MGOGORO WA ARDHI

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,269
7,771
Kuna mgogoro umemkumba jirani yetu hapa na ulipofikia anahitaji msaada wa kisheria. Huyu mama ana mtoto wa miaka 6 na Mme wake alifariki mwaka 2016. Marehemu aliacha watoto 5 na wake wawili na huyu mama ni mke wa pili. Kwa mke mkubwa Mali zilizoachwa na marehemu ni; nyumba, powertiller , ng'ombe 35, pikipiki, shamba la mahindi hekari 15, shamba la mpunga hekari 16. Kwa mke mdogo aliacha nyumba ambayo haijaisha ukarabati na shamba la mpunga hekari 10, ikumbukwe shamba hili alilitafuta marehemu na mke mdogo.

Wakati wa msiba ndugu walizuia taratibu za kumaliza msiba na kuomba kila mke atunze kile alichoachiwa na marehemu wakati taratibu za milathi na kumaliza msiba ziliposimama. Hapo kwamaana kuwa wataendeleza vile alivyoacha marehemu. Mke mkubwa aliuza ng'ombe 20 ndani ya mwaka mmoja na huku akiendelea kusimamia mashamba. Huku mke mdogo nae akiendelea kulima shamba la mpunga zile hekari 10.

Tarehe 28/08/2018 mtoto mkubwa wa marehemu alifungua shtaka katika baraza la ardhi la kijiji akitaka mama yake mdogo amkabidhi shamba la mpunga. Baraza lilisikiliza maelezo ya pande zote mbili, huku mlalamikaji akidai kuwa mama yake (mke mkubwa) ameishiwa kiuchumi na sasa anachoma mkaa kujinusuru hivyo analihitaji hilo shamba alime ili amuinue. Maamuzi ya baraza la kijiji ni kuwa maamuzi ya kikao cha mwisho cha familia yafuatwe kwamaana kuwa kila mmoja asimamie alichoachiwa mpaka milathi itakapo toka.

Leo tar 18/09/2018 amemfikisha mama yake mdogo katika baraza la ardhi la kata. Baada ya kusomewa shtaka la kuzuia ardhi mke mdogo amekana mashtaka. Baraza limemtaka mlalamikaji kulipa sh 15000/= kama ghalama za kufungulia mashtaka. Pia limewataka kutoa kila mmoja kiasi cha sh 200,000/=(laki mbili) jumla laki NNE kama ghalama za kufika eneo la shamba lililopo umbali wa km 12.

Msaada unahitajika katika mambo yafuatayo.
1: Kesi hii kwa mtazamo wa kisheria ni nani mwenye uhalali wa kulimiliki na kulima kwasasa?

2: Je ghalama hizi ni sahihi au kuna dalili za utapeli?

3: Maamuzi ya ndugu wakati wa kumaliza msiba yataweza kutengua hukumu itakayotolewa baada ya kesi hii?.

4:Mama huyu afanyeje amilikishwe eneo yeye?
 
Ok! Kitu cha msingi muda huu! ANGALIENI KAMA MAREHEMU ALIACJA WOSIA, Chagueni msimamizi wa mirathi, nendeni mahakamani akapate uthibitisho kama msimamizi wa mirathi then agawe hizo Mali kulingana na WOSIA (kama utakuwepo) kama hamna basi angalieni maisha ya marehemu aliishije ili mapate namna ya kugawa Mali

*kuhusu nani mwenye mamlaka ya kulima kwa sasa kwa vile kikao kiliamua shamba libaki kwa mke mdogo then yeye ndiye mwenye haki adi hapo msimamizi wa mirathi atakapo gawa Mali

*kuhusu gharama za kwenda kuona shamba MAHAKAMA ndiyo yenye kujibu hapa

*kwa msaada zaidi ANITAFUTE KWA "FURTHER LEGAL ADVISE"
 
Ok! Kitu cha msingi muda huu! ANGALIENI KAMA MAREHEMU ALIACJA WOSIA, Chagueni msimamizi wa mirathi, nendeni mahakamani akapate uthibitisho kama msimamizi wa mirathi then agawe hizo Mali kulingana na WOSIA (kama utakuwepo) kama hamna basi angalieni maisha ya marehemu aliishije ili mapate namna ya kugawa Mali

*kuhusu nani mwenye mamlaka ya kulima kwa sasa kwa vile kikao kiliamua shamba libaki kwa mke mdogo then yeye ndiye mwenye haki adi hapo msimamizi wa mirathi atakapo gawa Mali

*kuhusu gharama za kwenda kuona shamba MAHAKAMA ndiyo yenye kujibu hapa

*kwa msaada zaidi ANITAFUTE KWA "FURTHER LEGAL ADVISE"
OK thanks
 
Kwa mjibu wa Sheria watoto na Mali zingine ni Mali za mke na mme!!! Hivyo anapofariki mme ni lazima kikae kikao Cha ukoo ili waweze kuteua msimamizi wa mirathi na Kisha waende mahakama ya mwanzo au wilaya akathibitishwe usimamizi wake!! Kazi kubwa ya msimamizi wa mirathi ni kudai,kudaiwa madeni yote aliyeacha marehem na kusimamia Mali na kuhakikisha mgao unafanywa kwa wanufaika wote!! Hivyo basi wote waliokwenda baraza la Kijiji au kata hawakuwa na mamlaka kisheria kudai kuwa ile Mali either ni ya mke kubwa au vinginevyo. Mpaka hapo atakapoteuliwa msimamizi wa mirathi. Kwa mjibu wa utaratibu hizo Mali zinapaswa kubaki Kama zilivyokuwa zinatumika hapo awali mpaka hapo watakapoteua msimamizi wa mirathi. Kuhusu baraza la kata . Mara nyingi mabaraza ya kata hayana mafungu ya kujiendesha na wajumbe wake Mara nyingi hawana weredi wa Sheria zaidi saana busara. Hivyo inapotokea Kama Kuna site visiting wadaawa wote huchangia hizo gharama Kama ni laki mbili basi kila upande hutoa nusu !!! Kwa hali hiyo waende kwa afisa mtendaji wa kata ambae ndie msimamizi wa baraza Hilo ili akamwambie kuwa gharama alizoambiwa ni vyema pande zote mbili wakachangia.
 
kwa vyovyote vile mtu anapokufa , kama alikuwa anamiliki mali lazima hata kama aliacha wosia kesi ya mirathi ifunguliwe haraka iwezekanavyo, na kitaratibu hairuhusiwi kuuza ama kumilikisha ama kuhamisha kwa njia yoyote kabla mahakama haijamthibitisha msimamizi wa mirathi. Ninachokiona hapa ndugu wamefanya kosa kubwa sana kuruhusu mgogoro huu kwani baada ya kikao cha wanaukoo walitakiwa wamchague msimamizi wa mirathi ambaye angekwenda kufungua kesi ya mirathi. Katika kesi hiyo ndio mali zote za marehemu zingeorodheshwa na wategemezi wake wote, katika kesi hiyo kama kuna mtu ana pingamizi lolote ama hoja kuhusu mali hizo angeongea mahakamani na mahakama wakati wahukumu na kutoa asilimia ya mgao wa mali za marehemu inezingatia hoja zote ikiwa ni idadi ya mali za marehemu, wake na watoto wake, ushiriki wa wake hao katika kuchuma mali hizo pamoja na wosia kama upo ama kama hauna upendeleo. Mwisho washaurini shauri la mirathi lifunguliwe na sio shauri la umiliki wa mali kwanza.
 
2. Kabla ya mahakama ya mirathi kutoa hukumu hilo baraza la ardhi la kata halina mamlaka ya kuanza kusuluisha mgogoro wa ardhi kwani bado ni pre mature. Baraza la ardhi litatumika tuu kwama mtatuzi ama msikilizaji wa kwanza wa shauri la ardhi kwa mujibu ya sheria ya ardhi pale ambapo suala la mgao limishafafanuliwa na mahakama wanaenda kutembelea mali za marehemu kwani wamekuwa ndio wasimamizi wa mirathi?. Hivyo suala la kutoa fedha kwenda kutembelea eneo ni ukanjanja. Cha msingi mambo yote kwa sasa yakajadiliwe kwenye kesi ya mirathi
 
Baraza la ardhi la kata halina mamlaka na shauri hili, hili ni shauri la mirathi ambalo linaenda mahakamani na sio baraza la ardhi la kata, sasa wanaenda shambani kufanya nini? Kugawa au kufanyanyeje? Hiyo kazi ya kugawa mirathi wameitoa wapi?
 
Back
Top Bottom