Mgao wa umeme: South Africa walifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgao wa umeme: South Africa walifanyaje?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Invisible, Jul 24, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kuna tunachoweza (walau) kujifunza kutokana na paper hii kwa mazingira ya sasa?
  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Unajua kama taifa kuna kitu tunakikosa. Na inabidi wanaharakati wetu bila kuzingatia vyama, katika kila unit wachukue wawakilishi wakae chini tuweke vipaumbele kama taifa. Kuwe kuna mambo ambayo kitaifa itakuwa ni marufuku kutofauti, kwani hayajakaa kivyama bali kitaifa.

  Wala isiwe ni furaha kwetu eti JK kashindwa kumaliza tatizo la umeme nasi CHADEMA au CUF tushangilie na kudhani kupitia hilo ndio tupate dhamana y kuingia Ikulu.

  Tanzania yetu wasomi mbona wapo na haya yanaweza kufanyiwa kazi? ebu tubadilike jamani tuache ushabiki wa kivyama as if tunashabikia timu za mipira. Masuala ya kitaifa inabidi yasiingizwe katika siasa. Ni aibu kama taifa eti tunaacha kukomalia vipaumbele vya taifa ambavyo kila mtu bila kujali vyama vyetu kila mtu anatakiwa kuvilinda kwa nguvu zote.

  Na tuwe wakweli tunapochangia, tatizo la umeme limeoneka kama vile chanzo ni JK, kitu ambacho si sahihi, matatizo yalikuwepo tena makubwa even before sema media zilinyamanzia, mimi kwetu Kigoma umeme ilikuwa ni tatizo kubwa sana toka uhuru na limekuwa solved kipindi cha JK,barabara toka uhuru kigoma ilikuwa haijaunganishwa na mikoa mingine kwa lami, kiasi kwamba kutoka Kigoma tulitumia siku3 kufika Dar very soon tutatumia siku1, sasa hivi Kigoma-Bujumbura ni chini ya masaa 4.

  Kuna jamaa mmoja yeye alibahatika kufanyiwa utafiti na mtaalamu wake kuhusu uchumi wake na mtaalam akamuuliza mipango yake na jamaa akasema anaplan ya kuwakaribisha ndugu zake kuja kuishi naye, na mtaalam akamshauri kuwa jitahidi kuanzia sasa uchumi wako kila mwaka ukue kwa 10% lakini jamaa hakufanya hivyo hali ya kuwa anaendelea kuwashawishi ndugu zake kuja kukaa kwake, na baada ya miaka kadhaa huyo jamaa akawa ameondoka na mji kamkabidhi mdogo wake ambaye hakujua plan za kaka yake na mara wale ndugu zake wakawa wamekuja kwa wingi na hali ikawa mbaya sana. Swali ktk mji huo nani anapaswa kuonekana chanzo cha tatizo kati ya kaka na huyo dogo?
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  sisi TANESCO Wanasema SOLAR ni competitor, hivyo hawatoi ushauri kwa wananchi kutumia
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Na waraka wako mreefu huu, umesahau KJ alikuwa waziri wa mambo ya nje...

  Umesahau kugusia mikataba iliyosign niwa kipindi hicho mpaka sasa. Hujagusia mikakati yake ya kushugulikia huo umeme unakimbilia kumsafisha na kusifia jitihada zake kigoma.

  Ukitaka kuandika kwa kirefu hivi gusia kila kitu mpaka hotuba yake ya juzi na ile most popular quote of the century "Mimi sio Mawingu ninyeshe mvua mtera...mimi sio Mungu...laumuni ukame"
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Natofautiana nawe Mr Mark, kama watanzania tunachopigia kelele si Kikwete au rais mwingine yeyote Tanzania afanye kila kitu. Kelele zetu ni serekali yetu ijenge mazingira yatakayotoa nafasi ya mawazo mbadala na hata tafiti kufanyiwa kazi, na hapa ndio lilipo tatizo sasa kwa nini tusiilaumu serekali wakati haitaki ushauri wala nini ila ni ilani tuuuuu.

  Inastahili kulaumiwa kwa sababu inatulazimisha kuamini kuwa ina uwezo wa kufanya kila kitu, hebu jaribu kukumbuka ni tafiti ngapi za kitaalamu zimekuwa implemented na hii si kwa sababu za kukosa pesa bali ni kukosa vipaumbele hatimaye zote zinaishia kwenye makabati. Nikupe mfano wa karibu, upande wa upinzani ulijaribu kushauri njia mpadala kwa kushuhughulikia tatizo la umeme kilichotokea Waziri Mkuu bila hata kwanza kutafuta ushauri kwa wataalam alijibu hapo hapo hapana.

  Ni lazima kwanza iwepo nafasi ya mawazo na ushauri kupokelewa ndipo unayoyazungumza yatawezekana la sivyo tutaendelea kuilaumu serekali katika failure zote zinazotokea.

  Wewe unafikiri Tanesco hawana short/long term plan juu ya maendeleo ya umeme, mbona hawapewi nafasi kueleza mawazo yao kitaalam?. Ukiwauliza watakwambia waliyaona haya mapema na walikuwa na ushauri kwa serekali mapema lakini nani wa kuwasikiliza?
   
 6. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 701
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  ya nin malumbano, yanini, hakuna umeme ni hakuna, watu leo wanalalamika ndio hao hao waliwachagua hao MaJK miaka ya nyuma.
  soma iyo waraka ya sa uone kama sisi nasi tunaweza kuiga mfano huo??

  Ngeleja soma apa
  yajengwe mabwawa madogomadogo kabla ya power plants
  kwa kuwa maji huwa mengi sana wakati wa masika hata kuleta mafuriko yenye hasara kwenye baadhi ya maeneo, ivi haiwezekani kujenga mabwawa mengine madogo madogo kabla ya mtera/nyumba ya mungu/kidatu ili kutunza maji hayo pia kwa ajili ya kucontrol mafuriko? wataalamu saidien hii ni idea tu.
  Maji yaliyotumika yatumike tena.
  Kwa kuwa issue ni maji kujaa kwenye dam, jee haiwezekani maji yaliyotumika kuzungusha ili turbine kufanyiwa uchakachuaji yarudi tena kwenye bwawa then yatumike tena na tena na tena? wataalam mpo??
   
 7. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wee Robot, Kikwete alisema kwenye kama kuna Mtu anaweza kushauri au kuwa na maarifa mengine basi anakukaribisha Magogoni. Robot nafikiri nenda Magogogni ukamuone yule Vasco Da Gama kabla hajaenda kwenye space
   
 8. koo

  koo JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usimshauri mwenzio kupoteza muda labda kama ana njaa akale ubwabwa, saws lakini kutoa ushauri kwa mtu asiye jua anajukumu gani nikupoteza muda aliwahi kusema serikali isilaumiwe akimaanisha siyo jukumu lao hvyo wasipewe lawama.

  Sasa unampaje ushauri mtu ambaye hawajibiki na tatizo husika; zaidi robot ataonekana analichukulia tatizo kisisasa kwani wote waliojaribu kushauri walionekana wanatafuta mtaji wa kisisasa kwa tatizo la umeme mtu anadiliki kusema yeye sio wingu unategemea anakipya anakiwaza kweri nakusihi ujipange kuukabiri mgao wa masaa 24 unaoanza leo huku ukijutia kumnyima slaa kura kama ulifanya hivyo.
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mgosi na hata gazeti la raia mwema la wiki iliyopita iliweka taarifa ya hali halisi ya umeme na tanesco na hiyo ripoti ni ya 2009 na walieleza uwezekano wa hali hii tuliyonayo sasa lakini hakuna aliewasikiliza hii ndio serekali yetu bwana !
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Pia kuna hili la "TOPE",

  Kuna kipindi iliwahi kuanzishwa harakati na baadhi ya wadau kuwa mitambo ya kwenye mabwawa yetu haijawahi kuchujwa tope toka imefungwa enzi za mwalimu na mingine enzi za Mzee rukhsa.

  Sina utalamu na eneo hili, lakini hiyo hoja ilikuwa na mashiko sana cha ajabu sijawahi kuiona ikizungumziwa tena iwe kama kwa juhudi husika kufanyika au tu kukanusha kuwa "hamna kitu kama hicho" kitaalamu.
   
Loading...