Mgao wa Umeme uko Tanzania pekee kwa ukanda huu wa EA

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,507
Kwa kifupi Tanzania ndio pekee ina mgao wa umeme kwa sasa.Kenya walikuwa nao kipindi cha ukame ila baada ya masika mgao ukaisha na hadi leo hawana tena mgao. Uganda hakuna kitu kama hicho, Zambia nao walikuwa nao ila masika ilijaza bwawa lao na kwa sasa hawana mgao.

Tanzania haijalishi kuna Masika,Kiangazi au Elinino, migao iko pale pale, na sisi wajinga tuko Busy na kuwalamba watawala miguuu.

Ukipita mto pangani kipindi hiki unafurika maji balaaa, ila unaabiwa hayaingii bwawa la nyumba ya Mungu, sasa maji yale yanapotelea wapi?

Huu uhuni usingewezekana wakati wa JPM, unawezekanatu kipindi hiki.
 
Kwa kifupi Tanzania ndio pekee ina mgao wa umeme kwa sasa.Kenya walikuwa nao kipindi cha ukame ila baada ya masika mgao ukaisha na hadi leo hawana tena mgao.
Uganda hakuna kitu kama hicho, Zambia nao walikuwa nao ila masika ilijaza bwawa lao na kwa sasa hawana mgao.

Na Tanzania ni pekee EA ambako watawala ni wale wale tokea uhuru.

Zingatia CCM = TANU
 
Siyo hizo tu, ukweli ni kuwa katika nchi zote za Afrika nilizotembelea miezi ya karibuni, hakuna nchi yenye huduma hovyo kabisa ya umeme kama Tanzania.

Tatizo letu siyo upungufu wa mvua, bali ni uoungufu wa maarifa, upungufu wa akili, upungufu wa mipango na upungufu wa uwezo wa kuyaona mambo kabla hayajatokea kwa viongozi na watawala wa nchi hii.

Tanzania hata kama mvua zingekuwa zinanyesha mwaka mzima, kwa aina ya viongozi na watunga sera na wasimamizi tunaokuwa nao, tatizo la umeme na mengine mengi, hayawezi kwisha.

Kwisha kwa tatizo la umeme na mengine mengi kwa Tanzania, ni mpaka siku ambayo CCM itaisha. Maadam CCM ipo, maadam CCM ni ilele, mipango yake ni ilele, uwezo wa watu wake ni ule ule, matatizo yake yataendelea kuwa ni yale yale. Kama tunavyoivumilia CCM, yatubidi pia tuendelee kuyavumilia matatizo inayoyasababisha.
 
Na Tanzania ni pekee EA ambako watawala ni wale wale tokea uhuru.

Zingatia CCM = TANU
Hii inafikirisha sana. Kuongozwa na fikra mgando kwa zaidi ya miaka 60 ndiyo madhara yake. Kwa vile wameshahodhi dola hivyo hawana sababu ya kuumiza vichwa kutuletea maendeleo sababu hawana hofu ya kuondolewa madarakani.
Chama chochote kinapokuwa madarakani kwa ridhaa ya wapiga kura kinajitahidi kuwatumikia wananchi kwa vile kinajua kuwa kinyume cha hivyo kinaondolewa madarakani kwa njia hiyo hiyo iliyokiingiza madarakani.
Hapa Tanzania ni tofauti CCM imeshakuwa chama dola yaani kiko madarakani kwa nguvu ya dola na dola hiyo iko mfukoni mwa CCM ikimaanisha hakiwezi kuondolewa madarakani kwa vikaratasi vinavyotumbukizwa kwenye sanduku la kura. Wamesikika mara nyingi viongozi wa CCM wakitamba kuwa hawawezi kuondolewa kwa karatasi, na wengine wakaenda mbali zaidi kuwa hata goli la mkono wakimaanisha ikibidi kwa wizi wa kura. Na haya siyo maneno matupu kwani tumeshuhudia kilichotokea 2019-2020 jinsi mabavu ya dola yalivyotumika,polisi wenye waliovaa sare wakibeba mabegi yenye kura za wizi.
Tutaendelea kurudishwa nyuma na CCM kwani hatuna uwezo wa kuwaondoa kwa njia ile waliyoingilia yaani mabavu ya dola. Ila wajue ndoto yao hii ya kutaka kutawala milele kwa mabavu ya vyombo vya dola inatuandalia 'Hamas' hapa nchi, kama siyo kizazi hiki basi kijacho.
 
Kwa kifupi Tanzania ndio pekee ina mgao wa umeme kwa sasa.Kenya walikuwa nao kipindi cha ukame ila baada ya masika mgao ukaisha na hadi leo hawana tena mgao. Uganda hakuna kitu kama hicho, Zambia nao walikuwa nao ila masika ilijaza bwawa lao na kwa sasa hawana mgao.

Tanzania haijalishi kuna Masika,Kiangazi au Elinino, migao iko pale pale, na sisi wajinga tuko Busy na kuwalamba watawala miguuu.

Ukipita mto pangani kipindi hiki unafurika maji balaaa, ila unaabiwa hayaingii bwawa la nyumba ya Mungu, sasa maji yale yanapotelea wapi?

Huu uhuni usingewezekana wakati wa JPM, unawezekanatu kipindi hiki.
Mtanikumbuka ni heri nikawe raisi wa malaika!
 
Kwani viongozi wa Tanzania wanafanana na wa nchi nyingine za EA?
 
Hii inafikirisha sana. Kuongozwa na fikra mgando kwa zaidi ya miaka 60 ndiyo madhara yake. Kwa vile wameshahodhi dola hivyo hawana sababu ya kuumiza vichwa kutuletea maendeleo sababu hawana hofu ya kuondolewa madarakani.
Chama chochote kinapokuwa madarakani kwa ridhaa ya wapiga kura kinajitahidi kuwatumikia wananchi kwa vile kinajua kuwa kinyume cha hivyo kinaondolewa madarakani kwa njia hiyo hiyo iliyokiingiza madarakani.
Hapa Tanzania ni tofauti CCM imeshakuwa chama dola yaani kiko madarakani kwa nguvu ya dola na dola hiyo iko mfukoni mwa CCM ikimaanisha hakiwezi kuondolewa madarakani kwa vikaratasi vinavyotumbukizwa kwenye sanduku la kura. Wamesikika mara nyingi viongozi wa CCM wakitamba kuwa hawawezi kuondolewa kwa karatasi, na wengine wakaenda mbali zaidi kuwa hata goli la mkono wakimaanisha ikibidi kwa wizi wa kura. Na haya siyo maneno matupu kwani tumeshuhudia kilichotokea 2019-2020 jinsi mabavu ya dola yalivyotumika,polisi wenye waliovaa sare wakibeba mabegi yenye kura za wizi.
Tutaendelea kurudishwa nyuma na CCM kwani hatuna uwezo wa kuwaondoa kwa njia ile waliyoingilia yaani mabavu ya dola. Ila wajue ndoto yao hii ya kutaka kutawala milele kwa mabavu ya vyombo vya dola inatuandalia 'Hamas' hapa nchi, kama siyo kizazi hiki basi kijacho.

bIla kusahau na kuganda kwetu. Hatuoni umuhimu wa kuwaunga mkono wenzetu wenye malengo sawa. Angalia:

1. Wakulima wa kiteto
2. Wamasai loliondo
3. Mwabukusi na uwakili wake
4. Fatma na uwakili wake
5. Sauti ya Watanzania na agenda zao
6. Ndugai na sekeseke lake
7. Polepole, Bashiru na masekeseke yao
8. Nk

bIla kuwa na sauti ya kutuunganisha, bado sana!
 
Mgawo wa umeme wa tanzania

Uko kibiashara zaidi....dili yaani

Ova
 
Huku Rwanda hakuna mambo hayo,umeme ukikatika hauchukui dakika mbili bila kurudi.Ccm oyeeee bado na mtasema!!!!!
 
Pole ndugu yangu kwa kutambua hivyoo leo tokea tupate uhuru tanzania ni nchi ambayo kutatua chochote cha maendeleo ni ngumu kwao hadi washirikishe wazungu au waarabu waje watatue. Yaani kujituma kwao ni ngumu . Kwa hiyo Karibu TanzaniA karibu nchi yenye shida ya utatuzi kimaendeleo . 😎😎
 
Tanzania ndio nchi ambayo kama ingepata kaburu hakika ingekuwa na maendeleo kama ya South Africa. Ubaya wa bongo wawekezaji ni wageni vibarua ni wenyeji, mgeni anaenda kujenga nyumbani sio ugenini

Pamoja na ujinga na wizi unaofanywa na ccm juu ya Tanzania still bado ina survive. Ukitembelea nchi za kusini mwa Africa ndio utajua Tanzania ni moja ya nchi ambayo ina strategic advantage nyingi kuliko nchi zingine

South Africa nao mgao upo kama bongo tuu. Afrika yote ni moja utofauti ni jiografia tuu
 
Umeme unakatika kila siku na hauna muda maalum...alafu Yule sijui injinia wao anasema mgao umepungua makali...
Huyu jamaa ni aibu....aliingia na maneno tele..kiko wapi sasa..bora akae kimya aendelee kula mshahara na marupurupu tu ..uzuri tuna Rais ambae hatumbui wala nini...
 
Huu mgao ni huku Tanganyika tu wale wala urojo hauwagusi,na wala hawailipi TANESCO miezi michache iliyopita wafutiwa deni la zaidi ya bilioni 60 wakati sisi tunakamuliwa.
 
F_tkdZCWcAIZyzI.jpeg
 
Hii inafikirisha sana. Kuongozwa na fikra mgando kwa zaidi ya miaka 60 ndiyo madhara yake. Kwa vile wameshahodhi dola hivyo hawana sababu ya kuumiza vichwa kutuletea maendeleo sababu hawana hofu ya kuondolewa madarakani.
Chama chochote kinapokuwa madarakani kwa ridhaa ya wapiga kura kinajitahidi kuwatumikia wananchi kwa vile kinajua kuwa kinyume cha hivyo kinaondolewa madarakani kwa njia hiyo hiyo iliyokiingiza madarakani.
Hapa Tanzania ni tofauti CCM imeshakuwa chama dola yaani kiko madarakani kwa nguvu ya dola na dola hiyo iko mfukoni mwa CCM ikimaanisha hakiwezi kuondolewa madarakani kwa vikaratasi vinavyotumbukizwa kwenye sanduku la kura. Wamesikika mara nyingi viongozi wa CCM wakitamba kuwa hawawezi kuondolewa kwa karatasi, na wengine wakaenda mbali zaidi kuwa hata goli la mkono wakimaanisha ikibidi kwa wizi wa kura. Na haya siyo maneno matupu kwani tumeshuhudia kilichotokea 2019-2020 jinsi mabavu ya dola yalivyotumika,polisi wenye waliovaa sare wakibeba mabegi yenye kura za wizi.
Tutaendelea kurudishwa nyuma na CCM kwani hatuna uwezo wa kuwaondoa kwa njia ile waliyoingilia yaani mabavu ya dola. Ila wajue ndoto yao hii ya kutaka kutawala milele kwa mabavu ya vyombo vya dola inatuandalia 'Hamas' hapa nchi, kama siyo kizazi hiki basi kijacho.
KANUNI KUU inayosimama duniani kote kuhusu serikali ni kwamba: viongozi wa serikali hawawezi kusikiliza na kutoa huduma stahiki kwa wananchi kama hakuna TISHIO LA KUONDOLEWA MADARAKANI na hao wananchi, period. US na Ulaya siku zote wananchi wanapambana na serikali zao kupitia mabunge, mahakama, chaguzi, civil action (migomo, maandamano, mikutano, n.k.).

Bila tishio hilo, hawawezi hata kujali wala kuheshimu hazina ya taifa. (Eti umeme usikatike, mkiwa kama nani? Kwani mtafanya nini zaidi ya kelele tu?).

Wagiriki wa kale kufikia hatua ya kuamua kuutaka utawala wa kidemokrasia waliziona na kuzipitia adha kadhaa za viongozi wenye ukiritimba wa madaraka. Huku sisi tunadai: hayo ni mambo ya wamagharibi, hayatuhusu Waafrika - huku tumeiga mifumo yote ya utawala toka kwao!

Anayetarajia serikali iwe ya “kizalendo” na kutenda mema hivi hivi tu ni mgonjwa wa akili.
 
Back
Top Bottom