MGAMBO WETU.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,310
4,538
WETU MGAMBO.

1)Siwezi mi kuamini,kama ni wao wenyewe.
Imetoka ofisini,wale waje watendewe.
Ahadi zi mazishini,laona jicho la mwewe.
Hawa ndo wetu mgambo,na ndo kazi waliotumwa.

2)Wayatenda ya zamani,enzi zile za utumwa.
Hiingii akilini,kwamba wao.wakutumwa.
Ila niwape poleni,hili halitojazimwa.
Hawa ndo wetu mgambo,na ndo kazi walotumwa.

3)Biashara zifungeni,wala mna watetezi.
Uhuru na ubinyeni,watu wenu wawe wezi.
Hapo na mfurahini,yakisha kufa malezi.
Hawa ndo wetu mgambo"na ndo kazi walotumwa.

4)Na mateke ya usoni,endeleni kuwapiga.
Ipo siku karibuni,taona mnachofuga.
muwatie gerezani,kabla hayajavuruga.
Hawa ndo wetu mgambo,na ndo kazi walotumwa.

5)Mikanda washushieni,epukeni usaliti.
Na nguo wanyang'anyeni,timizeni mkakati.
Tena hivi karibuni,mtakua hati hati.
Hawa ndo wetu mgambo,na ndo kazi walotumwa.

Shairi=WETU MGAMBO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom