Mfupa uliomshinda Fisi hakuna mnyama atakaye uweza

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,248
Habarini,

Katika maisha yetu huwa kuna watu wanapenda, kupitiliza na akili ya upendo ukishindwa kuitawala hutopokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote na kila atae kushauri lolote kuhusu mahusiano, utamuona kama anaingilia mambo ya maisha yako.

Fisi bwana huwa hashindwi na mfupa, na ndio maana inaaminiwa kuwa fisi anapenda sana mizogo. mara nyingi mizoga huwa teyari imeshalaruliwa na wanyama wengine, fisi anakuja kumalizia. ikitokea fisi akakutana na mfupa ambao umeshinda kaa ukijua kuwa hapo porini hakuna mnyama atakae thubutu kuusogelea mfupa ulio mshinda fisi.

1595103861967.png


Katika maisha yetu ya kibinadam utakuta mtu anajua fika mwanaume yule ameachana na mke wake, na mwingine anajua fika mwanamke yule ameachana na mume wake. lakini bado mtu wa kati anaanzisha mahusiano na mtu alietoka kuachika wewe ni nani uuweze mfupa alioushinda fisi?

Sisemi kuwa kila alieachwa ana tabia mbaya no lakini cha kujiuliza ni kwanini ameachwa? au ni kwanini wameachana?

Vijana wengi wamekuwa wakilia lia kuchoshwa na tabia za kina dada walipachikwa jina la singlemother sijui na wadada nao wanalia kwa tabia wanazofanyiwa na single father.

Kumbe baadhi ya single mather na singlefather wana matatizo
labda ni walevi kupindukia na wengine wanashindwa kabisa kuacha mawasiliano na wazazi wenzao walioachana nao.

Ndugu yangu msomaji narudia tena kwa herufi kubwa "MFUPA ULIOMSHINDA FISI HAUTOUWEZA" Mwanaume mwenzako amemshindwa huyo mwanamke wewe unajifanya kidume kwa kuzani mwenzako hakuwa na akili unajiingiza kichwa kichwa mwisho wake ni majonzi tu na kujiona una mikosi.

1595103812396.png


Na wewe mwanamke, mwanamke mwenzako amemshindwa huyo bwana, wewe unajiona malkia kuwa hushindwi na mfalme.

Kama ingekuwa ni mari yangu ningewashauri watu wanaojiingiza kwenye mahusiano waache kabisa kujiingiza kwenye mahusiano na watu ambao teyari walishakuwa kwenye mahusiano. Ukiona mwanume ameshazaa na mwanamke mwingine ambaye yupo hai usithubutu kuanzisha naye mahusiano.

Ukiona mwanmke amezalishwa na mwanaume ambaye yupo hai na ameachwa shituka na ujiulize kwanini ameachwa. Wewe ni nani utakae weza kuutafuna mfupa alioushindwa fisi?

N.B
Lengo si kutenganisha, si unajua akili za kuambiwa unatakiwa uchanganye na za kwako kama umempenda single mather au single father endelea kupendana nae ila tumia akili kufikilia mara mbili mbili.
 
Ukweli huwa hauwekwi wazi kwa viumbe hawa wenye majina ya ex Kama hukufanikiwa kumwona ktk mahusiano yake ya kwanza mkikutana atamvisha ubaya ex wake na kujifanya mtakatifu hapo ndipo kipengele kitakapoanza ushauri wangu kama utapenda ex wa mtu hakikisha uliwahi kushudia maisha yake ya mahusiano sio kusimuliwa na yeye hakuna mtu anaweza sema mm niliachana na mke wangu nilikuwa namtesa au nilikua sina nidhamu ktk mahusiano yetu na uzuri wao huwa wanatafuta mtu ambaye hajawahi kuona alichoficha nyuma ya pazia hapo ndipo unajikuta ktk tanuri la nyuklia
 
Kwa kifupi kazia kuwa singo maza haolewi kwa mujibu ya kanuni hiyo ya "mfupa uliomshinda fisi ww utawezea wap"
 
Hayo yote ulioyaandika unaweza kuyatumia kwa wale ambao bado hawajaolewa/oa pia, kwamba kuna sababu kwa nini bado wako single, hivyo unajichosha bure tu kwa maoni yangu, tafuta mtu anayekukubali kama ulivyo na aliyetayari kuwa na wewe awe aliolewa au hakuolewa, maadamu ameshamaliza kule alikotoka haina noma, wote sisi ni binadamu tunafanya makosa na tunastahili second, third, fourth, fifth, sixth chance, ...
 
Ndefu kichizi nimeshindwa kuisoma



Ila fisi anakula mizoga ,leftover za nyama waliowinda wenzake ,ni muoga kutwa kucheka cheka ovyoo kama bwabwa
 
Wewe nawe unaongea pumba.

Aliyeacha naye si kaachwa? Au akiacha ile title ya single maza au singo faza inafutika? Huo mfano wa fisi haufai kwenye mahusiano. Mikuno ni tofauti.
 
Back
Top Bottom