Mgogoro mkubwa wafukuta TBC

Mgogoro mkubwa wafukuta TBC

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
551
Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!
 
Hawana tofauti na TTCL na TANESCO
With time mtakosa ata matangazo ya kibiashara yanayowatia kiburi
 
Muda si mrefu kitaeleweka,mshaanza kushikana uchawi! Ngoma inogile..kodi zetu zinawalaani.
 
stashangaa kusikia CDM wahusika na kuna mtu ataonekana kwenye Video akipanga njama za kuangamiza shirika zuri la umma
 
Chadema wanahusika cc @Zermacorpolo
 
Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

Viva Tido Mhando; Tutakukumbuka sana kwa umahiri wako katika tasnia ya habari!! CCM walitumbukiza lulu chooni!!
 
Hivi yakitajwa mashirika ya habari Ulimwenguni eti TBC nao huwa wanajitokeza...phweeeee!!!
 
Ukipenda boga,penda na ua lake,ukiipenda TBC ipende na CCM,TBC+CCM=TBCCM(R.I.P)
 
Sijui kama tunahitaji TBC kwani tangu nizaliwe hapa maeneo yetu (kyerwa) inasikika usiku tu kupitia MW peke yake.
 
Inakufa kama bwana ake atakavyokufa 2015 heheheheehehehheeheh
 
afu wanakera kweri kweri...why hawaajili mashori wakali aisee?
 
irudishwe kuwa mali ya umma
mkurugenzi wake achujwe na bunge
iwe chombo huru kisichofungamana na upande wowote
hapo ndio itapata watazamaji
kwa sasa wacha ijifie tu kwani CCM wameshindwa kuwalipa wakati ni TV yao..TBCCM
 
Toka wamuondoe Tido wamekuwa kama mafuta yenye maji ,, kwanza hiyo si Chinatbc au !!!!
 
Back
Top Bottom