Mgogoro wa Madaktari unahitaji msuluhishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa Madaktari unahitaji msuluhishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by robert_m, Feb 2, 2012.

 1. r

  robert_m Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hali ya huduma za Afya kwa kweli inazidi kuwa mbaya wakati ambao watu toka kila upande wameweza kutoa maoni yao bila mafanikio. Kwa kuwa Serikali imeweka wazi uamuzi wake ambao haujaweza kubadili msimamo wa wataalamu hawa muhimu naona tumefikia mahali pa kushindana nguvu. Swali la msingi kujiuliza ni, Je hali hii itaendelea mpaka lini.

  Kwa mchango huu naona kwamba kwa kuwa makundi haya mawili yote yameshindwa kufikia mwafaka kinachohitajika ni kuwa na mpango wa usuluhishi. Kama watu waungwana, nafikiri tufike mahali tukubali ya kuwa maoni yetu yameshatolewa na tuanze kutafuta ufumbuzi wa kweli. Pendekezo la Muhimu ni kuwa tunahitaji neutral body itakayotafuta namna ya kusuluhisha makundi hayo mawili. Tunaomba taasisi au kundi litakalochukua mtizomo wa kati kuandaa mazingira yatakayowezesha pande hizi mbili kukutana ili kuweza kufikia mwafaka.

  Vyama vya kijamii, wateteaji wa haki, taasisi za usuluhisi nk. tunaomba mtafute njia ya busara na kuweza kuwakutanisha wahusika hawa wawili.

  Nawasilisha.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri aitwe waziri wa Afya Znz Mh Juma Duni Haji awe msuluhishi wa mgogoro huo. Vinginevyo kama Sio Kikwete mwenyewe kuingilia kati basi mtaumbuka.

  Huo ni ushauri wangu.
   
 3. cai

  cai JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 958
  Likes Received: 793
  Trophy Points: 180
  kuna siku tutakaa uwanja wa ndege kuwazuia hawa viongozi wanaoenda kutibiwa maralia huko india (huku sisi wakitusisitizia tutumie dawa za mseto kama zinatibu kwanini wao nao wasizitumie) wasiende kutibiwa huko nje nao watibiwe hapahapa tanzania kwenye hizi hospitali zetu za wilaya, mkoa na rufaa nao waone adha iliyopo labda wataona umuhimu wa kuboresha sekta ya afya tz. Hata pamba ya kusafishia kidonda nayo tunasubiri jk akaombe kwa obama.

 4. cai

  cai JF-Expert Member

  #4

 5. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ni ushauri sawa: lkn kumbuka kuwa hao wote hawana sifa na nguvu za kisheria kuwa wasuluhishi sanasana ni siasa tu ndizo zitakazo endelea: Tanzania tunao wataalamu waliosomea mambo ya Usuluhishi na Uamuzi watafutwe/wafuatwe ili waweze kutumika hapa ndo maala pake.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hakuhitajiki msuluhishi hii ni kushindwa kwa wateule wa mkulu. Huwezi suluhishwa na watu walioshindwa kazi na wasio na hekima!
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama ni serikali ya ccm siji kukubali kusikiliza msuluhishi kwa kuhonga na kuchakachua hoja ccm hawajmbo, hivyo sitaweza kaa meza moja na ccm labda waje kutoa taarifa kuwa wanakuja kuota taarifa kuwa madai yetu yote yamekubaliwa bila mabadiliko, hapo nitakaa. Kwa sasa Ccm hawana sura ya usuluhishi.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .
  Nafikiri hujui hata madaktari wanadai nini?
  Je unajuwa madaktari wanadai nini?

  Je unajuwa bajeti yenu unafanywa lini?

  Kumbuka hapo hakuna siasa za uCCM au uChadema. Ni utelekezaji tu. Kuna mambo yanaweza tatuliwa moja kwa moja na kuna mengine yanawezekana lakin yanabidi awe na subra kusubiri Bajeti ya 2012/2013 kama suala la ongezeko la mishahara.

  Acha ushabiki katika mambo sensitive kama haya.

 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Suala hapa ni mwajili na mwajiliwa kwa maana ya Serikali na madaktari kukaa kitako na kuzungumza. Hakuhitaji miujiza zaidi ya kuomba Kheir itawale shari pasi na shaka mambo yatakuwa sawia.

 10. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama ni serikali ya ccm siji kukubali kusikiliza msuluhishi kwa kuhonga na kuchakachua hoja ccm hawajmbo, hivyo sitaweza kaa meza moja na ccm labda waje kutoa taarifa kuwa wanakuja kuota taarifa kuwa madai yetu yote yamekubaliwa bila mabadiliko, hapo nitakaa. Kwa sasa Ccm hawana sura ya usuluhishi.
   
 11. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #11

Loading...