RIP Dr Judy. Mwenyezi Mungu atakulipa na wote waliojikuta katika hali kama hii.
Watanzania tumekuwaje? Hatuoni kuwa huyu alijondoa katika tabaka lake kutumikia nchi na watu wake (class suicide)? Watu wa aina yake wengi wako huko Marekani, Geneva, Uingereza na kwingine wakilipwa mishahara minono yeye pamoja na tabaka lake binti aliyozaliwa na kulelewa kwa mazingira yake alisomea nje na ndani ya TZ kama mtoto wa Balozi, Waziri Mkurugenzi Mkuu nk. Kwa unyofu alikubali kusomea udaktari akabaki bongo kuwahudumia walalahoi wa Dar es Salaam lakini bado hatuoni hilo! chuki itatumaliza. Hata kama amekufa na ugonjwa gani, tabia yake ya kikazi na mazingira magumu ya kazi yake kwa TZ inawezekana kabisa ilisababisha kuugua ugonjwa ambao kama angekuwa sehemu nyingine ya kiwango chake asingekufa mapema hivyo.
Kufia nje ni tatizo ambalo ni la Kimfumo. Nikikumbuka viongozi wetu waliofia nje, nikilinganisha na hali ya Afya ya Mzee Mandele anayetibiwa nyumbani kwake na watu wake naamini kuwa huenda wasingestahili kufa haraka kiasi hicho kama wangetibiwa hapa. Watu uliowahudumia kwa uadilifu wanatupenda na kutujali zaidi wasiotujua hawatuthamini ni rahisi kufanya uamuzi wa kuondoa mashine haraka hata kama ingewezekana kupata nafuu au kupona. Kwa kweli maisha na afya ya Mzee Mandela yanatutengenezea dhana ya kuwekeza katika Afya na watumishi wa afya kama msingi mwingine wa ukombozi katika bara la Afrika hebu tuchukue hatua kuboresha huduma zetu za Afya na kuwapatia haki watumishi wa afya waliojitoa muhanga kufanya kazi hiyo ili hata marafiki wa nje kama Clinton wakisema wanaweza kugharamia matibabu bora zaidi katika nchi zao tuweze kusita kuwaamini kuwa ni bora kuliko zile tulizojenga wenyewe Mungu Ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.