Mfundishe mwanao kuwa na furaha; Usimfundishe kuwa tajiri.

Mithros

Member
Sep 16, 2019
9
8
Habari wana JF, natumaini mtakuwa wazima. Hili litakuwa chapisho langu la kwanza humu jukwaani na ningependa kuongelea kuhusu impact ya hayo mambo mawili( furaha na utajiri) kwenye saikolojia ya mwanao.

Kwanza nitatanguliza kisa hiki;

Nina rafiki yangu wa kitambo mno---nadhani toka tunasoma darasa la tatu hivi. Huyu jamaa kiufupi naweza muelezea kama mtu ambae ana uwezo wa kuridhisha wa kufikiri na ile akili ya 'nje ya darasa'. Kitaaluma hakuwa vizuri na hapo tu ndipo naweza sema tulipishana maana alikuwa akiweka wazi mara kwa mara kuwa hakuwa anapenda kusoma. Nje ya darasa alikuwa vizuri kwenye mpira wa miguu, extra-curricular activities na over-the-years amejifundisha skills nyingi nyingi tu. Bahati mbaya hakuweza kuendelea na masomo ya mbele...baada ya kuhitimu kidato cha nne na nilichaguliwa kwenda kusomea mkoa mwingine (A- Level) hivyo tulikuwa tukikutana zile siku za rikizo.

Huyu jamaa kalelewa na single-mother, hamjui baba yake na naweza sema kapitia changamoto nyingi nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine nimeepushiwa. Japo alikuwa hapendi mambo ya shule, tulipokuwa tukiketi na kuongelea mambo ya maisha...angeanza kunipa ndoto zake, jinsi anavyotaka kuwa tajiri anae heshimika, amjengee mama yake nyumba, anunue gari, sijui afungue biashara hii na ile, na mara moja moja angeongelea kutembelea vivutio mbali mbali duniani.

Hizo ndoto zake hazikuwahi kubadilika. Kilichobadilika ni jibu ambalo angenipa pale nilipomuuliza angefanikiwaje kihivyo wakati shule aliacha. Kuna wakati ningekuta kajifunza mambo ya Music Production na kuniambia vile ambavyo angetoka kimaisha kwa kuwa DJ. Ningemuuliza kama ashaanza kujaribu bahati yake ndipo angeniambia kuwa hakuwa na vifaa muhimu vya kuanzia. Siku nyingine ningekuta kajifunza kuandika riwaya, screen-plays, nk. Na kuniambia kuwa angeandika kitabu au 'muvi' maarufu ambayo ingemtoa kimaisha...alichosema ni kuwa hakuwa na vifaa. Baadhi ya mambo mengine ambayo angeniambia yangemtoa(ambayo ningekuta kajifunza vizuri) ni mpira, mambo sijui ya kuanzisha tech start up, alikuwa kajifunza software nyingi nyingi kwenye Internet Cafe jirani na angesema angeajiliwa kufanya kazi moja wapo kwenye hizo zote alizojua. Pia alikuwa na mawazo mengi mengi ya biashara.

Miaka ilienda, na hakuweza kufanya kitu chochote kwenye hayo aliyojifunza. Ile niko mwaka wangu wa pili chuo, kulitokea dharula na ikanibidi niende nyumbani. Kufika kule, haikuwa dharula kubwa kivile na ndani ya wiki ningerudi chuo. Nilimuulizia huyo rafiki yangu...na niliyoyasikia yalinishangaza kidogo hivyo ilinibidi nikamuone kujihakikishia....na yalikuwa kweli.

Ndani ya muda mfupi alikuwa kabadilika sana, alikuwa kakonda kweli kuliko nilivyokuwa nakumbuka, na alikuwa amenunua estate kubwa. Alikuwa na magari kadhaa, na pale kwake aliishi na mama yake. Nilistuka kidogo huo utajiri wa ghafla alikuwa kautoa wapi, na kama alikuwa tajiri kwanini alikuwa kakonda..ndipo nikajikakamua kuniuliza..na nadhani ni urafiki tu, bado hakuwa kabadilika kitabia na yeye akaanza kunihadithia;

Kufupisha mambo, ni kuwa kwenye pita pita zake usiku mmoja aliweza okota briefcase tatu pembeni ya barabara zimefichwa kichochoroni. Kama unavyoweza waza, zote zilikuwa na fedha na ma document kadhaa. Ilimbidi ampigie yule mwenye documents hizo maana alikuwa tajiri anayefahamika na kumwambia kuhusu hizo briefcase, sema alidanganya. Alisema ilikuwa moja na ndimo alimo kuta hizo document na hela. Yule tajiri alifurahi kweli maana hizo docs zilikuwa za muhimu na alikuwa kavamiwa usiku huo huo hivyo wakapanga kukutana, na yeye akamkabidhi. Kama zawadi, akapewa robo ya hizo fedha...na bado alikuwa na zile briefcase mbili nyumbani.

Hakusema kulikuwemo na fedha kiasi gani, ila hata ile robo aliyokuwa kapewa hakuwa amemaliza. Alisema alidhani angekuwa na furaha ila hakuwa anaiona. Alinambia vifaa vyote vilivyokuwa vinakosa kutimiza career zake(uDJ, kuandika vitabu, soccer, etc) alinunua, ila hakuwa anajua aende na kipi na kwanini. Yote aliyokuwa akisema angemfanyia mama yake alikuwa kamfanyia, shida ni kuwa mama yake alikuwa akimficha ugonjwa wake kwa muda(Terminal Cancer) na ulikuwa umekua kweli...naweza sema hakuwa na siku nyingi za kuishi hivyo alimleta ili aishi nae karibu, ili aweze kuhudumiwa vizuri na mkewe(na hao wafanyakazi wengine.)

Shida kubwa iliyokuwepo kuliko zote ni kuwa hakuwa na furaha kuwa alizipata hizo hela kibahati bahati na hakuziangaikia. Japokuwa alizipata na kutimiza ndoto zake kama alivyoziwazia. Hakuweza kufanya yale alitoka kufanya maana tayari alikuwa na njia mkato. Career zake zilipaswa kumfanya awe tajiri...ili aishi hayo maisha aliyowazia ila ilikuwa imetokea tofauti; Alikuwa amekuwa tajiri akatimiza ndoto zake ndipo akaondoa vikwazo vilivyokuwa vinamkwamisha kuendelea na career fulani fulani alizohangaikia kujifunza ili awe tajiri. (Sijui kama nimeielezea vizuri...kama alivyoiweka kwa maneno yake.)

Hapo ni ngumu kutoa ushauri. Ila nilimwambia ajaribu kuwa na furaha. Alinisaidia kidogo (kifedha) na mimi nikarudi chuo. Ndani ya mwezi taarifa zilinikuta kuwa mama yake alifariki na jamaa alizidi kukonda. Mwishoni mwa mwaka, alinipigia na kuniambia ana furaha. Baadae nilikuja gundua kuwa alikuwa kaanzisha kituo cha yatima, kikubwa kweli...na alikuwa akikifidia na zile brief case mbili kupitia Charity yake mwenyewe. (Yaani fedha zote aliziweka humo na kuiacha Charity i run hicho kituo na vingine kama vitano humo mkoani.)


Aliamuua kuanza kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii duniani na mkewe, na mpaka sasa ndicho anachofanya. Hicho ndicho kilicho mpa furaha, na naweza kukwambia kanenepa na ni kweli ana furaha.

Biashara kadhaa alizokuwa ameanzisha kwa hile robo aliyopewa, ndizo zinamuingizia kipato.

****

Ilinichukua muda kuweza kudadavua tatizo alilokuwa nalo wakati huo, na baada ya muda nilipata jibu. Jibu naweza kulirahisha kwenye sentensi ifuatayo;

"Kuna watoto wengi Tanzania ila hawana utoto ndani yao."

Tatizo alilokuwa nalo yeye hata mimi nilikuwa nalo, na ninawafahamu wengi ambalo wanalo. Utofauti ni kuwa kwangu likuwa tofuati. Kuwa na "Ndoto Kipofu" (Blind Dreams) na baadae kuja kukatishwa tamaa pale tunapofanikiwa kuzifikia ndoto zetu na kugundua kuwa haziko kama tulivyo ziotea.

Ukiweza kumfundisha mwanao kutaka kuwa na furaha na sio tajiri, utakuwa umemuondolea hili tatizo. Ikumbukwe kuwa nikisemea utajiri, simaanishi utajiri wa mali/fedha. Ila wa kila kitu.

Hivyo basi unamfundishaje kuwa na furaha?

Kwa wazazi wenye watoto, jaribuni kufahamu wanapendelea nini na watie moyo kuendeleza hizo passion zao. Vupo utavukuta vunapenda kuchora chora, vwingine utavukuta vunapenda kucheza mpira, vwingine kukimbia...vwingine kuimba, nk. Watieni moyo katika hayo. Haimaanishi ukimtia moyo kuwa mchoraji basi aisende shule, hapana..Aende ila awe na kipaji chake ambacho wewe kama mzazi umesaidia kukuza. Na maishani mwake mwote kitamsaidia kuwa na furaha. Sio mpaka kiwe kipaji, hata kikiwa kitu cha kawaida anachopenda kufanya. Kama ni kitu sahihi(kimaadili) then mtie motisha.

Utajiri upi unapaswa kumuepusha?

Muondolee mwanao hali ya kujaribu kuwa bora zaidi ya wengine bali kuwa bora yeye kama yeye. Nimekwambia kuhusu rafiki yangu, yeye alitafuta njia kibao za kuwa tajiri...alijifunza njia moja wapo kwa weledi mkubwa na mwishowe alipokosa 'vifaa' aliamia kwenye nijia nyingine. Hivyo hivyo alienda, na kichwani alichoamini ni kuwa angekuwa tajiri, basi angekuwa na furaha. Mambo yaligeuka alipokuwa tajiri bila kupitia yale mambo yaliyo mpotezea muda wake wote kujifunza. Alifanya kila kitu ambacho alidhani kingempa furaha na bado alijihisi mtupu. Ni kwa kuwa hakuwahi kuwa na material passion. Kuwa tajiri kwake ilikuwa ndoto, lengo na papo hapo....passion. Na hapo ndipo alipokosea. Kila mtu ndipo anapokosea. Kila mtu anahangaika kuwa tajiri, kuwa na gari la kifahali, kumiliki kampuni kubwa, kuweza kufanya kila kitu hela zinachoweza mruhusu kufanya. Siri ni kuwa vyote hivyo havikupi furaha. Pumzi unapumua ile ile na anaye panga, barabara ni ile ile, na bado kufa kuko pale pale.

*Passion ni kitu mtu anchopendelea kufanya. Na msaidie mwanao kukitafuta. Akishakipata, hicho ndicho kitakachomsaidia kuwa na furaha, maana kazi yake ikiendana na passion yake, ataipenda, atakuwa na furaha na kuwatia furaha wote watakao mzunguka.

Ahsante.
 
Mimi nitamfundisha vyote. ....

Ila mkuu ni bora kulia ukiwa ndani ya benzi ..kuliko kulia ukiwa barabarani huku una Tembea kwa miguu ni fedheha
Kwa kutilia mkazo
f277c252c05eb8df6e56fa4121d94f94.jpeg
 
Hahaha indeed. .... ila Tuachani masihara aise. .pesa ina acha vipi kukupa furaha wakati binafsi napokuwa sina na kuwa na sonona nakosa uchangamfu. .full of stress.

But pindi ni napokuwa nazo najihisi kujiamiamini na kiwango cha furaha kina ongezeka. .

Mimi ni nadhani hawa wanaosema pesa haileti furaha .ni masikini wenzangu kama mimi so wana jaribu Kujifariji tu
 
Hahaha indeed. .... ila Tuachani masihara aise. .pesa ina acha vipi kukupa furaha wakati binafsi napokuwa sina na kuwa na sonona nakosa uchangamfu. .full of stress.

But pindi ni napokuwa nazo najihisi kujiamiamini na kiwango cha furaha kina ongezeka. .

Mimi ni nadhani hawa wanaosema pesa haileti furaha .ni masikini wenzangu kama mimi so wana jaribu Kujifariji tu
Nashangaa huyo jamaa eti ana pesa ila hana furaha kisa kazipata kwa shortcut, wakati nasoma stori nikajua jamaa hana furaha na pesa labda alizipata kwa njia iliyopelekea akahatarisha afya yake kwa magonjwa kama HIV kumbe kapata tu mgao? Atakua ana tatizo sehemu
IMG_20190917_071955_590.jpeg
 
Mimi nitamfundisha vyote. ....

Ila mkuu ni bora kulia ukiwa ndani ya benzi ..kuliko kulia ukiwa barabarani huku una Tembea kwa miguu ni fedheha

Nakuelewa na naomba nisiwe misquoted. Sio vibaya kuwa na Benz, kama unao uwezo waweza kuwa nayo as long as utakuwa na furaha na sio kuonekana una Benz. Kuna kuishi na kupretend unaishi....mambo mawili tofauti.
 
Hahaha indeed. .... ila Tuachani masihara aise. .pesa ina acha vipi kukupa furaha wakati binafsi napokuwa sina na kuwa na sonona nakosa uchangamfu. .full of stress.

But pindi ni napokuwa nazo najihisi kujiamiamini na kiwango cha furaha kina ongezeka. .

Mimi ni nadhani hawa wanaosema pesa haileti furaha .ni masikini wenzangu kama mimi so wana jaribu Kujifariji tu
Sababu ya kuandika huu uzi ni kumsaidia mwanao asiwe kama wewe. Kudhani kuwa furaha inatokea wallet ikivimba.
 
Mwingine furaha Yake Ni kuwa Bora kuliko wengine.Mfano mzuri bilionea mumiliki wa kampuni ya TATA inayotengeneza magari ambako India nzima huyatumia yeye usafiri wake hutumia daladala na mabasi ya safari ndefu ya abiria ya TATA .Alipoulizwa kwa Nini wakati yeye bilionea akajibu hakuna kitu kinanipa Raha Kama kuona watu wanatumia mabasi yaliyoyengenezea na kampuni yangu nikiangalia abiria Sio ndugu zangu wanatumia huduma inanipa Raha Sana na inanitanya nijitume Sana niwe Bora zaidi kuliko yeyote India sekta ya magari.

Bilionea mwingine Ni Dangote yeye toka mdogo furaha Yake ilikuwa kuwa mfanyabiashara mkibwa kuliko wote Nigeria na kawa.

Furaha Ni subjective kila mtu ana kitu kiwezacho kumpa furaha huwezi mfundisha mtu furaha Yake iweje.Shule vyuo michezoni nk Kuna ambao furaha yao huwa kuwa Bora kuliko yeyote.
 
Bila pesa hata humu mtandaoni usingeingia kuandika ulicho kusudia kuandika kwa kupinga ebu jaribu kuacha kutafuta pesa kaa kama mwali ndani uone jinsi mke wako atakavyo kuzarau apo ndio utajua heshima nini
 
Asante kwa uzi mzuri wachache sana tutakuelewa umeandika nini
Bilionea Billy gates toka mdogo wazazi wake walimsistiza chochote afanyacho afanye vizuri kuliko yeyote.Akadevelop na hiyo spirit Hadi Sasa Ni best duniani kwenye ma software ya Microsoft.Kumzuia mtoto kuwa best kuliko wengine Ni kuua potential iliyo ndani ya mtoto .Mtoto anatakiwa achochewe potential zake to the maximum
 
Bilionea Billy gates toka mdogo wazazi wake walimsistiza chochote afanyacho afanye vizuri kuliko yeyote.Akadevelop na hiyo spirit Hadi Sasa Ni best duniani kwenye ma software ya Microsoft.Kumzuia mtoto kuwa best kuliko wengine Ni kuua potential iliyo ndani ya mtoto .Mtoto anatakiwa achochewe potential zake to the maximum
😮😊 Main theme ya uzi sio kumzuia asiwe zaidi ya wengine. Ni kumsaidia atafute passion. Then anaweza taka awe best, hapo ni sahihi kama haimpi stress na anafuraha. Kwa point of view yako ni sawa na kumchukua Bill Gates na kujaribu kumfanya awe best kwenye mpira wa miguu na sio passion yake. Ninakuwa misquoted.
 
Back
Top Bottom