Mgogoro wa Ardhi Kivule: Hii imekaaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa Ardhi Kivule: Hii imekaaje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mama Mdogo, Oct 27, 2012.

 1. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Hii imekaaje, viongozi wetu wanatakiwa walinde wananchi au wawasumbue wananchi????

  PART ONE

  WANANCHI wanaoishi maeneo ya Kivule mpakani mwa Wilaya ya Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam, wameiomba Serikali kudhibiti kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA), kuvunja nyumba zao, wakati mgogoro wao wa ardhi ukiwa bado mahakamani.

  Mjumbe wa Shina namba 26 Mtaa wa Magole, Kata ya Kivule, Moris Kaombwe, alisema wananchi hivi sasa wanaishi kwa wasiwasi, kutokana na kikundi hicho kuvamia makazi yao nyakati za usiku na kuvunja nyumba zao, pamoja na kung'oa mboga katika bustani zao.

  Kaombwe alisema, wanahusisha uvamizi huo na UVIKIUTA, kwani wana ugonvi wa kugombea mpaka na tayari kesi yao ipo mahakamani.

  "Mgogoro wetu na UVIKIUTA upo mahakamani, hivyo tunashangazwa na hatua za kuvunjiwa nyumba zetu, na huo ni ukiukwaji mkubwa wa utawala wa sheria, ni vema sote tusubiri uamuzi wa mahakama.

  "Lakini pia tunashangazwa na kikundi hicho, kudai eneo hili ni lao, wakati wao wako Temeke na sisi tuko Ilala, na katika zoezi la sensa mwaka huu, tulihesabiwa kama wananchi wa Ilala, sasa nani ni mkweli wa kufahamu mipaka hii, ni Serikali au UVIKIUTA?," alisema na kuhoji Kaombwe.

  Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro huo, John Anania, alisema vijana wanaohusika na ubomoaji wa nyumba zao, wanakuwa wamevalia fulana nyekundu na suruali nyeusi, huku wakipeperusha bendera nyekundu na kuimba nyimbo mbalimbali.

  Alisema hali hiyo, imezusha hofu miongoni mwa wananchi, ambapo Serikali isipoithibiti inaweza kusababisha mauaji na vita ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo hilo.

  "Kero yetu ni hawa majirani zetu UVIKIUTA, kwa kumtumia kiongozi wa Serikali hapa Dar es Salaam, wanatuma watu kubomoa nyumba za watu usiku ndani ya makazi, yanayopakana na makazi ya kikundi hicho.

  "Hali hii ya uchokozi wa makusudi, ikiendelea inaweza kusababisha mauaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo hili, hatutaki tufike huko, tunaiomba Serikali ichunguze kikundi hiki kinachotaka kuhatarisha amani kwa wananchi wake," alisema Anania.

  Naye, mlezi wa UVIKIUTA, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, alipoulizwa alisema, amri ya kuvunjwa kwa nyumba zilizojengwa katika eneo la mgogoro, ilitolewa na Baraza la ardhi la Temeke, baada ya Wakili wake kulalamika kwamba, wavamizi wanaendelea na ujenzi katika eneo hilo lenye mgogoro.

  Alisema mahakama, ndiyo iliyoidhinisha na kuteua dalali wa kuvunja nyumba hizo, hata hivyo alipoulizwa ni lini Mahakama hiyo, ilimteua dalali huyo, alisema aliteuliwa jana, muda ambao tayari nyumba hizo zilikwisha kubomolewa tangu wiki iliyopita.

  Eneo la Kivule lenye mgogoro, lina ukubwa wa zaidi ya ekari 600, na wakazi zaidi ya 1,000 tayari wameweka makazi ndani ya eneo hilo, ambapo wanadai kuwa, eneo hilo ni mali yao na mpaka unaowatenganisha na UVIKIUTA ni barabara na si vinginevyo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala (RPC), Marietha Komba, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema hana taarifa, ameahidi kulishughulikia.

  Vitendo vya jamii kujichukulia sheria mkononi, vimezidi kushamiri katika miaka ya hivi karibuni, ambapo baadhi yake vimesababisha maafa, yakiwemo mauaji ya watu wasio na hatia na uharibifu mkubwa wa mali za wananchi.

  Source: Wananchi wataka UVIKIUTA idhibitiwe


  PART TWO


  WAKAZI zaidi ya 600 wanaoishi eneo la Kivule katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, wameazimia kumburuza mahakamani Mkuu wa Wilaya (DC) ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, kwa madai ya kutumia cheo chake vibaya na kutaka kuwanyang'anya ardhi wanayomiliki kihalali.
  Wakizungumza na Tanzania Daima jana, wakazi hao walieleza kushangazwa na kitendo kilichofanywa na Rugimbana cha kufika katika eneo hilo lenye hekari zaidi ya 372 na kugawa vipeperushi vya kuwataka wakazi hao kuondoka kwa hiyari kabla ya kubomolewa nyumba zao.

  Akizungumza kwa niaba ya uongozi uliochaguliwa na wakazi hao, mjumbe wa kamati ya mgogoro huo, Barton Kigola, alisema mkuu huyo wa wilaya anatumia nguvu aliyonayo kutaka kuwaondoa katika eneo hilo, hivyo watamfikisha mahakamani ili waweze kutetea haki yao. Kigola alisema mbali na kutumia nguvu aliyonayo, pia hukitumia kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (Uvikiuta) kuchukua ardhi hiyo.

  "Hatuelewi kiongozi huyu anapata wapi idhini ya kutupokonya ardhi na hatuelewi kwanini anataka ardhi yote hii? Hata hivyo tunaiomba serikali wakichunguze kikundi hicho ambacho jina lake haliendani na matendo yake," alisema.

  Alisema eneo hilo lilikuwa mashamba ya wazawa ambapo mwaka 1974 baadhi ya wananchi waliondolewa katika operesheni vijiji na Rais wa awamu ya kwanza, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
  Kigola alisema kutokana na wazawa kushindwa kulipwa fidia walilazimika kurudi katika maeneo yao na kuyaendeleza hadi sasa unapojitokeza mgogoro huo.

  John Anania, alidai kabla ya kugawa vipeperushi hivyo baadhi ya vijana waliopo wa Uvikiuta walivamia eneo hilo Oktoba 17, mwaka huu majira ya saa 8:00 usiku na kubomoa nyumba zaidi ya saba zilizopo katika eneo hilo kwa madai ya kutumwa na kiongozi huyo.

  Rugimbana alipotafutwa kuzungumzia madai hayo alikiri kuwa na uhalali wa eneo hilo na kumwomba mwandishi wa habari hizi kwenda ofisini kwake ili kuona nyaraka halali alizonazo za kumiliki eneo hilo.
  "Naomba tuwasiliane kesho kwa kuwa kwa sasa nipo nje ya ofisi, ili nikuonyesha ushahidi nilionao. Kuhusu kutumia nguvu ya madaraka si kweli, kama wanaona hilo, basi wanifikishe katika vyombo vya kisheria, naamini huko ndiko kuliko na haki," alisema Rugimbana.

  Source: Wakazi Kivule kumburuza DC kortini
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,217
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa hizi ma mdogo!
  Nayafahamu fika maeneo hayo tajwa, ingawa sikuwa najua kuwa kuna mgogoro wa ardhi. Ni ndugu yangu anaishi hilo eneo la Uvikiuta, ila hajaniambia kama wana mgogoro wa ardhi.
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mh, haya ndo' maisha bora kwa kila Mtanzania...
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,300
  Trophy Points: 280
  Nasubiri Part Three ambayo bila Shaka itakua ni Mapanga Style a.k.a Mfekane War.

  Mungu epushia mbali hii!!
   
 5. N

  Nafwachii Senior Member

  #5
  Aug 13, 2016
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 163
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  nmesikia hata mimi , wananchi bado wanaendelea na ujenzi maeneo haya....mahakama bado haijaliamulia suala hili....pia nilisikia viongozi wa eneo hilo wamekuwa wakiwachangisha pesa wakazi wa eneo hilo kwa pazia la kesi kumbe wanawapiga hizo pesa
   
 6. N

  Nafwachii Senior Member

  #6
  Aug 13, 2016
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 163
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  nmesikia hata mimi , wananchi bado wanaendelea na ujenzi maeneo haya....mahakama bado haijaliamulia suala hili....pia nilisikia viongozi wa eneo hilo wamekuwa wakiwachangisha pesa wakazi wa eneo hilo kwa pazia la kesi kumbe wanawapiga hizo pesa
   

  Attached Files:

 7. N

  Nafwachii Senior Member

  #7
  Nov 29, 2016
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 163
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  leo hii ubomoaji unaendelea haya maeneo,nilikuwa maeneo haya tukifanya survey ya kupitisha umeme
   
Loading...