Mgao wa escrow: Jimbo la Muleba limepata 1.6 bilion

Chal

Senior Member
Oct 7, 2010
128
52
Wakuu,
Nadhani si jambo la kushangaza wala siyo habari mpya kwamba nchi yetu imejaa viongozi wabinafsi na wanaojali matumbo yao kuliko utu na utaifa. Kwa kiasi kikubwa tuna upungufu wa viongozi wenye uzalendo.

Msingi wa hoja yangu ni namna baadhi ya viongozi wa umma walivyonufaika na pesa za Escrow wao binafsi ilihali wangeweza kutumia nafasi zao kuwanufaisha watanzania masikini na fukara katika maeneo yao kwa kuchangia katika miradi ya maendeleo.

Sote humu tunafahamu utatezi alioutoa Mama Anna Tibaijuka juu ya uhalali wa yeye kupewa 1.6 bilion mwenyewe ameita huo msaada umetolewa in good faith.

Wakuu, hapa mimi nawaza tu.. Hivi kama ameweza kujipatia 1.6 Bilion in good faith kutoka kwa Ndg Lugemalira peke yake, kwa kiasi gani angeweza kutumia ushawishi huo kukusanya 1.6 bilion zingine au hata zaidi kutoka kwa watu wengine na.kuziingiza katika shughuli za maendeleo jimboni kwake?

Inaonesha Prof Anna Tibaijuka ana ushawishi mkubwa sana kwa matajiri kiasi sanaweza kumsikiliza na kumsaidia, je jimbo lake limenufaika vipi na uwezo wake huo?

Hivi jimbo lake la Muleba halina miradi ya maendeleo iliyosimama kutokana na ukosefu wa fedha? hospitali zina vifaa tiba vya kutosha? akina mama wajawazito wanatembea umbali mfupi kupata huduma wakati wa kujifungua? je huduma ni bora na za kisasa? shule zote za sekondari zina maabara na vifaa vyake? Kuna nyumba za kutosha za watumishi kama waliku, madaktari na wengineo, barabara zote jimboni zinapitika mwaka mzima?

Haya ni baadhi ya maeneo ambayo pesa ile kama Prof Anna Tibaijuka angeitumia kizalendo angeweza kupeleka katika hayo maeneo. Lakini kwa sababu ya "nature" ya viongozi tulionao 1.6 bilioni imekwenda katika shule yake binafsi.

Pamoja nae wapo wanufaika wengine kama Andrew Chenge ambao wao hawajatoka hadharani na kusema kwanini wamepata huo mgao. Taarifa ziononyesha Chenge pia amepokea 1.6 bilioni. Bado hajatueleza matumizi ya hizo fedha yalikuaje? Nadhani anaona ni vijisenti vingine tu.

Wakuu, kwa mtizamo huu, sina kusudi kabisa la kuhalalisha wizi ule na wala mgao uliofanyika kwani kama taifa bado tunahitaji kapu letu lijae na zichotwe humo kwa njia halali kwa ajili ya maendeleo yetu sote.
 
Hela ala yeye binafsi,ametimuliwa anaenda kuomba huruma jimboni kwake na watu tulivyo wajinga tnanaenda kufanya maandamano ya kumpokea mtoto wetu shujaa anayerudi nyumbani kwa kuwa kaonewa na wote tunalaani vikali kuondolewa kwenye cheo utafikiri hicho cheo ni haki yake.Ingekuwa kule kwetu angepokelewa kwa mawe na kufungiwa barabara,hizo ni dhihaka kwa wananchi,wakiiba na wasipokamatwa huwasikii kupiga kelele kuwa jamani nimepataa fungu wana jimbo njoo tule pamoja ,akigundulikana kituo cha kwanza jimboni na kujifanya sasa nitawatumikia wananchi wangu vizuri,huko ni sizitaki mbichi hizi baada ya kuzikosa,sampuli ya akina Tibaijuka ,Chenge na timu yao ni watu wa kuwatosa bila kupepeta kope,mtindo wa kukimbilia majimboni ili kutaka kupata kinga na kuonewa huruma ,ni siasa za maji taka,wananchi tusikubali kutumiwa ni wakati wa kusema imetosha hapana,tutakuwa mazuzu hadi lini?
 
Mh. kwenu ni wapi huko wanakopokelewa kwa mawe!!? Duu mnatisha ka Singasinga Sethi.
 
Chuki dhidi Ya elimu Ya Mtoto wa kike inawasumbua, Mliozoea Kubebwa na Mfumo dume ndo hamuachi kumsakama huyu mama,hakuna mapambano yasiyo na vikwazo
Wanawake wenye akili tupo pamoja nawe
 
Chuki dhidi Ya elimu Ya Mtoto wa kike inawasumbua, Mliozoea Kubebwa na Mfumo dume ndo hamuachi kumsakama huyu mama,hakuna mapambano yasiyo na vikwazo
Wanawake wenye akili tupo pamoja nawe
shule ipo muleba?mbona husemi masharti Rugemalira aliyoyatamka Kikwete ili ampe pesa huyo Tibaijuka?
 
shule ipo muleba?mbona husemi masharti Rugemalira aliyoyatamka Kikwete ili ampe pesa huyo Tibaijuka?

Ukweli ni kwamba mama Tibaijuka kateleza sana kwenye hili. Mimi nimeanza kufikiri hii pesa ilikuwa ni maandalizi au kutunisha mfuko wa kumuandaa kwenye mbio za uraisi kwani hata yeye alikuwa ana hiyo ndoto. Tunafanya makosa sana kuanza kusema kaonewa. Sisi mheshimiwa maige alipofukunzwa uwaziri kwa kashifa ya kuuza twiga tulichukulia ni sawa kabisa. Ndugu zetu wana Muleba naamini mna wasomi wengi ambao watakuja kuchukua nafasi kubwa zaidi hata hiyo ya mama yetu, msikubali kubeba dhambi ya mama Tibaijuka bure. Bilioni 1.6 msidhanie magunia ya senene ni pesa nyingi sana kupewa kama mchango tu wa shule.
 
Malizia kuwa ni nyingi kwako na wala sio kwa wenye nazo
 
Nitawashangaa wanaMuleba kama watamchagua tena Tibaijuka. Kama angekuwa anawajali wanamuleba basi hizo 1.6bn angezipeleka Muleba zingejenga maabara za sekondari ktk jimbo hilo na nyingine kununulia madawati. Lakini kazipeleka Babro-Johanson iliyopo Dar na wanakosoma watoto wa vigogo. Lo!
Angekuwa mzalendo angeboresha shule za kata za Muleba na hata kuwajengea nyumba za walimu. Wanamuleba amkeni.
 
Chuki dhidi Ya elimu Ya Mtoto wa kike inawasumbua, Mliozoea Kubebwa na Mfumo dume ndo hamuachi kumsakama huyu mama,hakuna mapambano yasiyo na vikwazo
Wanawake wenye akili tupo pamoja nawe

Ukiisoma thread vizuri utaona haijazungumza kuhusu mifumo ya kiutawala wala haijaibua chuki dhidi ya elimu kwa watoto wa kike. Hata hivyo kama umefuatilia kwa karibu suala hili utakuwa na taarifa kuwa idadi ya watoto wanaosoma bure pale Babro ni ndogo mno tena sana kiidadi kuliko wanaolipa. Hili jambo linahitaji thread yake kama haipo humu..
 
Back
Top Bottom