Mgodi wa Tanzanite One Mererani wafukia watu

mlemwa

Member
Jan 8, 2016
8
0
Taarifa za awali zisizo rasmi kutoka Mererani mgodi wa Tanzanite one ambao punde ulikuwa na mgogoro na viongozi wa chama cha wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla, ni kwamba kumetokea ajali ya mgodi kuanguka na kufukia watu katika moja ya shaft zake inayoitwa JW.

Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya waliokuwa chini ila kulingana na Maelezo ya mhanga mmoja alobahatika kutoka ni kwamba wako watu zaidi ya 13.

Tuwaombee wahanga MUNGU awanusuru na zaidi sana tutapeana taarifa kamili.
 
sisi tulishajua haya yatatokea tu huyu husen gonga anatamaa sana wanalipua zile nguzo unategemea nini? mtanzania hakuna anachoweza kuendeleza anachojua ni kuharibu tu kama serikali itakaa kimya basi tutazika wengi kwenye huo mgodi soon
 
Huo mgodi wa jw unangema za kutosha mzungu alisimamisha usifanye kazi mpka miundombinu iwekwe sawa...wamekuja washwahili wanataka mawe 2 hawaangalii usalama wa wafanyakazi
 
hii ndio shida ya kuwapa waswahili mgodi mkubwa kama ule watawamaliza vijana wetu hasa wanyaturu wamejaa kweli pale
 
mkuu shida ni gharama kuendesha mgodi kunahitaji wataalam n geologist wenye uzoefu sasa pale hakuna ni kupiga tu nguzo shaft inasogezwa kwa nguvu za soda.....waliojaa pale sio wanyaturu ni kondoa moja
 
ni kweli mkuu husen gonga amejaza warangi wenzake atawamaliza ule mgodi ni bora magufuli awanyanganye hawa watu kwa sababu kuuendesha wameshindwa hata kulipa wafanyakazi ni taabu tupu sasa ivi watu wanamkumbuka mzungu
 
sisi tulishajua haya yatatokea tu huyu husen gonga anatamaa sana wanalipua zile nguzo unategemea nini? mtanzania hakuna anachoweza kuendeleza anachojua ni kuharibu tu kama serikali itakaa kimya basi tutazika wengi kwenye huo mgodi soon
wao wanajua unachimba tu kama shimo la muhogo hawajui kuna kuacha nguzo au hata kujengea nguzo na zenge inapobidi ilikuweka usalama , sasa wao na nguzo wamelipua ili tu wapate TANZANITE waongezee idadi ya MABILIONEA wa arusha haya sasa tuone
 
ni kweli mkuu husen gonga amejaza warangi wenzake atawamaliza ule mgodi ni bora magufuli awanyanganye hawa watu kwa sababu kuuendesha wameshindwa hata kulipa wafanyakazi ni taabu tupu sasa ivi watu wanamkumbuka mzungu
Wamezoea kuuza juice kuwekeza mgodi mkubwa hawawezi
 
Taarifa za awali zisizo rasmi kutoka Mererani mgodi wa Tanzanite one ambao punde ulikuwa na mgogoro na viongozi wa chama cha wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla, ni kwamba kumetokea ajali ya mgodi kuanguka na kufukia watu katika moja ya shaft zake inayoitwa JW.

Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya waliokuwa chini ila kulingana na Maelezo ya mhanga mmoja alobahatika kutoka ni kwamba wako watu zaidi ya 13.

Tuwaombee wahanga MUNGU awanusuru na zaidi sana tutapeana taarifa kamili.
kuna wakati wachimbaji waligoma wakidai mgodi si salama ... sasa imekuwaje tena
 
Back
Top Bottom