Mgana Msindai arudishe kadi ya CHADEMA

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Mwaka 2010, baada ya kuangushwa katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Jimbo la Iramba mashariki, na pia kuenguliwa na NEC ya CCM kule Dodoma, Mgana Msindai alihqmia CHADEMA, akapewa kadi. Wakapanga na Tundu Lissu ili wakafanye press conference Singida.

Baadhi ya watu wa CHADEMA na waandishi walifika eneo la Ukumbi, yeye akasema gari imeharibika njiani akitokea Dodoma kuja Singida.

Baadaye alipotea katika mazingira ya siasa, hadi alipokuja kuibuka juzi akiwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Yeye ni Mwanachama halali wa CHADEMA, na alichukua kadi na kuilipia kwa miaka 5, na alitaka kugombea Ubunge wa jimbo hilo hilo kupitia CHADEMA. Awe Muungwana arudishe kadi yetu mahali alipopewa arudishiwe sehemu ya ada ya miaka iliyobaki.
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,634
4,472
Naona sasa imekuwa ni mwendo wa kudaiana kadi. Hata hivyo mbona wananchi wengi tu wana kadi za vyama zaidi ya kimoja.?
 
MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,048
1,095
Ni kweli kwani hata mimi nilikuwa shuhuda wakati Msindai anachukua kadi ya CHADEMA. Tulienda naye mpaka nyumbani Isanzu.
 
Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,519
1,396
KADI..KADI..KADI...KADI!! naona mmeshasahaulishwa kuwaza mambo ya maana kuhusu mustakabali wa nchi yetu, mnajadili CARD za vyama.
 
segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Mi nachukia watu kucheza ngoma ya vuvuzela la ccm,tusipokuwa makini ccm ndo watatumia huu mwaya kuhamisha mawazo ya watu ili kufunika ishu iliyoko mezani sasa hv yaani hela zetu walizoficha mafisadi uswis na kwingineko.Magamba wanatakiwa kuwawekea ulinzi wa mbwa mkali kila wanapojaribu kujitutumua wanang'atwa maana tukijisahau wataanzisha ufisadi mpya kwa sababu wanataka tuhame kwenye hoja za msingi
 
Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Mwaka 2010, baada ya kuangushwa katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Jimbo la Iramba mashariki, na pia kuenguliwa na NEC ya CCM kule Dodoma, Mgana Msindai alihqmia CHADEMA, akapewa kadi. Wakapanga na Tundu Lissu ili wakafanye press conference Singida.

Baadhi ya watu wa CHADEMA na waandishi walifika eneo la Ukumbi, yeye akasema gari imeharibika njiani akitokea Dodoma kuja Singida.

Baadaye alipotea katika mazingira ya siasa, hadi alipokuja kuibuka juzi akiwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Yeye ni Mwanachama halali wa CHADEMA, na alichukua kadi na kuilipia kwa miaka 5, na alitaka kugombea Ubunge wa jimbo hilo hilo kupitia CHADEMA. Awe Muungwana arudishe kadi yetu mahali alipopewa arudishiwe sehemu ya ada ya miaka iliyobaki.

Nakubali ni kweli kulikuwa na suala kama hilo, lakini Mgana Msindai alipoingia mitini CHADEMA kule Singida, hatukutilia maanani, tunajua mtu hawezi kuwa mwanachama wa vyama viwili wazi wazi, na suala la mtu kuwa na kadi ya Chama Kiingine sio suala la uanachama. Kuna kanuni zake.

Ndio maana leo ukienda ofisi za CUF utakuta kadi za CCM ambazo wanachama wamerudisha, au ukienda CCM utakuta kadi za CHADEMA Mfano zile zilizorudishwa Jangwani mbele ya watanzania kwenye Televisheni ya Taifa tunayoilipia kodi, Nape amezirudisha wapi? Tukomae watanzania.

Tusipeleke nchi kwa mijadala ya propaganda, tunajiangamiza wenyewe kushindwa kufikia maendeleo ya kweli kulingana na rasilimali tulizo nazo kwa kuendekeza utani zaidi katika masuala muhimu ya Kitaifa.

Hilo suala la kadi ya CHADEMA kwa Msindai Mwambieni Nape akamdai, maana ni Mwanachama wao kwa sasa. Wakidaiana wakiona inawasumbua waisalimishe CHADEMA
 
NO EXCUSE

JF-Expert Member
Sep 10, 2012
417
212
Enzi zetu kila mwanafunzi wa sekondari kuwa mwana CCM umoja wa vijana ILIKUWA LAZIMA. Baada ya hapo JKT Ikawa LAZIMA. Na kupata kazi ilikuwa lazima uwe mwana CCM.

Baada ya kuja mfumo ya vyama vingi watu wengi walianza kuwa na kadi za NCCR MAGEUZI. Baada ya hapo walewale wakachukua kadi za Cuf na kisha TLP leo wanazo za CDM.

Watu wamekuwa walichukua kadi hizo kulingana na matumaini yao kwa manufaa ya umaarufu wa chama husika wakati huo. Labda tujadili kama ni kosa watu hawa kuwa na kadi za vyama karibu vyote vilivyowahi kuvuna hapa nchini.

Hata waanzilishi wa CCK NA ADC hatujawahi kusikia wamerudisha kadi za uanachama wa vyama walilokuwa
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,380
10,152
KADI..KADI..KADI...KADI!! naona mmeshasahaulishwa kuwaza mambo ya maana kuhusu mustakabali wa nchi yetu, mnajadili CARD za vyama.

Actually hilo ndilo lengo kuu la akina Nape na hoja hii ya kadi isiyo na mashiko kwa watz;wanataka tusahau kuwahoji kwa nn maisha ya TZ yapo hovyo ili hali TRA wametoa taarifa kuwa wamekusanya kodi kwa asilimia zaidi ya 100!

Mm sina maji,umeme,matibabu na wajukuu zangu wanamaliza darasa la 7 bila kujua kusoma wala kuandika lkn wanafaulishwa kwenda secondari kwenye shule za kata LKN leo hii badala ya at least kutuambia mmejipanga vipi kumaliza kero hiz;NAPE UNAKUJA NA MADAI YA KITOTO KAMA HAYA YA KADI?

Tueleze maazimio yenu ya Dodoma hivi karibuni mlijadili lolote kuhusu umeme ulivyo athiri biashara yangu ya kinyozi hapa Kyela mjini?
 
swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
37
kujadili eti mtu fulani ana kadi ya chama fulani ni ufinyu wa fikra na upotevu wa muda badala ya kujadili ni vipi tutapata majibu ya matatizo yetu tuliyonayo yanayosababishwa na viongozi wetu. tunayo matatizo mengi ya msingi hayo ndiyo tuyajadili.
 
Ally Kanah

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
1,479
388
Mwaka 2010, baada ya kuangushwa katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Jimbo la Iramba mashariki, na pia kuenguliwa na NEC ya CCM kule Dodoma, Mgana Msindai alihqmia CHADEMA, akapewa kadi. Wakapanga na Tundu Lissu ili wakafanye press conference Singida.

Baadhi ya watu wa CHADEMA na waandishi walifika eneo la Ukumbi, yeye akasema gari imeharibika njiani akitokea Dodoma kuja Singida.

Baadaye alipotea katika mazingira ya siasa, hadi alipokuja kuibuka juzi akiwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Yeye ni Mwanachama halali wa CHADEMA, na alichukua kadi na kuilipia kwa miaka 5, na alitaka kugombea Ubunge wa jimbo hilo hilo kupitia CHADEMA. Awe Muungwana arudishe kadi yetu mahali alipopewa arudishiwe sehemu ya ada ya miaka iliyobaki.

View attachment 74039 hahahahaahahahahahaha
 
Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,519
1,396
Actually hilo ndilo lengo kuu la akina Nape na hoja hii ya kadi isiyo na mashiko kwa watz;wanataka tusahau kuwahoji kwa nn maisha ya TZ yapo hovyo ili hali TRA wametoa taarifa kuwa wamekusanya kodi kwa asilimia zaidi ya 100!

Mm sina maji,umeme,matibabu na wajukuu zangu wanamaliza darasa la 7 bila kujua kusoma wala kuandika lkn wanafaulishwa kwenda secondari kwenye shule za kata LKN leo hii badala ya at least kutuambia mmejipanga vipi kumaliza kero hiz;NAPE UNAKUJA NA MADAI YA KITOTO KAMA HAYA YA KADI?

Tueleze maazimio yenu ya Dodoma hivi karibuni mlijadili lolote kuhusu umeme ulivyo athiri biashara yangu ya kinyozi hapa Kyela mjini?

babu punguza hasira, 2015 sio mbali!
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Kadi ni nini? Msindai ni nani?
Kama ni huyu mwenye mahipsi mwacheni hana madhara
 
manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,067
10,707
Kwani sheria inasemaje kwa mtu anaemiliki kadi ya vyama zaidi ya kimoja?
 
tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,512
490
Hivi Sakata la hela zetu kufichwa uswisi limeishia wapi?.. Kagasheki anasemaje kuhusu wizi wa wanyamapori kupitia KIA, je, mabosi wake wanasema walihusikaje?.. Pembe za ndovu zilizokamatwa ughaibuni zilisafirishwa na katibu mkuu wa mafisadi au kuna wengine nyuma yake?
 
mmkhotya

Member
Nov 25, 2012
43
5
Card za vyama viwili au hata vitatu sio issue sana. Tunatakiwa kujadili mambo ya msingi kama jinsi ya kuleta maendeleo.
 
mmkhotya

Member
Nov 25, 2012
43
5
Msindai ni Mkt halali wa CCM mkoa wa Singida. Na anafanya kazi ya kuijenga CCM. Hoja zingine hazina mashiko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom