Mgao wa umeme Arusha umeanza

Mgao wa umeme Arusha umeanza

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,963
Reaction score
5,552
Hapo vipi,

Watu wa Arusha kwa ujumla wameifuta CHADEMA - Arusha wakaweka kijani kibichi ambayo ni ishara ya neema.

Ni takriban wiki sasa Arusha maeneo ya Sakina, Mianzini, Sanawari, Sekei, Kimandolu, Ngulelo n.k wanakata umeme alafu wanarudisha jioni hakuna taarifa yeyote.

Mwananchi ana haki yakupewa taarifa kwasababu kuna watu wanategemea umeme kuingiza kipato na TRA hawataki kujua kama umeme umekatika au lah.

TANESCO tunaomba kama mnakata umeme mtoe taarifa ili Wananchi wajipange namna ya kukabiliana na hali hiyo.
 
Hiyo ndio faida ya kura za wizi za CCM. Hatuwezi kuwalaumu wananchi wa Arusha maana hawajawachagua CCM, bali tume ya uchaguzi ndio iliagizwa iwatangaze CCM.
 
Mbona hata DSM umeme unakatika hovyo, TANESCO watangaze mgawo wa umeme nchini wasiogope ukali wa mfalme, hata yeye hupenda kujinadi msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Ikifika saa tatu wanakata hata sasa hivi amna kitu.
 
Mbona hata DSM umeme unakatika hovyo, TANESCO watangaze mgawo wa umeme nchini wasiogope ukali wa mfalme, hata yeye hupenda kujinadi msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Watu wanaumizwa kimya kimya.
 
Bila kusahau njiro lemala na moshono.lakini ni nyumba za watu wa chadema tu
 
Cheka ung'atwe,kambi ya fisi,matejoo,kwa mama nairo,n.k
Kote huko giza saa hizi
 
Moshi wiki hii yote umeme unakatika asubuhi na kurudi jioni kwa kupokezana maeneo. Mfano jana kwetu ulikua haupo kabisa, leo upo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom