nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,858
- 2,348
Habari wanajamvi,
Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.
basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.
Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura
Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa
Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya
Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.
Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.