Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,547
- 139,883
Naona una kazi ya ziada Mzito Kabwela
mjirekebishe bana,mnajidharirisha hata kama hutuwajui,sio wote kuna wengine wanawajua
Naona una kazi ya ziada Mzito Kabwela
Mtanzania siku hizi kidogo wameshika adabu baada ya kitanzi cha siku 90
mgeja ni nani katika nchi hii?akawaonye akina vick kamata
CHADEMA rafiki yao shetani. Wote wamelaaniwa
Hivi huyu Mgeja ni Mgeja yupi? Namkumbuka Mgeja mmoja mweupe mfupi alikuwa mwizi mkubwa wa mifukoni hapo Shinyanga. Alisumbua sana, sana. Siku moja niliulizia mtu mmoja akaniambia ni huohuyo aliyekuwa pickpocket wa kutisha Shinyanga. Hivi CCM ina mamatizo gani? Haya angalia Mabina, Mgeja na hata huyu Meya wao Matata, mbona wana sifa moja, ya.....MENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa vurugu kilizozifanya kwa kuwavamia wafuasi wa CCM na kuwakata mapanga na kuwasabishia baadhi yao ulemavu wa kudumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa baada ya kuwatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando,Mgeja aliitaka serikali ichukue hatua kali kwa wahusika.
Mgeja alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Mbunge wa Maswa Mashariki, Joseph Kasulumbayi ni cha kinyama.
Wanachama wa CCM waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuhamishiwa hapo kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na hali zao kuwa mbaya ni pamoja na Charles Mhiga ambaye ni dereva wa gari la CCM ambaye alikatwa mapanga kichwani na kushonwa nyuzi 12.
Mwingine ni Alphone Kimaro na Sebastian Masonga ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Kata ya Majengo ambaye alipigwa nondo na kuvunjwa mkono wa kushoto.
Mgeja alisema vurugu zinazofanywa na viongozi na wanachama wa Chama hicho zimelenga kuifanya nchi isitawalike na wananchi kuishi kwa hofu.
Alisema wakati umefika kwa Serikali na Jeshi la Polisi kuchukua hatua madhubuti kukomesha vitendo vya vurugu vinavyofanywa na viongozi na wafuasi wa Chadema.
CHADEMA wamekuwa wakitafuta uongozi kwa njia ya mkato kwa kufanya vurugu .wanapaswa kushindanisha hoja na wananchi ndiyo waamuzi.
Huwezi kutumia nguvu pamoja na mapanga kusaka uongozi katika hili hatua kali zinapaswa kuchukuliwa kwa wahusika, alisema Mgeja.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania, Februari 7, 2014.
Mwendo huu wa CHADEMA unaoshabikia vurugu kila pahala penye uchaguzi mdogo, ni dalili tosha chama hiki kinafika ukingoni!!!!
mgeja ni nani katika nchi hii?akawaonye akina vick kamata
jitu moja linaingia na id kumi. Wakiwa wanne ujue ni id 40. (tazama uandishi wa simiyu yetu, ifweero, tume ya katiba, utaifakwanza,) (kisha tazama uandishi wa chamviga, zemarcopolo, msalani) kisha tazama uandishi wa tandale one ,@ mafilili, katibu mwenezi) wakiingia badala ya kujenga hoja wao huishia kuporomosha matusi kwa wana cdm na viongozi wao. Mwishowe wanakula ban na mods wanaunganisha id zao. Wewe utaona hawadumu kumbe id zimeunganishwa
Ona aibu mkuu, unafurahishwa na uchafu huu unaofanywa na CHADEMA.
kawaida ya ccm wakiguswa wanalalamika sana! Ni hawahawa ambao waliwakatakata mapanga wabunge wa mwanza kupitia Chadema, na hatukuwasikia hawa kina mgeta mlamba miguu ya fisadi lowasa, ccm kwa mauaji ndo wanaongoza na kujeruhi watu pia!Mgeja ameongea maneno ya busara sana, hawa CHADEMA wanataka kuigeuza Tanzania kuwa uwanja wa vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Ona aibu mkuu, unafurahishwa na uchafu huu unaofanywa na CHADEMA.[/QUOTE
ccm mnatia aibu, mbona Wabunge na wafuasi wa Chadema wamepigwa na hata wengine kuuwa lakini polisi wamekuwa vipofu. Tendeni haki kwa wote isiwe kwa sababu.
ukishikwa shikamana, ccm ndiyo wanzirishi wa fujo zote hizoMtiririko wa fujo katika chaguzi ndogo za madiwani; walianzia Kahama, Njombe, Iringa, Arusha Mjini. CHADEMA ni janga la taifa