Mfungo na adha zake

Mfungo na adha zake

(Mimi ni mkatoliki lialia)

1. Nchi yetu wengi tumezaliwa tukajikuta kwenye nchi nyema ya ajabu ambapo wakristu na waislamu wanaishi pamoja kwa upendo

2.Unakuta kwenye familia moja kuna mchanganyiko wa dini lakini wanashirikiana pamoja kwenye mambo ya kiukoo bila kujua mwenzake ni dini gani

3. Ni Tanzania pekee muislamu anamnunulia mtoto wake nguo mpya siku ya krismass na kusherekea na watoto wenzake wa kikristo na virse versa kwa wakristu wakati wa idd lazima pilau la nguvu lipigwe

4. Ni Tanzania pekee akiwa anachinja kitoweo lazima amwite jirani yake muislamu amchinjie

5. Ni Tanzania pekee wakati wa mfungo wa ramadhani wakristu huvaa kanzu kama wavaao ndugu zao waislamu na mara nyingi kupunguza kula hadharani kwa hiari ili kutowakwaza ndugu zao waislam

6. Ni Tanzania pekee, wakati wa mfungo vijana hupita kuwaamsha watu kwa ngoma usiku wakati wa daku hata kwenye nyumba za kikrisu lakini tunavumiliana

7. Ni Tanzania pekee ambapo siku zikikaribia mfungo kuisha , vijana hao hupita kila nyumba bila kujali dini na kuzawadiwa.

8. Kwa taarifa yako mtoa mada, wengi wanaowatunza vijana hao ni wakristu. Kwanza wanawapongeza vijana hao ambao nje ya dini ni wanajamii wenza kwa kuweza kulinda imani yao pili kinaendelea kukuza mashirikiano kati ya dini zote mbili.

9. Mimi nashauri tuendelee kutunza utamaduni huo ambao tumeuridhi kwani ni moja wapo ya vitu vinavyofanya nchi yetu kuwa na baraka na dini kuheshimiana tofauti na chi nyingine ambazo hizi dini watu wanagombana
 
Kwanza natanguliza wazi mimi ni Muislam wa kuzaliwa na kuamini. Pia sina lengo la kukashifu dini yoyote au imani ya mtu. Bali najaribu kuelezea mambo yanayojili katika mwezi huu wa Ramadhani ambayo , kisheria na kiustaarab hayako sawa kabisa.

Nitaelezea jambo moja. Wenyewe tumezoea kuliita kupiga daku. Hizi ni ngoma wazozunguka vijana kupiga katikaajumba kwa lengo 'sijui ni lipi'. Nasema sijui ni lipi.

Kipindi cha nyuma ilikua zaidi wanazunga majumbani usiku kuamsha watu kula chakula cha usiku mkubwa(daku). Hivyo mantiki yake ilikua ni kuamsha watu, na walioamshwa waliwapa senti kidogo kama sadaka.

Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia-Siku hizi kuna alarms, pia suala la usalama kuwa dogo maeneo mengi hawa wamaepungua kufanya shughuli hii.

Lakini kupiga mchana sijui hasa mantiki yake ni nini.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni hiki.

Leo mida ya mchana nilikua dinning, na bi mkubwa(mwenye shida ya pressure), na baadhi ya family members. Ghafla tukasikia ngoma zinapigwa ndani kwa nguvu wakiimba. Waliimba na kupiga ngoma kwa muda wa dakika takribani kumi. Finally nikatoka na kuanza kuwaeleza kuwa wanakosea, wakaanza kulalamika kuwa siwafanyii vyema, niwape sadaka waondoke. Sikuwapa hata sh moja, wakaendelea kupiga ngoma kwa takribani dakika 20, walipochoka wakaondoka.

Hii ni tabia kwa watu waliokulia mazingira ya mikoa ya kiislamu ni common sana.

Ni mazoea sana, ni tabia za kawaida. Lakini kiundani zina athari sana. Na inapashwa ikemewe sana.

1. Kuingia nyumba ya mtu bila kuruhusiwa hiyo ni trespassing na ni kosa kisheria, ukimkuta mtu aliye 'pinda', hawa vijana watalala 'ubaoni'.

2. Ni mwanzo na dalili za wizi.

3. Inaweza kuwa ni uchoraji wa mazingira ya ujambazi. Mchana daku usiku wanarudi ujambazi.

4. Inaweza sababisha mauaji. Mfano hawajui ni nani yumo ndani na ana maradhi gani, sauti za ghafla zinaweza kuleta mauti.

5. Si kila nyumba ni waislam, na hata kama ni waislamu si wote wanataka 'kelele' hizo.

Ndugu zangu waislam(hasa), tukemee suala hili na tuache kulilea, tunatengeza vibaka, na kulemaza kuacha kufanya kazi kutegemea kupewa 'sadaka'.
Ukiona kero, rudi mkoani kwenu, mbali na dini, hiyo ni kama tamaduni yetu ya watu wa ukanda wa pwani, ilimradi halivunji sharia za dini, na sheria za nchi, hatutaacha ng'o kisa, we m bara umechukia.
 
Yaaan mm najiulizaga hivi Wao hawajui muda huu ni wakuamka kwenda kula daku au kwenda misikitini
Vitu vingine bana useme Wanakujia juu ati makafiri
Mi pia ni mwislam na hawa madogo hua wananiboa coz wanaficha kuombaomba pesa nyuma ya kuamsha watu kula daku na hii inadhihirika pale wanapokuja na ngoma zao hadi mchana au kuendelea kupiga ngoma zao kwa muda mrefu usiku usipotoka kuwapa pesa ni kama sasa wanafanya kukomoa kisa hujawapa pesa so wakusumbue na makelele..

Ni tabia mbaya na haipaswi kuendelea ila na we kabla hujawakosoa wenzio kua hawajui muda wa kwenda msikitini jiulize pia kwani upande wa pili hawajui muda wa kwenda kanisani hadi kuwe na ile KENGELE inayopiga kelele kila saa 12 asubuhi, saa 6 mchana na jioni?
 
Sasa si waweke adhana kwenye alarm halafu iwafikie wale wanaotaka tu, wanaoona usumbufu wasiipate.

Mbina Quran yenyewe imeandika dini hailazimishwi?

Unakataa kusumbuliwa na wapiga daku kwa sababu una alarm, halafu unakubali wengine wasumbuliwe na adhana?

Mbina una double standard hivyo?
Halazimishwi mtu kuifata dini,yaani kufanya au kusilimu.

Ila adhana ikiadhiniwa ni lazima mtu aende huko kunakoadhiniwa...kama hataki"atajuana yeye na MUNGU.
 
Halazimishwi mtu kuifata dini,yaani kufanya au kusilimu.

Ila adhana ikiadhiniwa ni lazima mtu aende huko kunakoadhiniwa...kama hataki"atajuana yeye na MUNGU.
Ukishamlazimisha mtu kusikiliza adhana,tena ya mahubiri, ushamlazimisha mtu kufuata dini.

Kama dini hailazimishwi, adhana isipigwe misikitini kiasi cha kuwafikia watu ambaohata si Waislamuna hawataki kuwa Wasilamu.

Kwao ni kelele za kero tu.

Karaha tu.

Mnawalazimisha kitu ambacho hawakitaki.
 
kwa hiyo kero uliyooiona ni ya kuamshw
Kwanza natanguliza wazi mimi ni Muislam wa kuzaliwa na kuamini. Pia sina lengo la kukashifu dini yoyote au imani ya mtu. Bali najaribu kuelezea mambo yanayojili katika mwezi huu wa Ramadhani ambayo , kisheria na kiustaarab hayako sawa kabisa.

Nitaelezea jambo moja. Wenyewe tumezoea kuliita kupiga daku. Hizi ni ngoma wazozunguka vijana kupiga katikaajumba kwa lengo 'sijui ni lipi'. Nasema sijui ni lipi.

Kipindi cha nyuma ilikua zaidi wanazunga majumbani usiku kuamsha watu kula chakula cha usiku mkubwa(daku). Hivyo mantiki yake ilikua ni kuamsha watu, na walioamshwa waliwapa senti kidogo kama sadaka.

Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia-Siku hizi kuna alarms, pia suala la usalama kuwa dogo maeneo mengi hawa wamaepungua kufanya shughuli hii.

Lakini kupiga mchana sijui hasa mantiki yake ni nini.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni hiki.

Leo mida ya mchana nilikua dinning, na bi mkubwa(mwenye shida ya pressure), na baadhi ya family members. Ghafla tukasikia ngoma zinapigwa ndani kwa nguvu wakiimba. Waliimba na kupiga ngoma kwa muda wa dakika takribani kumi. Finally nikatoka na kuanza kuwaeleza kuwa wanakosea, wakaanza kulalamika kuwa siwafanyii vyema, niwape sadaka waondoke. Sikuwapa hata sh moja, wakaendelea kupiga ngoma kwa takribani dakika 20, walipochoka wakaondoka.

Hii ni tabia kwa watu waliokulia mazingira ya mikoa ya kiislamu ni common sana.

Ni mazoea sana, ni tabia za kawaida. Lakini kiundani zina athari sana. Na inapashwa ikemewe sana.

1. Kuingia nyumba ya mtu bila kuruhusiwa hiyo ni trespassing na ni kosa kisheria, ukimkuta mtu aliye 'pinda', hawa vijana watalala 'ubaoni'.

2. Ni mwanzo na dalili za wizi.

3. Inaweza kuwa ni uchoraji wa mazingira ya ujambazi. Mchana daku usiku wanarudi ujambazi.

4. Inaweza sababisha mauaji. Mfano hawajui ni nani yumo ndani na ana maradhi gani, sauti za ghafla zinaweza kuleta mauti.

5. Si kila nyumba ni waislam, na hata kama ni waislamu si wote wanataka 'kelele' hizo.

Ndugu zangu waislam(hasa), tukemee suala hili na tuache kulilea, tunatengeza vibaka, na kulemaza kuacha kufanya kazi kutegemea kupewa 'sadaka'.
a daku ila kelele za disco hujaziona na jee kwa nini husemi
 
Ukishamlazimisha mtu kusikiliza adhana,tena ya mahubiri, ushamlazimisha mtu kufuata dini.

Kama dini hailazimishwi, adhana isipigwe misikitini kiasi cha kuwafikia watu ambaohata si Waislamuna hawataki kuwa Wasilamu.

Kwao ni kelele za kero tu.

Karaha tu.

Mnawalazimisha kitu ambacho hawakitaki.
Vumilia tuu hata wenzio wanavumilia kengele ya roma, nashukur maana ilikuwa alarm ya kwenda shule
 
Ukishamlazimisha mtu kusikiliza adhana,tena ya mahubiri, ushamlazimisha mtu kufuata dini.

Kama dini hailazimishwi, adhana isipigwe misikitini kiasi cha kuwafikia watu ambaohata si Waislamuna hawataki kuwa Wasilamu.

Kwao ni kelele za kero tu.

Karaha tu.

Mnawalazimisha kitu ambacho hawakitaki.
Unajua maana ya kulazimisha?

Ukitaka kulazimisha unayoitaka wewe"hata miziki majumbani basi isiwashwe,maana hata sisi husikia na wengine hatupendi.

NB:
Kulazimisha yaani kushurutisha kufuata.

Adhana inawaita walioamini waislamu,asiehusika na uislamu halazimiswi aendelee tu na shughuli zake sio lazima.

Maneno yako wazi hayo.
 
Ukishamlazimisha mtu kusikiliza adhana,tena ya mahubiri, ushamlazimisha mtu kufuata dini.

Kama dini hailazimishwi, adhana isipigwe misikitini kiasi cha kuwafikia watu ambaohata si Waislamuna hawataki kuwa Wasilamu.

Kwao ni kelele za kero tu.

Karaha tu.

Mnawalazimisha kitu ambacho hawakitaki.
Aya kwenye kitabu cha Quran imesema"
Halazimishwi mtu kuifuata dini.
Yaani kuifuata.
Kama adhana inaita na wewe hutaki"acha hulazimishwi.
 
Dah, wee jamaa mchonganishi aseee. Nimejikuta hata sjui niandikaje ati.

Ila unajua, hii kitu siku hizi hamna kabisa kama zamani coz tangu mwezi umeanza huu mie sijakutana na wapiga daku hata mara moja na mpaka usiku nakuwepo kwenye mitaa mbalimbali ya jiji.

Kiukweli nilijua huu mtindo wa daku umeshakufa ndio kwanza nimekuja kuona hii mada hapa nikakumbuka hii daku, zamani ilikuwa ni daku kweli aisee ila siku hizi hamna kitu.

Kuna jamaa alikuwa anacheza pale mbele kavaa gunia kama msuli halaf sjui kaweka nini inafanana na mshipa hivi. Hatarious aseee.

Those days bhana. Acha tu mkuu.
 
Kweli kabisa siku hizi daku sizisikii kabisa.

Zamani walikuwa hawakosi kila usiku na siku ya idi lazima wazunguke asubuhi wakipiga vingoma vyao.

Wakishapiga nyimbo zao mbili tatu wanamalizia na........."Mama Mwajuma ni mtu wa imani ukimwomba maji akugeia chai, kikombe cha kwanza andazi mkononi, kikombe cha pili kwaheri tunakwenda"
 
Umetoa hoja pia kwamba zamani mantiki ya hao vijana ilikuwa kuwaamsha watu waliolala wale daku. Siku hizi kuna alarm. Watu hawahitaji kuamshwa.

Nikakuuliza, muazzin naye anaamsha watu waliolala wakaswali. Kwa kuwa kuna alarm siku hizi, tuache kufanya azzana?

Hujajibu.
We jamaaa mbishi kuelewaa sanaee
 
MTOA MADA NIKUSAIDIE KITU
1. Kwa maeneo mengi mfano kwa jiji la Dar es salaam hilo suala la watu kupita kuamsha daku na kanda ya Pwani sio kitu kigeni na wala hawavamii nyumba za watu kama unavyojaribu kupotosha.
2.Tabia ya wizi ni tabia ya mtu mwenyewe sio mpaka watu wakusanyike waamshe daku wizi ndo utokee. Panya road wale walikuwa ni waamsha daku?
3.Wale wapitaji wanapita zao njiani na kama wamepita katika eneo lako ukaona wanakupigia kelele kama unavyodai toka nje ongea nao kistaarabu halafu wataondoka na pia hujalazimishwa au kuandikwa katika maandiko ya kiislam kwamba lazima uwape hiyo pesa. Ukijisikia kuwapa ni utashi wako na usipojisikia kuwapa ni utashi wako vilevile.
Na pia huo mda waliokaa hao vijana kama angewahi kuwapa japo mia tano angeokoa japo 15% za hizo kelele ...huyu nae ni wale wale wanaotoa sadaka halafu mtaa mzima ukajua.
 
Ninakumbuka ngoma za kula daku tulipokuwa wadogo huku kwetu Kwamtogole zilipigwa baada ya insha, kuna mama mmoja alikuwa mnene sana.
Watoto wa kula daku wamekwenda kwake wakaanza kuimba “ mke mnene sioi mke mnene sioi bwana. Akilala kitandani kama gunia la nazi bwana.” Aliwafukuza tena akiwaonyesha hela aliyopanga kuwapa.
Hahaha kuna watu sana kipaji cha kuimba papo kwa papo aisee, hata mimi nakumbuka kipindi nikiwa mdogo ilikua ukifanya tukio basi usiku jiandae kuimbwa kwa mashairi ya kuudhi.
Mungu amlaze mahala pema peponi aliekuwa kinara wa mashairi.
 
Sasa si waweke adhana kwenye alarm halafu iwafikie wale wanaotaka tu, wanaoona usumbufu wasiipate.

Mbina Quran yenyewe imeandika dini hailazimishwi?

Unakataa kusumbuliwa na wapiga daku kwa sababu una alarm, halafu unakubali wengine wasumbuliwe na adhana?

Mbina una double standard hivyo?
Mm nafikiri wangeweka sound proof msikitini ili sauti isisikike, pia swala la hao wapiga ngoma huku kwetu wamewekeana mipaka, ukiingia kwy mipaka ya mtu mwingine ni vita.
 
.
Nikakuuliza, muazzin naye anaamsha watu waliolala wakaswali. Kwa kuwa kuna alarm siku hizi, tuache kufanya azzana?

Hujajibu.
Sio kusudio la adhana kuamsha watu waliolala, lengo la adhana ni kuwajulisha waliomacho kuwa muda wa swala umeingia. Watu waliolala wanatakiwa waswali pale watakapo amka. Adhana ni utambulisho muda wa swala umeingia.
 
Back
Top Bottom