MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,200
MENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa vurugu kilizozifanya kwa kuwavamia wafuasi wa CCM na kuwakata mapanga na kuwasabishia baadhi yao ulemavu wa kudumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa baada ya kuwatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando,Mgeja aliitaka serikali ichukue hatua kali kwa wahusika.
Mgeja alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Mbunge wa Maswa Mashariki, Joseph Kasulumbayi ni cha kinyama.
Wanachama wa CCM waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuhamishiwa hapo kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na hali zao kuwa mbaya ni pamoja na Charles Mhiga ambaye ni dereva wa gari la CCM ambaye alikatwa mapanga kichwani na kushonwa nyuzi 12.
Mwingine ni Alphone Kimaro na Sebastian Masonga ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Kata ya Majengo ambaye alipigwa nondo na kuvunjwa mkono wa kushoto.
Mgeja alisema vurugu zinazofanywa na viongozi na wanachama wa Chama hicho zimelenga kuifanya nchi isitawalike na wananchi kuishi kwa hofu.
Alisema wakati umefika kwa Serikali na Jeshi la Polisi kuchukua hatua madhubuti kukomesha vitendo vya vurugu vinavyofanywa na viongozi na wafuasi wa Chadema.
"CHADEMA wamekuwa wakitafuta uongozi kwa njia ya mkato kwa kufanya vurugu….wanapaswa kushindanisha hoja na wananchi ndiyo waamuzi.
"Huwezi kutumia nguvu pamoja na mapanga kusaka uongozi…katika hili hatua kali zinapaswa kuchukuliwa kwa wahusika," alisema Mgeja.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania, Februari 7, 2014.
Mwendo huu wa CHADEMA unaoshabikia vurugu kila pahala penye uchaguzi mdogo, ni dalili tosha chama hiki kinafika ukingoni!!!!