Mgogoro wa ardhi ya mirathi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa ardhi ya mirathi?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KISHOKA_ZUMBU, May 20, 2012.

 1. KISHOKA_ZUMBU

  KISHOKA_ZUMBU Senior Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  wanasheria wa jf tafadhari naomba msaada wa ushauri wa kisheria kuhusiana na mgogoro wa ardhi iliyouzwa na msimamizi wa mirathi.

  Marehemu alikuwa amezaa na wanawake watatu tofauti, mke wa kwanza ana watoto watano, mke wa pili alizaa nae watoto wawili, mimi ni mmoja wapo, mke wa tatu alizaa nae mtoto mmoja (marehemu kwasasa).

  1. Msimamizi alichaguliwa 1998 (mtoto wa kwanza kutoka nyumba ya mke mkubwa mwenye watoto watano)
  2. Mwaka huo huo aligawa mali za marehemu kwa warithi (watoto). Hapa hakuandika popote kuhusu mgao huo, lakini alishirikisha ndugu akiwapo kaka wa marehemu na baadhi ya watoto wa marehemu.
  3. Sisi watoto wawili wa nyumba ya pili tulipewa uwanja, watoto wa nyumba kubwa (wale watano walipewa nyumba na kila kilichopo ndani yake), mdogo wa mwisho alipewa banda la uani ili kodi yake imsaidie kulipa ada ya shule.
  4. Kwa kuwa mimi na mdogo wangu ni watu wa kujishughurisha kutafuta maisha mbali ya mji wa marehemu mzee, tulikaa kwa muda mrefu bila ya kuandikishiana na msimamizi wa mirathi kuhusu mgao.
  5. Mwaka 2009 msimamizi aliamua kuuza kile kiwanja alichotugawia bila taalifa yetu wala ruhusa yetu.
  6. Tulifanikiwa kumuita kwenye mahakama iliyomteua kuwa msimamizi wa mirathi kumhoji kwanini aliamua kuuza ardhi aliyogawa kwa wadogo zake.
  7. Alidai kuwa hiyo ilikuwa ardhi yake aliyopewa na baba kabla ya kufa, lakini alipotakiwa kutoa udhibitisho wa maandishi ku-support madai yake hayo, hakuwa nayo.
  8. Baada ya hakimu kumuelimisha wajibu wa msimamizi wa mirathi, aliamua kukiri mbele ya hakimu yeye mwenyewe na kuandika kwa mkono wake kuwa mali aliyouza si mali yake na kuwa kuanzia pale anarudisha kwa wenyewe ambao ni mimi na mdogo wangu.
  9. Baada ya kupata hati ya kukiri ya msimamizi wa mirathi tulienda balaza la ardhi la kijiji na kuwaonyesha, wao wakatoa stop order kwa mnunuzi asiendeleze ujenzi
  10. Lakini mnunuzi aliamua kuendeleza ujenzi.
  11. Tulifungua shauri la mgogoro wa ardhi balaza la ardhi la kata, lakini tuliona ubabaishaji mwingi unaofanyika kutokana na mnunuzi kumwaga fedha.
  12. Tulihamisha shauri hadi balaza la ardhi la wilaya.

  Madai ya msimamizi na mnunuzi.
  1. Alipewa na marehemu kabla ya kufa, hati hana.
  2. Anasema hatutambui sisi kama ni watoto wa marehemu, lakini wakati namhoji maswali alikubali mahakamani kuwa aliwahi kuambiwa na marehemu kuwa kuna watoto wengine wawili, yaani mimi na mdogo wangu.
  3. Ameleta mashahidi wanadai hawatutambui
  4. Mashahidi wake wanadai eneo alilouza kaka yao ni haki yake.

  Mambo niombayo msaada:
  1. Kati ya kaka wa marehemu na mtoto wa kwanza, nani anakubalika kisheria kuwatambua watoto wa marehemu?
  2. Kama akiendelea kudai kuwa hatujui, mahakama inaweza kuchukulia uzito hoja yake?
  3. Je ile hati ya kukiri mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo inaweza kuwa na nguvu ya kisheria kumbana?
  4. Wao wameweka wakili, waliita mashahidi watano. Je mashahidi wanaweza kutoa ushahidi kabla ya mdaiwa kujieleza mbele ya mahakama? Na ikifanyika hivyo wadaiwa wakiwepo kotini si kukosea utaratibu wa kutoa ushahidi?
  5. Je inawezekana hakimu huyu nae kala mlungula ili atukandamize?
  6. Je tufanyeje katika hili la hakimu, tunaweza kulipoti takukuru ili wamfuatilie?

  Naombeni ushauri wenu tafadhari.
   
Loading...