Mgodi wa almasi Mwadui hawajalipa kodi kwa miaka yote

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
The-main-entrance-to-De-Beers-Tanzania-Williamson-Diamonds-Ltd-at-Mwadui-in-Shinyanga.-LEONARD-MAGOMBA.jpg

The main entrance to the old De Beers Mwadui mine in Shinyanga, Tanzania, (now owned by Petra Diamonds Ltd)​

SERIKALI bado inaendelea kupoteza mapato makubwa kutokana na misamaha ya kodi inayotolewa kwa makampuni makubwa, hususan yale ya migodi, ambayo yanachuma madini na kudai kuwa yanapata hasara. Mgodi wa almasi wa Mwadui mkoani Shinyanga ambao ulianza kuchimbwa miaka mingi iliyopita chini ya umiliki wa Kampuni ya Williamson ni mojawapo ya migodi ambayo imejichotea madini bila kulipia kodi wala gawiwo kwa serikali.

Kwa miaka yote ya uchimbaji, wamiliki wa mgodi huo walikuwa wakidai kupata hasara, hivyo kutolipa kodi ya mapato hadi mwaka 1994 mgodi huo uliponunuliwa na Kampuni Petra ambayo nayo inauendesha hadi leo bila kulipia kodi.



800px-Williamson_Diamond_Mine%2C_Mwazui%2C_Tanzania_03.jpg


Chini ya umiliki wa Williamson, almasi iliyokuwa inachimbwa ilikuwa ikichambuliwa nchini Uingereza pasipo kuwepo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, kujua kiasi cha madini yaliyopatikana.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, taarifa za mapato ya mgodi huo zimeendelea kuwa siri kiasi kwamba hata ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kamati ya Bunge mwaka 2004, katika mazingira ya kushangaza haikuwahi kujadiliwa hadi leo.


Ili kuhakikisha serikali inayabana makampuni hayo ya migodi na simu, mwaka 2010, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria ya madini na sheria ya Mawasiliano.
Lengo likiwa ni kuhakikisha makampuni hayo yanajiorodhesha katika soko la mitaji ili taarifa za mapato yake kuhakikisha zinakuwa wazi na kuwawezesha wananchi kununua hisa. Hata hivyo, serikali imeendelea kuwa na kigugumizi cha kutengeneza kanuni za kuendesha utaratibu huo licha ya sheria kuagiza jambo hilo lifanyike ndani ya miaka mitatu tangu kutungwa kwa sheria hizo.


Hivi karibuni akijibu suala hilo bungeni, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alisema serikali inachukua hatua ili kuhakikisha utekelezaji wa sheria hiyo unafanikiwa.
Alisema kuwa wameunda vikosi kazi viwili, kimoja kikiwa ni kwa makampuni ya simu na kingine cha makampuni ya migodi ili kutengeneza kanuni ambazo zitahusisha Sheria ya Mawasiliano na Sheria ya Madini za mwaka 2010.


Alisema kwa sababu ni sheria mbili zinazosimamia sekta tofauti ndiyo maana wameunda vikosi kazi viwili tofauti ili kulitekeleza jambo hilo ambapo kwa makampuni ya simu kinaratibiwa na TCRA na kingine cha migodi kinaratibiwa na Wizara ya Nishati na Madini.
Alisema katika mwaka wa fedha 2013/14, kanuni hizo zitakuwa zimekamilika, hivyo kuwezesha Watanzania kupata umiliki kwenye kampuni za madini kupitia uuzaji wa hisa za umma.Mkuya alisema kuwa kanuni hizo zitawekewa kipengele cha adhabu kwa yale makampuni yatakayoshindwa kutimiza matakwa ambayo yamewekwa kwenye hizo taratibu.


Wakati serikali ikiendelea kuzembea, Tanzania Daima ilidokezwa kuwa taarifa ya uchunguzi kuhusu mgodi huo iliwasilishwa bungeni Juni 6, 2004, asubuhi kama hati za kuwasilishwa mezani.
Wakati huo, Spika wa Bunge akiwa Pius Msekwa, taarifa hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamad Rashid Mohamed (CUF).Lakini kwa fununu zilizopo ni kwamba vigogo wa Mwadui waliteka Bunge na kuhakikisha ripoti hiyo haijadiliwi, mpaka leo imekuwa ikipigwa danadana.


Akizungumza na gazeti hili, Hamad alisema kuwa ripoti hiyo ilikuwa inapigwa vita hata kabla ya kuwasilishwa bungeni na kwamba hata baada ya kuiwasilisha mezani alielezwa kuwa itapangiwa siku ya kuwasilishwa.
"Hadi tunamaliza Bunge, ripoti hiyo haikupangiwa nafasi ya kujadiliwa na wabunge," alisema. Hamadi alisema katika uchunguzi wao walijiegemeza kujua sababu za serikali kuuza asilimia 25 ya hisa zake kutoka asilimia 50, hivyo kumpa Williamson uhalali wa kumiliki hisa asilimia 75. "Hawa watu hawakuwahi kulipa kodi wala gawiwo kwa muda wote waliokaa nchini kwa madai kuwa wanapata hasara, sasa tulitaka kujua kwanini waendelee na uwekezaji wakati wanapata hasara," alihoji.


Alisema kuwa katika uchunguzi wao waligundua kuwa mgodi huo unaweza kufanyakazi miaka 100 ijayo, hivyo wakashangaa kusikia wamiliki wanadai kupata hasara.
Hamad aliongeza kuwa wamiliki hao katika hatua ya kushangaza walinunua mtambo wa kusafisha dhahabu nchini Australia badala ya mtambo wa kusafisha almasi. Alisema kuwa hata sehemu ya kuhifadhiwa dhahabu alikuwa haingii mtu yeyote kwa kisingizio kwamba zinafanya kazi mashine tu lakini wao walipoingia walibaini kuwa Wazungu hao wanaingia ila watendaji wa wizara wanazuiwa, hivyo hawajui kiasi cha almasi kinachochukuliwa.


"Wakati huo kituo cha kusafisha almasi cha Tansort kilikuwa nchini Uingereza kabla ya kuletwa hapa nchini baada ya mapendekezo ya kamati yetu.
Hivyo almasi ilikuwa inafikia mikononi mwao kisha ndipo inapelekwa Tansort," alisema. Aliongeza kuwa wakiwa nchini Uingereza, Tansort walishangazwa na hatua ya mgodi huo kutolipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara, wakisema kuwa hata jiwe moja la almasi hiyo lilitosha kulipa kodi hiyo.


Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) naye alilidokeza gazeti hili kuwa baada ya kuifuma ripoti hiyo, mwaka 2012/2013 wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati alizungumzia kwa kirefu namna mgodi huo usivyolipa kodi.
"Ripoti hiyo niliipata kwa bahati baada ya kutafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mpaka nilijaribu kumwomba kijana mmoja aliyekuwa mgeni katika maktaba ya Bunge Dodoma ambaye alinipatia. "Na nikaitumia kuihoji serikali kwa kina mwaka jana ila baada ya kuchangia Waziri Sospeter Muhongo aliomba kupata ripoti ile, nilipeleka ofisi zao za Dodoma na kumkabidhi naibu wake, Boniface Simbachawene, ambaye alielekeza nitoe nakala, wakahidi kushughulikia," alisema.


Kafulila alisema kuwa ripoti ile ilionesha kuwa almasi inayochambuliwa na Tansort ili kupanga madaraja ni asilimia 10 tu, na asilimia 90 inakadiriwa, hivyo kuwa mwanya wa hasara kwa kukadiria mapato kidogo.
"Kuna mapungufu mengi sana yaliripotiwa kwenye taarifa ile, yalitosha kabisa kutaifisha mgodi ule, bahati mbaya baada ya kuonesha ripoti ile bungeni iliibiwa katika mazingira ya utata hotelini kwangu," alisema.


Kafulila alisema kuwa wawekezaji hao wa Mwadui walikuwa pia nchini Lesotho, walikowekeza muda mfupi wakaona hawapati faida wakarudi kwao na kuhoji ni kwanini wamendelea kuwekeza Tanzania kama wanatangaza hasara."Juni 10, 2013 tukiwa bungeni waziri aliitisha bodi ya Kampuni ya Petra Diamond ambayo inamiliki Mwadui kuanzia mwaka 1994.
Kamati ya Nishati na Madini imekubaliana na waziri kwenda Mwadui hivi karibuni kuanza uchunguzi," alisema.


Naye Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), katika mkutano wa Bunge uliopita alionesha jinsi makampuni ya madini yanavyolipa kodi kidogo wakati wafanyakazi walioajiriwa katika makampuni hayo wanalipa kodi kubwa zaidi.
Alisema kati ya mwaka 1999 hadi 2004, makampuni ya madini yalilipa kodi sh sifuri kama kodi ya mapato wakati wafanyakazi wa makampuni hayo walilipa sh bilioni 51.82. Lissu aliongeza kuwa katika kipindi hicho cha mwaka 1999 hadi 2012, makampuni hayo yalilipa kodi ya mapato sh bilioni 467.98 na wafanyakazi walilipa kodi za sh bilioni 505.4. "Mwaka 2001 hadi 2012, makampuni ya madini yalipata mapato ya dola za Marekani bilioni 11.9 sawa na sh trilioni 19.635 na kipindi hicho yalilipa kodi sh trilioni 1.216 au asilimia sita ya mapato yao.

Hisani ya Tanzania Daima
 
Kwa miaka yote hii makampuni yanayochimba almas huko Mwadui/Shinyanga walao yangefanya ubinadamu tu kujenga majengo ya shule nchini walao kila mwaka shule mbili au tatu wangekuwa na cha kuoneysha kuliko walivyoliibia taifa mamilioni yote bila hata asante kwa kile wanachokichota toka ardhi yetu ya Tanzania.
 
Du nimeiona Sort House bana! nakumbuka miaka ya nyuma wakati nalinda na shotgun yangu bana! Afande Marwa, Ndoda, Chubwa, Mgundulwa n.k sijui bado wapo?
 
Du nimeiona Sort House bana! nakumbuka miaka ya nyuma wakati nalinda na shotgun yangu bana! Afande Marwa, Ndoda, Chubwa, Mgundulwa n.k sijui bado wapo?

Siku za nyuma niliwahi kupita hapa. Lakni cha kushangaza kama wanapata hasara miaka yote inakuwaje waendelee na mradi huo?
 
Siku za nyuma niliwahi kupita hapa. Lakni cha kushangaza kama wanapata hasara miaka yote inakuwaje waendelee na mradi huo?
Mgodi huo umekaa kivyake vyake sana. Hivi umewahi hata kuona wakitangaza nafasi za kazi? Hata wenzetu waliopo humo kama Mkurugenzi wa Utawala Balyoluguru na wenzake ni wanyonyaji tu na hata siku moja hawawezi kuijulisha serikali mbinu zinazotumiwa na wazungu hao kukombeleza almasi zote. Kuna wakati rafiki yangu aliwahi kuandika gazetini artile iliyokuwa ikionesha jinsi makaburu walivyokuwa wakitunyonya, kijana huyo alifukuzwa kazi kwa artile aliyoitoa gazeti la Mtanzania. Kwa wakati huo kijana alitufumbua macho kuwa MD wa Williamsons Diamond alikuwa akilipwa zaidi ya shilingi milioni 32 za Kitanzania. Wazungu walikasirika sana na wakaamrisha kijana huyo atimuliwe kazi. Kwa sasa inasemekana mshahara wa MD hapo MWadui ni zaidi ya shilingi milioni 50 kwa mwezi kando ya marupurupu mengine kama nyumba yenye swimming pool, wafanyakaza wa ndani zaidi ya 6, ulinzi, usafiri bure, mbwa bure, na mapochopocho mengine kibao. Hapo unadhani serikali itapata nini?
 
Siku za nyuma niliwahi kupita hapa. Lakni cha kushangaza kama wanapata hasara miaka yote inakuwaje waendelee na mradi huo?
nilibahatika kupita migodi yote nikifunga VSAT, nilianzia GGM, kikaenda Buzwagi, Bulyankulu, Turawaka na nikamaliza hapo Shy - Mwadui.

Niliyoyaona nikiwasimulia ni hatari, na mjue kwamba wale wanaokaa kando kando ya migodi hii si machizi kuvamia migodi kutaka kupora mali - sitaki kuwapandisha hasira ila Tunaibiwa mchana mweupe.
 
Watanzania tuamke, Kama hawataki kulipa kodi kwa kisingizio cha kujiendesha kwa hasara kwa nini wanaendelea na biashara hizo?.
 
Watanzania tuamke, Kama hawataki kulipa kodi kwa kisingizio cha kujiendesha kwa hasara kwa nini wanaendelea na biashara hizo?.
blanketi la ccm limetuziba, ishafika mchana ila sisi tunahisi bado ni usiku wa manane ndiyo tunalivuta nalo zaidi.
 
blanketi la ccm limetuziba, ishafika mchana ila sisi tunahisi bado ni usiku wa manane ndiyo tunalivuta nalo zaidi.

Jua likishazidi, Blanketi litasababisha na joto na pale watanzania watakapotoka kufunua nyuso zao kupata hewa ndio watakojua kumbe kumekucha saa nyingi na wamechelewa kwenda kazini. Utaona watakavyolitupa kwa hasira tena kwa haraka bila kukawia.
 
Mmeanza kukichokonoa kibibi cha watu kimetulia na crown yake huko wenst.. nanihii saa hizi,wachokozi nyiee!
 
Mgodi huo umekaa kivyake vyake sana. Hivi umewahi hata kuona wakitangaza nafasi za kazi? Hata wenzetu waliopo humo kama Mkurugenzi wa Utawala Balyoluguru na wenzake ni wanyonyaji tu na hata siku moja hawawezi kuijulisha serikali mbinu zinazotumiwa na wazungu hao kukombeleza almasi zote. Kuna wakati rafiki yangu aliwahi kuandika gazetini artile iliyokuwa ikionesha jinsi makaburu walivyokuwa wakitunyonya, kijana huyo alifukuzwa kazi kwa artile aliyoitoa gazeti la Mtanzania. Kwa wakati huo kijana alitufumbua macho kuwa MD wa Williamsons Diamond alikuwa akilipwa zaidi ya shilingi milioni 32 za Kitanzania. Wazungu walikasirika sana na wakaamrisha kijana huyo atimuliwe kazi. Kwa sasa inasemekana mshahara wa MD hapo MWadui ni zaidi ya shilingi milioni 50 kwa mwezi kando ya marupurupu mengine kama nyumba yenye swimming pool, wafanyakaza wa ndani zaidi ya 6, ulinzi, usafiri bure, mbwa bure, na mapochopocho mengine kibao. Hapo unadhani serikali itapata nini?

kama bado una chaneli za ndani uliza, huyo jamaa alipata matatizo ya moyo baada ya kutishiwa kufukuzwa kazi. What's painful ni walivyovunja majumba
 
Migodi yote inalipa kodi kidogo sana. Mchezo wa kuigiza juzi VP wa ABG Ndg Mwanyika kasaini mkataba wa kuwasidia Wachimbaji wadogo wakati ABG ndio wana funga virago baada ya madini kuisha wameanza na Kufunga mgodi wa Tulawaka, Buzwagi wafanyakazi wameshataarifiwa waanze kutafuta ajira sehemu nyingine. Inaingia akilini hawa watu wanamaliza uchimbaji ndio wanajitoa kwenye jamii na kupigwa picha na vyombo vya habari.Mh. waziri wa madini najua unapita humu una maoni gani kwa haya magumashi yanayoendelea na wachimbaji wakubwa?
 
Vijana wa lumumba huwezi kuwaona katika post hii. Wao busy na kuiponda chadema tu wakati nchi inazidi kutafunwa na wachache.
 
Inauma sana kuishi serukamba country. Halafu wanaongeza kodi kwenye vitu vinavyomgusa mwananchi moja ili kumkandamiza zaidi huku resources zikichuliwa kama hazina mwenyewe. Mamlaka zimeng'ang'ania kudeal na ugandamizaji wa raia badala ya kudeal na mambo makubwa Kama haya. Hivi TIS wamebakiza kazi gani ya kujivunia? Maskini Tanzania yangu.:A S 20::A S 20:::A S 20::A S 20:
 
Zamani usalama wa taifa walikuwepo hadi bar wakijua hadi idadi ya bia ulizokunywa, mabenki ndo usiguse. Inakuwaje miradi mikubwa yenye masilahi ya taifa inakosa uangalizi wa kiusalama ku reveal mbinu chafu za wawekezaji uchuro? Ndo maana sishangai kuona Face book I wanapanda juu ya maeneo nyeti ya ikulu ambayo hata pccm hawajawahi yagusa. Ni sawa na kumpisha mgeni kulala master bedroom ukiwanumeacha rockers wazi. Ni nchi ya kipekee ambapo mgeni Ana nguvu na thamani kuliko wenyeji, na kujiamulia kufanya kwa kadri wanavyojisikia. By the way, kulipa kodi ni huruma tu, tangu lini wenye mtindio wa ubongo wakapewa hela ya maendeleo yao? Labda ya kununulia pop corn:frusty::frusty:
 
Nimezaliwa Mwadui..nimekulia mle na kusoma Mwadui 'B' Primary School...baadae nikafaulu 'nje' TABORA SCHOOL....Baba yangu ni miongoni mwa mwaliofungua kesi dhidi ya Mwadui mwaka 1994 ktk Mahakama kuu kanda ya Tabora kudai malipo baada ya kuachishwa kazi mara tu De Beers walipouchukua mgodi,wakiwa na kina Mazengo,hakuwah kupata haki yake mpaka amekufa..ameanzisha mgodi na Wiliamson,alijiunga 1958....naumia sana,nilikuwa mdogo,lakn baba alidhulumiwa
 
mbona majamaa wa tra wanadai sana kodi kwa wanyonge ata kama wamepata hasara. mkumbuke nyerere alisema serikali dhaifu uwa aichukui kodi kwa wakubwa inaishia kukimbizana na wafanyabiashara wadogo tu
 
yawezekana bado de beers wanakula tax holiday, iyo ndo ccm wanajifanya kama hawapaoni uko

umeona pia kempisk hotel? kala tax holiday kaondoka na kwa sasa panaitwa hyatt hotel nao watakula tax holiday nao wataondoka, yan wiz wa wazi, ccm km hawaoni vile
 
Back
Top Bottom