MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

Kutokana na kitendo walichokifanya UVCCM jana..cha kukemea na kukosoa viongozi wa serikali inayoongozwa na CCM, kuhusu kuilipa deni la DOWANS, bila kufuata taratibu kama kanuni zinazoongoza "jumuia" hiyo zinavyoelekeza, basi ni halali wahusika wote walioshiriki mpango huo watimuliwe katika nafasi za uongozi wanazozishikilia katika "jumuia" hiyo. Mimi binafsi sikubaliani na uamuzi wa kulipa deni la DOWANS, kilichonisukuma kutoa hoja hii ni ukiukwaji wa kanuni za UVCCM.Nawasilisha hoja kwenu WanaJF.

Ilakuilipa downs sikukiuka Kanuni? Nakamanikukiuka alietamka naaetakakutuibia mabilioni zitonilipi?
 
Hili la kutukana wao wanaona ni fashion...ukianza na ryeyemamu...uje wao...yaaani mashairi ya taarabu ndio principle yao kuu katika kujibu hoja...hata rais wao hivyo hivyo.......SIKU TUTAKAYO WATUNISI WATAJUTA...tumeshawachoka...miaka nenda rudi hali ni ile ile wao wanazidi kuneemeka...hii nchi ni ya wakulima na wafanyakazi na cio genge la wezi..
 
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoani Pwani umehoji matamshi ya mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa, ya kukikosoa Chama na serikali bila ya kufuata utaratibu, ukisema hatua hiyo inachochea machafuko nchini. Aidha, umemuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete, katika kukiboresha Chama aanze na kuirekebisha sekretarieti yake kwa kuwa imeshindwa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la UVCCM mkoa, Mwenyekiti wa UVCCM mkoani humo, Abdallah Ulega, alisema matamko yaliyotolewa na Sumaye na Lowassa hayaelekei kushauri, bali yalijikita katika ajenda binafsi zilizojificha. "Kila mmoja alimsikia hivi karibuni, Waziri Mkuu mstaafu, Sumaye akiitaka CCM kujibu hoja za CHADEMA na si kuiachia serikali, sasa unaweza kujiuliza CCM ni nani, kwa nini asitumie vikao vya Chama kushauri hilo, hata kama kulikuwa na uharaka kwanini asingekwenda kwa Mwenyekiti kumshauri jambo ambalo ni rahisi kwake?
"Pia, tumemsikia mzee wetu Lowassa naye akisema eti serikali ipandishe mishahara ya wafanyakazi, yeye mwenyewe alikuwa ndani ya serikali miaka miwili tu iliyopita, kwanini hakushauri hilo huko nyuma mpaka sasa aje aeleze tena si katika vikao vya Chama, bali kwa waandishi wa habari," alihoji Ulega.
Ulega alisema wapo viongozi ndani ya Chama ambao wamekuwa wakikiuka maadili na kufanya vile wanavyopenda wao bila ya kutazama athari za wanayoyasema kwa taifa.
Alisema viongozi wakuu serikalini hawamsaidii Rais Kikwete kwa kuwa wamekuwa wakijiweka pembeni na kushindwa kutetea mambo mbalimbali yanayokosolewa, ukiwemo mfumuko wa bei unaotajwa kuikumba nchi hivi sasa licha ya kuwa wanayo maelezo juu ya hilo.
Alieleza viongozi hao wakiwemo mawaziri, wamekuwa kimya hata pale wanapoona yapo mambo wanayoweza kuyatolea ufafanuzi kabla ya Rais Kikwete, lakini hawafanyi hivyo na kumuachia rais aeleze na kutetea kila jambo.
"Linapotokea jambo hakuna anayesema lolote... wanamwachia rais aseme na ikitokea wanazungumza basi wanasema ya hovyo," alisema.
Kwa mujibu wa Ulega, ipo dhana iliyojengeka miongoni mwa Watanzania kuwa urais ni lazima uende kwa watu wa upande fulani wa nchi, jambo ambalo si lazima kwa kuwa Tanzania ni moja na kila mmoja ana haki ya kuongoza hasa anapokuwa na sifa zinazokubalika.
"Tunafahamu kuwa upinzani umekuwa ukiongezeka kwa malengo fulani ya wahusika, hasa kutaka nafasi za kisiasa, lakini tunawaeleza wazi kuwa hawawezi kufanikiwa hayo wanayoyataka kwa kumharibia Rais Kikwete, na yeye ataendelea kuongoza hadi muda wake utakapokwisha," alisema.
Mwenyekiti huyo aliyekuwa akizungumza kwa kuwahamasisha vijana wa CCM kusimama kutetea mema ya Chama, alisema baadhi ya watu wanashindwa kusimama na kueleza au kukemea madudu yanayodaiwa kwa kuwa wamekuwa wakipokea fedha kutoka kwa wasiopenda mafanikio ya serikali, lakini kwake hilo halipo.
Alisema viongozi hao wanataka kuifikisha nchi pabaya, ilhali wao wameshaitumikia kwa muda mrefu bila ya kubughudhiwa na wanafanya hivyo sasa ili ikiwezekana hata machafuko yatokee.
"Nchi hii inaongozwa na CCM kutakapotokea lolote watakaopelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ni viongozi wake bila kujali nani ni nani, lazima tusimame tukemee, mimi nasema kwa kuwa sikula cha mtu, nipo huru nasema lolote," alisema.
Alimwomba Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kabla ya kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Chama, awatazame viongozi walioshindwa kuwajibika na kuwatosa kama kafara kwa wengine waliojificha na wasioitakia mema nchi.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, mbunge wa jimbo la Bagamoyo, ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema vijana wameshindwa kukitetea Chama mbele ya wanaopinga mafanikio kiliyoyaleta.
Dk. Kawambwa alisema licha ya mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu, bado vijana wanashindwa kutembea kifua mbele na kukitetea na kuacha wapinzani wakikishambulia kana kwamba hakuna jema lililotendeka.
Viongozi wa umoja huo kutoka mikoa mbalimbali walikuwa mingoni mwa waalikwa waliohudhuria mkutano huo, mbapo pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Ridhwan Kikwete, mbunge wa Mchinga, Said Mtanda na wanafunzi kadhaa kutoka vyuo vikuu nchini.
 
umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm), mkoani pwani umehoji matamshi ya mawaziri wakuu wa zamani frederick sumaye na edward lowassa, ya kukikosoa chama na serikali bila ya kufuata utaratibu, ukisema hatua hiyo inachochea machafuko nchini. Aidha, umemuomba mwenyekiti wa ccm taifa rais jakaya kikwete, katika kukiboresha chama aanze na kuirekebisha sekretarieti yake kwa kuwa imeshindwa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Akizungumza katika ufunguzi wa baraza la uvccm mkoa, mwenyekiti wa uvccm mkoani humo, abdallah ulega, alisema matamko yaliyotolewa na sumaye na lowassa hayaelekei kushauri, bali yalijikita katika ajenda binafsi zilizojificha. "kila mmoja alimsikia hivi karibuni, waziri mkuu mstaafu, sumaye akiitaka ccm kujibu hoja za chadema na si kuiachia serikali, sasa unaweza kujiuliza ccm ni nani, kwa nini asitumie vikao vya chama kushauri hilo, hata kama kulikuwa na uharaka kwanini asingekwenda kwa mwenyekiti kumshauri jambo ambalo ni rahisi kwake?
"pia, tumemsikia mzee wetu lowassa naye akisema eti serikali ipandishe mishahara ya wafanyakazi, yeye mwenyewe alikuwa ndani ya serikali miaka miwili tu iliyopita, kwanini hakushauri hilo huko nyuma mpaka sasa aje aeleze tena si katika vikao vya chama, bali kwa waandishi wa habari," alihoji ulega.
Ulega alisema wapo viongozi ndani ya chama ambao wamekuwa wakikiuka maadili na kufanya vile wanavyopenda wao bila ya kutazama athari za wanayoyasema kwa taifa.
Alisema viongozi wakuu serikalini hawamsaidii rais kikwete kwa kuwa wamekuwa wakijiweka pembeni na kushindwa kutetea mambo mbalimbali yanayokosolewa, ukiwemo mfumuko wa bei unaotajwa kuikumba nchi hivi sasa licha ya kuwa wanayo maelezo juu ya hilo.
Alieleza viongozi hao wakiwemo mawaziri, wamekuwa kimya hata pale wanapoona yapo mambo wanayoweza kuyatolea ufafanuzi kabla ya rais kikwete, lakini hawafanyi hivyo na kumuachia rais aeleze na kutetea kila jambo.
"linapotokea jambo hakuna anayesema lolote... Wanamwachia rais aseme na ikitokea wanazungumza basi wanasema ya hovyo," alisema.
Kwa mujibu wa ulega, ipo dhana iliyojengeka miongoni mwa watanzania kuwa urais ni lazima uende kwa watu wa upande fulani wa nchi, jambo ambalo si lazima kwa kuwa tanzania ni moja na kila mmoja ana haki ya kuongoza hasa anapokuwa na sifa zinazokubalika.
"tunafahamu kuwa upinzani umekuwa ukiongezeka kwa malengo fulani ya wahusika, hasa kutaka nafasi za kisiasa, lakini tunawaeleza wazi kuwa hawawezi kufanikiwa hayo wanayoyataka kwa kumharibia rais kikwete, na yeye ataendelea kuongoza hadi muda wake utakapokwisha," alisema.
Mwenyekiti huyo aliyekuwa akizungumza kwa kuwahamasisha vijana wa ccm kusimama kutetea mema ya chama, alisema baadhi ya watu wanashindwa kusimama na kueleza au kukemea madudu yanayodaiwa kwa kuwa wamekuwa wakipokea fedha kutoka kwa wasiopenda mafanikio ya serikali, lakini kwake hilo halipo.
Alisema viongozi hao wanataka kuifikisha nchi pabaya, ilhali wao wameshaitumikia kwa muda mrefu bila ya kubughudhiwa na wanafanya hivyo sasa ili ikiwezekana hata machafuko yatokee.
"nchi hii inaongozwa na ccm kutakapotokea lolote watakaopelekwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ni viongozi wake bila kujali nani ni nani, lazima tusimame tukemee, mimi nasema kwa kuwa sikula cha mtu, nipo huru nasema lolote," alisema.
Alimwomba mwenyekiti wa ccm rais kikwete kabla ya kufanya mabadiliko makubwa ndani ya chama, awatazame viongozi walioshindwa kuwajibika na kuwatosa kama kafara kwa wengine waliojificha na wasioitakia mema nchi.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, mbunge wa jimbo la bagamoyo, ambaye pia ni waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, dk. Shukuru kawambwa alisema vijana wameshindwa kukitetea chama mbele ya wanaopinga mafanikio kiliyoyaleta.
Dk. Kawambwa alisema licha ya mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu, bado vijana wanashindwa kutembea kifua mbele na kukitetea na kuacha wapinzani wakikishambulia kana kwamba hakuna jema lililotendeka.
Viongozi wa umoja huo kutoka mikoa mbalimbali walikuwa mingoni mwa waalikwa waliohudhuria mkutano huo, mbapo pia ulihudhuriwa na mjumbe wa baraza la uvccm taifa ridhwan kikwete, mbunge wa mchinga, said mtanda na wanafunzi kadhaa kutoka vyuo vikuu nchini.


c.r.a.p
 
Mwandishi uliosema hapo ni ya ukweli kabisa lazima hawa jamaa watakuwa na ajenda wameificha tumewashtukia muda mrefu na wataendelea kuchafuka maana kwa sasa wanajitahid kutaka kumchafua JK ila wapi wanabaki wao tu kuchafuka.Kikwete kula baba hao wote wana chuki na riziki yako unayoipata, inawauma sana ,inawachoma sana ila ndio hivyo baba wengi tunakupenda wachache kama hao ndio wanakuchukia.
 
ni jambo jema kama ndani ya CCM kuna watu walio na macho ya kuona nanma baadhi ya wastaafu kuanza kutoa kauli tata kwa ajili ya kujipanga kwa mbio za urais 2015.
lowasa na sumaye wana ajenda za siri
suala la sekretarieti kupwaya lipo wazi kabisa.
fumua wote hao akianza mzee Makamba ambae kiti cha ukatibu wa chama kimezidi mbali busara zake
 
Hamna kitu hapo, kwanza vijana wenyewe wa pwani ndo kabisaaa hawawatishi watu. Tangu lini mswahili akaogopa mbu?
 
Dk. Kawambwa alisema licha ya mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu, bado vijana wanashindwa kutembea kifuambele na kukitetea na kuacha wapinzani wakikishambulia kana kwamba hakuna jema lililotendeka.
Viongozi wa umoja huo kutoka mikoa mbalimbali walikuwa mingoni mwa waalikwa waliohudhuria mkutano huo, mbapo pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Ridhwan Kikwete, mbunge wa Mchinga, Said Mtanda na wanafunzi kadhaa kutoka vyuo vikuu nchini.

Nitarudi ngoja ninywe chai kwanza. Maana unaweza jikuta unatapika bure
 
Hakuna chochote hapo. JK anawajibu kina Sumaye kwa kutumia mgongo wa vijana. huo usanii umeshazoeleka hapa Tanzania
 
hawa CCM wanatafunana wenyewe kwa wenyewe, hawana jipya hiyo dhambi ya Ufisadi inawatafuna kama cancer, embu angalia UVCCM imejaa watoto wa matajiri na Vigogo huko mlalahoi hapewi nafasi ng'o! Bravo Lowasa and sumaye Divide them (CCM) and we(CDM) rule them.
 
Kashaga kaongea hivyo bila woga kwa sababu eti 'hajala' cha mtu! Akila cha mtu atasema?
 
Hakuna chochote hapo. JK anawajibu kina Sumaye kwa kutumia mgongo wa vijana. huo usanii umeshazoeleka hapa Tanzania

ina maana JK anaviogopa hivi vikongwe vya kisiasa kiasi hicho anashindwa kuwa attack directly. huyo JK si alikuwa mwanajeshi kwa nini asitumie ukakamavu aliofundishwa jeshini kuwa attack hawa "Bully Boys"
 
Inahitajikaakili ya ziada kwa Umoja wa vijana waccm kusimama na kuyasifia mazuri yaliyofanywa na CCM,Kama yngekuwepo Watnzania tusingefika hapa tulipo ,maisha yasingekuwa hivi,mfumuko wabei usingefika hapa.yote haya yanafanywa na wafanyabiashara marafiki,wanachama wa CCM,Ufisadi unafanywa na Watu wa karibu wa CCM Kama si wanaCCM,Wamiliki wakubwa waviwanda vya sukari ni wafadhiri wa CCM Kama si wamiliki wa mashamba makubwa ya miwa kina mkapa,nani anajeuri ya kushusha bei ya sukari wanakimbilia kuondoa ushuru sukari toka nje mbona hawaimuru wazalishaji wa ndani wa sukari kuuzwa bei ya chini?Mafisadi wanaporomosha majumba makubwa Dar.Wahindi ndiowamiliki wa vuwanda vikubwa ndio wachangiaji wakubwa bajeti ya CCM,Hamna jeuri ya kuwaamuru kushusha bei hayo yote yanafanyika UVCCM WAPO SUMAE YUPO LOWASA YUPO .WASIDANGANYEHAWANA JIPYA .SI UMOJA WA VCCM WALA VIONGOZI WASTAAFU TOKA CCM Wanaweza kusema chochote .hakuna wa kutoa sauti ya mwisho ndani ya CCM wote wamekuwa kambale.
 
CCM maumivu yakizidi muone daktari, maana kwa babu mmeanda bado hamjui mnaumwa nini? Kumbe hamjui kila mtu anahatarisha amani si Chadema pekeyao. Usanii ukizidi mambo watu wananyamaza,mawzairi wamshuri vipi wakati JK anawaombua. Mwanasheria kamshauri alipe dowans, kombaini kamshauri asifanye mabandiliko ya katiba yeye anaunda tume, wakati wenzake walisoma ilani hawakuona swala la katiba. Watashikana uchawi mpaka kieleweke. Na jinsi mlivyopaniki kwa yanayotokea urabini lazima mtatoana roho wenyewe kwa wenyewe. Chadema kaza uzi mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom