Wakuu,
Nadhani si jambo la kushangaza wala siyo habari mpya kwamba nchi yetu imejaa viongozi wabinafsi na wanaojali matumbo yao kuliko utu na utaifa. Kwa kiasi kikubwa tuna upungufu wa viongozi wenye uzalendo.
Msingi wa hoja yangu ni namna baadhi ya viongozi wa umma walivyonufaika na pesa za Escrow wao binafsi ilihali wangeweza kutumia nafasi zao kuwanufaisha watanzania masikini na fukara katika maeneo yao kwa kuchangia katika miradi ya maendeleo.
Sote humu tunafahamu utatezi alioutoa Mama Anna Tibaijuka juu ya uhalali wa yeye kupewa 1.6 bilion mwenyewe ameita huo msaada umetolewa in good faith.
Wakuu, hapa mimi nawaza tu.. Hivi kama ameweza kujipatia 1.6 Bilion in good faith kutoka kwa Ndg Lugemalira peke yake, kwa kiasi gani angeweza kutumia ushawishi huo kukusanya 1.6 bilion zingine au hata zaidi kutoka kwa watu wengine na.kuziingiza katika shughuli za maendeleo jimboni kwake?
Inaonesha Prof Anna Tibaijuka ana ushawishi mkubwa sana kwa matajiri kiasi sanaweza kumsikiliza na kumsaidia, je jimbo lake limenufaika vipi na uwezo wake huo?
Hivi jimbo lake la Muleba halina miradi ya maendeleo iliyosimama kutokana na ukosefu wa fedha? hospitali zina vifaa tiba vya kutosha? akina mama wajawazito wanatembea umbali mfupi kupata huduma wakati wa kujifungua? je huduma ni bora na za kisasa? shule zote za sekondari zina maabara na vifaa vyake? Kuna nyumba za kutosha za watumishi kama waliku, madaktari na wengineo, barabara zote jimboni zinapitika mwaka mzima?
Haya ni baadhi ya maeneo ambayo pesa ile kama Prof Anna Tibaijuka angeitumia kizalendo angeweza kupeleka katika hayo maeneo. Lakini kwa sababu ya "nature" ya viongozi tulionao 1.6 bilioni imekwenda katika shule yake binafsi.
Pamoja nae wapo wanufaika wengine kama Andrew Chenge ambao wao hawajatoka hadharani na kusema kwanini wamepata huo mgao. Taarifa ziononyesha Chenge pia amepokea 1.6 bilioni. Bado hajatueleza matumizi ya hizo fedha yalikuaje? Nadhani anaona ni vijisenti vingine tu.
Wakuu, kwa mtizamo huu, sina kusudi kabisa la kuhalalisha wizi ule na wala mgao uliofanyika kwani kama taifa bado tunahitaji kapu letu lijae na zichotwe humo kwa njia halali kwa ajili ya maendeleo yetu sote.