Mgogoro wa kisiasa Zanzibar!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Nini sababu ya msingi hasa ya kufuta uchaguzi na kuurudia upya?

Kama kweli wewe una hofu ya Mungu na unataka tumtangulize Mungu kwa kila jambo basi nijibu swali langu kwa ufasa ndani ya yakini ya moyo wako!

Nje na hapo basi ni ushetani kufanya aliyoyaharamisha Mungu na hata siku ya kiyama wewe utakayekula haramu utakua kundi moja na huyo sheitwani na familia yake.
 
Kwa kuwa mshindi wa ccm hakushinda, wala usihangaike kutafuta kitu kingine chochote kile chini ya jua.
 
Hivi jecha atalindwa kama rais maisha yake yote?, nani atagharamia hizo gharama za kumlinda?
 
Nini sababu ya msingi hasa ya kufuta uchaguzi na kuurudia upya?

Kama kweli wewe una hofu ya Mungu na unataka tumtangulize Mungu kwa kila jambo basi nijibu swali langu kwa ufasa ndani ya yakini ya moyo wako!

Nje na hapo basi ni ushetani kufanya aliyoyaharamisha Mungu na hata siku ya kiyama wewe utakayekula haramu utakua kundi moja na huyo sheitwani na familia yake.

Jibu ni rahisi tu! Unguja na Pemba ni nchi ya mtu mweusi kama mimi na hivyo Mwarabu, Muhindi, Persia hatuwezi kuruhusu tena waongoze visiwa vyetu, ni rahisi ki hivyo tu!
 
Sababu ya msingi hasa ya kufuta na kurudiwa uchaguzi ni hii: Mgombea wa ukawa kupitia cuf, Maalim Seif kutangaza idadi ya kura alizopata yeye na zile alizopata Dr. Shein. Tafsiri ya tendo hili ni kwamba alijitangaza mshindi. Hili ni kosa kubwa, alivunja sheria za ZEC ambayo ni mamlaka pekee inayopasa kutangaza kura za kila mgombea na hatimae mshindi. Nashangaa kwanini Maalim Seif hajachukuliwa hatua za kisheria.
 
Maalim SEIF KUJITANGAZA MSHINDI

BAADHI YA KARATASI ZA MATOKEO HASA ZILIZOTOKA PEMBA KUONEKANA ZIMEFUTWA...hii ni ishara ya uchakachuaji.

Baadhi ya vituo kuwa na idadi ya wapiga kura kuliko waliojiandikisha hasa huko pemba...hii ni ishara ya uchakachaji

Kwa ufupi ziko sababu tisa zilizotolewa na mamlaka ya kusimamia uchaguzi Zanzibar....

HATA MUNGU ANATUTAKA TUHESHIMU MAMLAKA(ZEC)
 
je Tanganyika sio ya mtu mweusi basi kurunzinza anweza kuja kutawala tanganyika
 
Sababu ya msingi hasa ya kufuta na kurudiwa uchaguzi ni hii: Mgombea wa ukawa kupitia cuf, Maalim Seif kutangaza idadi ya kura alizopata yeye na zile alizopata Dr. Shein. Tafsiri ya tendo hili ni kwamba alijitangaza mshindi. Hili ni kosa kubwa, alivunja sheria za ZEC ambayo ni mamlaka pekee inayopasa kutangaza kura za kila mgombea na hatimae mshindi. Nashangaa kwanini Maalim Seif hajachukuliwa hatua za kisheria.
Angetangaza baada ya kitangaziwa na tume tungemuelewa...lakini alipotangaza yeye alijipa mamlaka ya ZEC...Na aliwataka NEC wamtangaze kwa kutumia hayo matokeo yake ya kuchakachua...

tarehe 20 machi kutakuwa hakuna fursa ya kupika matokeo....!
 
Nini sababu ya msingi hasa ya kufuta uchaguzi na kuurudia upya?

Kama kweli wewe una hofu ya Mungu na unataka tumtangulize Mungu kwa kila jambo basi nijibu swali langu kwa ufasa ndani ya yakini ya moyo wako!

Nje na hapo basi ni ushetani kufanya aliyoyaharamisha Mungu na hata siku ya kiyama wewe utakayekula haramu utakua kundi moja na huyo sheitwani na familia yake.
Hili swali aliye asisi haya yote na kumtuma Jecha ana majibu yote lakini ngoja nivae kiatu chake, KUFUTWA KWA UCHAGUZI KUMELETWA NA KUSHINDWA, KURUDIA UCHAGUZI NI MKAKATI WA KUJIPANGA UPYA KUCHEZA RAFU.
 
Jibu ni rahisi tu! Unguja na Pemba ni nchi ya mtu mweusi kama mimi na hivyo Mwarabu, Muhindi, Persia hatuwezi kuruhusu tena waongoze visiwa vyetu, ni rahisi ki hivyo tu!
Hata Marekani ilikuwa hivyo mwishowe siku ya Obama ikafika!!! Just the matter of time!!!
 
Nini sababu ya msingi hasa ya kufuta uchaguzi na kuurudia upya?

Kama kweli wewe una hofu ya Mungu na unataka tumtangulize Mungu kwa kila jambo basi nijibu swali langu kwa ufasa ndani ya yakini ya moyo wako!

Nje na hapo basi ni ushetani kufanya aliyoyaharamisha Mungu na hata siku ya kiyama wewe utakayekula haramu utakua kundi moja na huyo sheitwani na familia yake.

Kama unaongelea Mungu kwa maana ya Allah basi hakuna sababu kabisa ya kufanya uchaguzi.
 
Sababu ya msingi hasa ya kufuta na kurudiwa uchaguzi ni hii: Mgombea wa ukawa kupitia cuf, Maalim Seif kutangaza idadi ya kura alizopata yeye na zile alizopata Dr. Shein. Tafsiri ya tendo hili ni kwamba alijitangaza mshindi. Hili ni kosa kubwa, alivunja sheria za ZEC ambayo ni mamlaka pekee inayopasa kutangaza kura za kila mgombea na hatimae mshindi. Nashangaa kwanini Maalim Seif hajachukuliwa hatua za kisheria.
sasa kama ni hivyo kwa nini wasimtangaze Shein kuwa mshindi? maana hata mimi sasa hivi natangaza matokeo ya atakayeshinda kwenye uchaguzi wa marudio kuwa atakuwa mgombea wa ccj, je watafuta matokeo?
 
Wenye kutangaza wamesema uchaguzi umefutwa, nani amtangaze Shein ndo mshindi?

Ukitangaza wewe, uchaguzi hauwezi kufutwa kwa sababu huna impact yoyote katika mchakato mzima wa uchaguzi. Sana sana utaonekana ni mshabiki, mpuuzi au mlevi fulani. Usifanye hivyo.

Umesema '............ATAKUWA mgombea ccj ......' duhh naona sasa unatoa unabii. Uchaguzi hauwezi kufutwa kwa tangazo la nabii, sana sana utaitwa nabii wa uongo. Usifanye hivyo. Upo?
 
Maalim SEIF KUJITANGAZA MSHINDI

BAADHI YA KARATASI ZA MATOKEO HASA ZILIZOTOKA PEMBA KUONEKANA ZIMEFUTWA...hii ni ishara ya uchakachuaji.

Baadhi ya vituo kuwa na idadi ya wapiga kura kuliko waliojiandikisha hasa huko pemba...hii ni ishara ya uchakachaji

Kwa ufupi ziko sababu tisa zilizotolewa na mamlaka ya kusimamia uchaguzi Zanzibar....

HATA MUNGU ANATUTAKA TUHESHIMU MAMLAKA(ZEC)
Tayari Pemba ni nchi na UNguja ni nchi jesha shein mkapa mwinyi na magufuli hii zambi itawafuata hata ndani ya makaburi yao
 
Jibu ni rahisi tu! Unguja na Pemba ni nchi ya mtu mweusi kama mimi na hivyo Mwarabu, Muhindi, Persia hatuwezi kuruhusu tena waongoze visiwa vyetu, ni rahisi ki hivyo tu!
Acheni ubaguzi mbona mweusi anaongoza America?
 
Wacha kulinganisha vitu visivyolingana, ni nani anamiliki Marekani? Ni nani anamiliki Uchumi wa Marekani? Kuna siku Mzungu aliwahi kutawalia na kufanywa mtumwa na mtu mweusi? Kuna siku Mzungu wa Marekani aliwahi kubaguliwa na mtu mweusi?
 
Basi wekeni ubaguzi wenu kwenye katiba hao uliowataja wasiruhusiwe kugombea urais.
 
Sijawahi kusikia popote eti mtu anaruhusiwa kugombea lakini haruhusiwi kushinda, only in tanzania.
 
Huyo jecha mzuri kipindi hiki subili wamalize uchaguzi hakuna takaye kuwa na habali naye hatokuwa na ulinzi wowote atalalamika tu ipo siku anamtumikia shetani
 
Back
Top Bottom