Mgogoro wa Machame na Kibosho

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
Kwanza nipende kuwaarifu kuwa hapo Mwanzo kabla ya utawala wa Sina hapakuwepo na uhasama kati ya Mashami na Kiwoso. Watu walikuwa wanashirikiana na kuoana toka sehemu zote mbili kama mahali pengine popote, ingawa kulikuwepo mgogoro midogo.

Sina ni jina Mangi Sina alilopewa na Wamachame kwa sababu ni mtoto wa kambo aliyekulia kwenye familia ya Mangi Shangali na alikuja Machame wakati mama yake alipoolewa na Mangi. Unajua tena wakati ule Mangi alikuwa anaoa wake wengi. Sina alipewa jina hilo kwa sababu ya kupenda kula nyama zenye mifupa.

Wakati alipopelekwa kutawala sehemu ya Kiwoso, watu wa Kiwoso waliomba mtawala kutoka kwa Mwitori (Mangi Shangali) kwa sababu Mchili aliyekuwepo alikuwa amekufa.

Kwa sababu ilipambana na kipindi ambacho Mangi Shangali alikuwa amegawa jimbo la Hai kwenye sehemu tano, basi Sina akatawazwa kuwa Mangi wa Kiwoso.

Alipoanza kutawala Kiwoso alikuwa anafahamu siri nyingi za Mangi wa Hai na Mashami kwa sababu ni mtoto aliyekulia kwenye familia ya Mangi. Alikuwa anawafahamu majemadari wote wa vita wa Machame. Lakini alingiwa na tamaa ya kutawala Hai yote na kama angechukua Mashami basi lengo lake lingetimia maana ndipo kulikuwepo na Mangi Shangali.

Ili kutekeleza lengo lake, Mangi Sina alijifanya kuwa amekufa na taarifa ilipelekwa kwa Mangi Shangali. Mila iliyokuwepo ni kwamba Mangi akifa anakwenda kuzikwa na majemadari.

Majemadari wa Mashami waliondoka kwenda Kiwoso kwenye Msiba kushirikiana na wenzao wa Kibosho
Walipofika kwenye Ngome ya Mangi Sina walitakiwa waache silaha zao nje.

Dada zao waliokuwa wameolewa Kibosho waliona huruma kwa ndugu zao watakavyoingia kwenye shida na wakawa wametoboa ndizi kwa vijiti na kutupa njiani ili watakapoona wakimbie wajue siyo msiba bali ni vita. Lakini ni majemedari wawili tu walitambua na kutoroka kupitia msituni.

Walipoingia kwenye Kasri kumbe Sina alikuwa amechinja mbuzi akamwacha aoze na alinuka wakaona wafanye kuzika haraka. Kabla ya kufanya hivyo ndipo wajemedari wote walioingia kwenye Kasri waliuawa na waliofanikiwa kutoka nje ya Kasri walijikuta wakikimbizwa kuelekea kwenye dimbwi kubwa lilikuwa kwenye mto uliokuwa karibu na Kasri. Jeshi lote la Mashami lenye nguvu za kivita na ulinzi liliishia huko. Kwa Mashami ulikuwa msiba mkubwa kwa sababu karibu kaya zote zilikumbwa na msiba (ni kama mithili ya yaliyotokea Rwanda).

Mangi Sina alijua tayari nimeshadhoofisha utawala Mashami na akataka kuja kuvamia Mashami. Lakini kwa bahati mzuri au mbaya ndipo na mkoloni akaingia na Mangi Shangali aliwapokea na ndipo wakaleta usuluhishi wa kupoozesha mgogoro huo. Mangi Sina hakuweza tena kuendelea na lengo lake.

Mgogoro huu ulileta laana ambayo imegawanya hizi sehemu mbili. Maana Wamashami waliweka uhasama kuwa:

-Wamashami wote wakijenga nyumba milango au mbengye haiwezi kuelekezwa Kiwoso.

-Wamashami walikuwa wakipita kwenye ardhi ya Kiwoso walitakiwa wabebe kibuyu. Ni afadhali wakojoe kwenye kibuyu kuliko kukojoa kwenye ardhi ya Kiwoso.
-Hakuna tena mtoto wa Mashami kuoa au kuolewa Kiwoso.

Hapo nyuma miaka ya 1960-1980 kulikuwepo na msemo kuwa Dimbwi walipofia Majemedari wa Mashami lilikuwa linachemka na kutoa sauti na lilikuwa linawaletea shida zile familia zilizoshiriki kwenye mauaji. Ili kulituliza watoto walikuwa wanakuja kuibiwa Mashami na kutumbukizwa kwenye hilo Dimbwi . Hatujui kama hayo mpaka wakati huu yapo

Ninatoa rai kwa Wakuu wa Dini na Kiroho (Wachungaji, Maaskofu, Manabii na wengine wanaofanana na hao). Kukutanisha wawakilishi au wakaaji kutoka Kiwoso na Mashami ili kufanya maombi maalumu (special prayer) kuomba kwa Damu ipitayo Damu zote (Damu ya Yesu) ili kuondoa hii laana ambayo imekwenda kwenye vizazi vingi, ili watu wa sehemu hizi mbili wafunguliwe na wawekwe huru. Neno la Mungu linasema yote yanawezekana kwa yeye aaminiye.
 
Mleta mada una hoja hili tatizo la kuzaa ndani na nje ya ndoa lina matatizo makubwa mfano waisraeli na wapalestina wanatwangana hadi leo watoto wa baba mmoja ila mama tofauti .Baba yao wote ni mangi IBRAHIM Mangi wa WAISRAEL aliyezaa Isaka baba yao akazaa mtoto mwingine Ishmael kwa mama mwingine wa kufikia ambaye ndie baba yao waarabu wapalestina

Kila mmoja anachukia mwenzie na kwa mwenzie hilo tatizo naliona ndio liko kwenu

wanume waache kuzaa zaa ovyo
 
Historia hii ingekuwa tamu zaidi kama ungeweka miaka na majina ya hao majemedari wa mashami! Pia uwaandikie Dr shoo Askofu wa kkkt DK na mwenzake Askofu Ludovick Minde wa Jimbo Katoliki Moshi na wengine ili waongoze upatanisho uliopendekeza?
 
Nimekuelewa sana. Ni kweli upatanisho unawezekana ila wachaga watataka wamwage damu ya wanyama kama patanisho ma pia watupie kidogo mbege na wasalie mizimu yao
Historia hii ingekuwa tamu zaidi kama ungeweka miaka na majina ya hao majemedari wa mashami! Pia uwaandikie Dr shoo Askofu wa kkkt DK na mwenzake Askofu Ludovick Minde wa Jimbo Katoliki Moshi na wengine ili waongoze upatanisho uliopendekeza?

Au mnasemaje mods
 
Hii vita ya sina mpaka akajifanya amekufa imewahi kuletwa umu kwa kirefu
 
Hawa wasimuliaji wanatofautiana kuna wengine wanasema Mangi wa mashami alitaka kulitawala eneo loote la kibosho lakini huyo sina alikuwa korofi na akapata taarifa baada ya kujifanya ammekufa mangi wa wamexhame alikuja na watu wake kuja kuwagawia maeneo. Alipotaka kuushuhudia mwili wa marehemu alifumuliwa ubongo na sina na watu wake wote waliuawa
 
Soon watabadilika ni suala la muda kwasabababu wameishaanza kuchangamana na jamii za makabila mengine na kujifunza utamaduni mpya ila wamachame wanajiharibia wanawake wao wakatili sana wana falsafa ya kuua mume ndio prestige wanaume wote waliooa machame wanaisoma namba namfaham mama mmoja alimtumia majambazi mmewe wamuuwe baada ya kumaliza ujenzi wa hotel jamaa alikua anaitwa Kweka
 
Back
Top Bottom