Mgogoro mkubwa wafukuta TBC

Walipombwaga Tido walithani atatetereeka... Sasa ana bonge la ofisi Mwananchi. Poleni tbc
 

Hujamuelewa tu Pasco, ni mchimvi sana. Msome vizuri utaelewa.
Halafu kama unadhani hapendi taarifa kama hizi zitoke unakosea sana.

Angalia ikiwekwa Taarifa kama ya aina hii ni mwepesi kuchungulia na kuchangia!
 
Last edited by a moderator:
hata mtangazaji akiwa anatangaza taarifa utamwona anavyotangaza kwa unyonge kama amelazimishwa vile kumbe hajalipwa mshahara
Sio hilo tuu,hata kusoma habari ambazo ni uongo na uzushi wa dhahiri lazima sura na nafsi vitofautiane. Mfano umepewa scrip imeandikwa " Katika miaka 50 ya uhuru wetu chama Tawala CCM kimeboresha maisha ya Mtanzania kwa kiwango cha juu kuliko mataifa mengi kusini ya jangwa la Sahara na sasa ahadi ile ya maisha bora kwa kila Mtanzania imetimia ....."
Ndugu yangu hata ingekuwa wewe sura yako ingekuwaje wakati unasoma hako kasehemu? Najua moyoni ungekuwa unatukana.
 

Kwani siri ni nini hasa? Unashauri watu watunze siri hata kama mambo hayaendi vizuri !! Lengo hasa ni kulinda maslahi ya TBC au umma ? Kumbuka whistle blower ndo walifichua siri na hasara za makampuni makubwa kama Enron . Na kweli yali file bankrupt.

Kama watu wenye influence humu Jf kama wewe na muajiriwa kwa miaka mingi Tbc ,anaweza kutoa ushauri wa kuficha siri za kiovu makazini ,hasa taasisi za umma, watanzania tumeumia!
 
Kama watafungua bar mimi nitakuwa mteja namba moja. Namkumbuka sana tido muhando kwa ujasiri wake
 
Kwenye udini na ukabila wamezidi lol!
 
Pole TVT, nikisema TBC namkumbuka tirdo mhando.bora niite TVT.
 
muda si mrefu kitaeleweka,mshaanza kushikana uchawi! Ngoma inogile..kodi zetu zinawalaani.
hata senti moja ya mtanzania maskini haita kwenda bure,,nakwambia itakwenda na mtu,leo tbc wamepokwa watanzania na kupewa ccm,chombo ambacho ni mali ya watanzania,tbc imekua ni kijiwe cha ccm,inakwenda kukesha chimwaga kurusha live mambo ya chama,huku watanzania wakinyimwa hata burudani ya timu yao ya taifa inapocheza,matangazo yanakatizwa halafu kanajitokeza kamtu kanasema tunajiunga live dodoma chimwaga,huu ni upuhuzi ambao auwezi kuruhusiwa kuendelea kwenye mashirika ya uma,leo mtu yoyote wa ccm akitaka kupiga propaganda kwa cdm,huyoooooo tbc anapewa kipindi na kutekeleza mambo yake,nawapongeza sana hawa wafanyakazi wa tbc hambao hawataki tena kutumiwa na vibaraka wa ccm,,,,,na mimi nawaunga mkono huyu bw,mshana hafai hafai aendezake akapewe ukuu wa wilaya,na senti za kodi za watanzania zitawa tafuna,
 
Tido tido,tuna kukumbuka baba watanzania ulitupenda sana ukatupa burudani kutoka tvt mpaka tbc sasa chombo hiki kimekua mali ya chama cha mapinduzi,watanzania tunakosa[uefa] [afcon] [epl] baba hupo wapi hata tukkufuate watanzania tumekua kama yatima wanacho penda watawala ndio tunacho honyeshwa,baba nenda hata [ting] tutakkufuhata,,,mwenyezi mungu akulipie mema mjawake hulie tupenda sana watanzania,
 
Huyu jamaa (mushana) ameharibu TBC binafsi nilishaacha kufuatilia matangazo yao kwa sababu, imegeuzwa bango la CCM na viongozi wa serikali wee ukitaka kufahamu JK, mfalume wa nyuki (pinda), mawaziri n.k wako wapi na wanafanya nini angalia tbc.
 


Mkuu Mchai_chai_dawa
Naafikiana na wewe baadhi ya hoja zako, lakini nakuomba tafadhali hapo ulipo, fanya very simple survey jaribu kudodosa watu kumi Tu swali lifuatalo JE TAARIFA YA HABARI WANATAZAMA CHANNEL ZIPI TBC/ITV/STAR TV. halafu uje na jibu uwe mkweli.
 

Umelaaniwa wewe si bure. Watu wanatoa siri za magogoni wewe unasema siri za TBC zisitoke? Kama vipi waambie waajiri robots ambazo hazina hisia.
 
ucha kuongea kama siio mwanasheria kasema ukweli na ukweli ndio dira ya maendeleo bila ukweli nchi itayumba ukweli ndio utatuweka huru nampongeza mtoa mada
.
Mkuu Lokissa, hapa tunazungumzia vitu viwili tofauti, mimi nazungumzia utii wa sheria bila shuruti kwa kufuata, sheria taratibu na kanuni!, mimi niliwahi kuwa mtumishi wa umma, na miongoni mwa mambo ya msingi sana kwa mtumishi wa umma, ni pamoja na kutunza siri za serikali!.

Kusema ukweli daima is one thing, na utunzaji wa siri za serikali is another thing, kama ilivyo katika familia, unapogundua wife wako kacheza rafu, unatangazia majirani na mataifa?, ili iweje?. Utumishi wa umma umeweka kanuni na taratibu za kila jambo!, sasa hili la kuwatangazia mataifa matatizo yao ya ndani ndio ili iweje?!.

Hata hao wanasheria, nao wana yao ambayo wanayajua kwa ukweli halisi, lakini bado wanamshauri mteja wao akanushe!.

TBC ni taasisi nyeti, inayohitaji uvumilivu na ustahimilivu wa hali ya juu kuwepo pale!, sisi tulioshindwa hayo, tulifungwashwa virago vyetu tukatimuliwa!, na akipatikana aliyeyaleta haya humu jf, anatakiwa kufungashwa!. Channels za malalamiko zipo, hapa jf wanaleta mambo yao ya ndani ya nini?!. Huku ni kumwaga tuu mpunga kwenye kuku wengi!.

Pasco.
 
mkuu habari za kaisho, ile hoteli/ guest ya yule aliyekuwa mbunge - ipo mkono wa kushoto ukiwa unatoka Omulushaka unaelekea Murongo bado ipo?
Sijui kama tunahitaji TBC kwani tangu nizaliwe hapa maeneo yetu (kyerwa) inasikika usiku tu kupitia MW peke yake.
 
hivi hii tbc bado ipo? mie nilishapiga marufuku tv yangu kuonyesha hii kitu, huwa nahisi inanakula sana umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…