents wanavyomkimbia Trump

Mwaka 2017 America first haikujali APEC, wanaona China inavyojitanua wanarudi kwa kasi.

America first iimefanya nchi hiyo kuanza kutengwa na kupoteza Influence katika world stage.

Kilichotokea Paris wakati wa Armistice kinaeleza kitu

CIA wanapotoa taarifa ''leak' kuhusu MBS na mauaji wanafanya makusudia ili Trump asiweze kulifukia.Wamebaini anataka kufanya hivyo kwa masilahi yake na familia na si America

Suala sasa lipo Congress. Intel community zinajua jamaa ni ignorant na ill informed, haziwezi kuwa katika kundi la Trump. Zinajua America first kwa maana halisi si maana ya Trump
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
RAIS TRUMP NA TAARIFA YA CIA KUHUSU SAUDIA

Rais Trump ameendelea kusisitiza US ''haitaiadhibu'' Saudi Arabia kutokan na mauji ya Khashoggi
Habari zilizovujishwa kutoka CIA zinasema, mamlaka hiyo 'ina confidence' kuhusu ushiriki wa MBS

Rais Trump anasema, inawezekana au haiwezekani kuwa alishiriki kwa vile taarifa haina hitimisho

Ni utaratibu wa CIA kutumia maneno 'confidence' kuliko 'conclusion' kwasababu uchunguzi unaweza kubadilika taarifa, hata hivyo, CIA inaposema ina confidence, kwa maneno mengine ina ushahidi

Rais Trump anasisitiza uhusiano na Saudia ni muhimu kibiashara hasa ya silaha, mafuta na usalama
Katika kupoteza mada, TV ya Fox wanasema Khashoggi ni mwanachama wa muslim brother hood

Kumekuwa na reactions kutoka kwa watu wa mrengowa kulia na kushoto.
Hoja yao ni kuwa haki za binadamu ni thamani ya US na haibadilishwa kwa biashara za mafuta au silaha

Kauli za Trump zinamweka mahali tata. Kwanza, wapo wanaohoji kuhusu mashambulizi yake dhidi ya vyombo vya habari anavyoita 'enemy of the people' na kwamba, Khashoggi ni mhanga wa hali hiyo

Pili, wapo wanaochunguza ikiwa Saudia ina mahusiano binafsi na Trump.
Inaeelezwa, wa Saudia wamenunua nyumba Trump Tower, na wanapofika DC hufikia hotel ya Trump

Jambo hili linawafanya watu wahisi suala zima si kwa masilahi ya US bali masilahi binafsi yaTrump

Tatizo linalojitokeza si kuhusu hatua atakazochukua au asizochukua.

Ni kutokana na Maseneta wa Republicans kufadhaishwa na hali ilivyo ambapo mmoja wao Bob Corker ameandika 'hakutarajia kuona Marekani ikiwa kitengo cha mahusiano cha prince crown MBS''

Akiwa na mazonge zonge ya Mueller, bintiye Ivanka na emails, Act AG Whitaker n.k. suala la Saudia linaweza kuanza kuwatenga maseneta wa GOP na Rais Trump huku tayari akiwa amepoteza House

Tusemezane
 
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
13,129
Likes
17,500
Points
280
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
13,129 17,500 280

Naona Suala la Khashog limekufa kimya kimya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Naona Suala la Khashog limekufa kimya kimya!
Mkuu hili jambo halijafa kama inavyoonekana. Kinachoendelea ni kufuatilia sanaa ya watu walioshtakiwa na MBS sita kati yao wakikabiliwa na hukumu ya kifo
MBS anacheza karata zake kujinasua, ukweli unabaki pale pale kwamba Khashoggi aliuawa kwa maagizo yake

Vyombo vya nchi za Ulaya vinafuatilia kwa umakini ingawa vya Marekani vinaonekana kukaa kimya
Hata hivyo, ukimya wa vyombo vya Marekani si ule wa 'ukimya' watu wapo kazini wakitafuta data za kutosha

Siyo suala la Khashoggi tu kama mtu, hili ni pana likimuhusisha Trump na Familia yake ya akina Kushner
Kuna link inatafutwa na ipo siku utaliona suala hili 'likiwa bichi' na linavuja damu

Uhusiano wa MBS, Kushner, Trump na biashara zao hauwezi kutoa nafasi ya suala hili kufa

Unaweza kushangaa siku litakapoibuka linaweza kuwa sehemu ya uchaguzi likuhisisha mambo muhimu

Ni suala la muda tu
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
22,607
Likes
29,437
Points
280
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
22,607 29,437 280
Mkuu hili jambo halijafa kama inavyoonekana. Kinachoendelea ni kufuatilia sanaa ya watu walioshtakiwa na MBS sita kati yao wakikabiliwa na hukumu ya kifo
MBS anacheza karata zake kujinasua, ukweli unabaki pale pale kwamba Khashoggi aliuawa kwa maagizo yake

Vyombo vya nchi za Ulaya vinafuatilia kwa umakini ingawa vya Marekani vinaonekana kukaa kimya
Hata hivyo, ukimya wa vyombo vya Marekani si ule wa 'ukimya' watu wapo kazini wakitafuta data za kutosha

Siyo suala la Khashoggi tu kama mtu, hili ni pana likimuhusisha Trump na Familia yake ya akina Kushner
Kuna link inatafutwa na ipo siku utaliona suala hili 'likiwa bichi' na linavuja damu

Uhusiano wa MBS, Kushner, Trump na biashara zao hauwezi kutoa nafasi ya suala hili kufa

Unaweza kushangaa siku litakapoibuka linaweza kuwa sehemu ya uchaguzi likuhisisha mambo muhimu

Ni suala la muda tu
Nasubiri huo wakati ufike namimi nipate kuwa shuhuda wa hilo saga litakapo kuwa limeotesha mizizi upya ", naomba wakati uniweke mpaka hapo itakapo timu ... binafsi ni miongoni mwa watu wanao uchukue ule utawala wa kiimla unaoendelea pale saudia ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,250,884
Members 481,523
Posts 29,749,538