Swali zuri.
Mfumuko wa bei (inflation), ni mfumuko wa level ya bei za bidhaa na huduma kiujumla, si kitu kibaya, ukiwa kwa kiwango kinachotakiwa unachangamsha uchumi kwa kuwapa motisha wazalishaji kama ulivyosema katika swali.
Ukweli ni kwamba kukiwa hakuna ongezeko la bei kabisa, au level ya bei kuwa zinashuka kutokana na nguvu za urari wa soko, demand and supply, (deflation, not to be confused with disinflation), jambo hilo hufanya watu wakose motisha ya kuzalisha. Kitu hiki kilitokea Japan muda fulani, mpaka kukawa na negative interest rates, yani benki kuu ya Japan il8kuwa inalipa benki za ndani riba benki zikichukua mkopo, badala ya benki za ndani Japan kuilipa benki kuu riba, benki kuu ililipa benki zingine riba (-0.1% by January 2016), hizi zilikuwa jitihada za kuongeza hela katika uchumi na kuchochea ongezeko la bei ili kuongeza motisha ya kuzalisha.
Hivyo, kiujumla ongezeko la bei si kitu kibaya.
Tatizo linakuja unapokuwa na mfumuko wa bei unaopanda kwa kasi, kiingereza wanaita galloping inflation, ambayo inakuwa 10% au zaidi, hapo sasa hata ile faida ya kuwapa watu motisha ya kuzalisha inamezwa na ukweli kwamba, hata hao watakaozalisha watakabikiwa na mfumuko wa bei. Kwa mfano, unaweza kusema mfumuko wa bei utakuwa unaleta motisha kwa wakulima kulima mazao ya vyakula, wapate faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za vyakula, lakini unaweza kujuta faida watakayopata inaenda kufidia ongezeko la bei za mbolea, pembejeo, madawa, uhifadhi na usafirishaji, kufanya mkulima akose faida, au hata kuingia hasara kabisa.
Kwa hiyo, kifupi, mfumuko wa bei ukiwa katika kiwango sawia unatakuwa na unatoa motisha kwa wazalishaji kuendelea kuzalisha, kwa sababu wazalishaji wakijua bei zinashuka wataacha kuzalisha, lakini mfumuko huo ukiwa mkubwa sana, hususan zaidi ya 10%, unafanya bei za bidhaa na huduma nyingi zipande, kiasi za gharama za uzalishaji kupanda na kumfanya mzalishaji arudishe gharama za uzalishaji bila faida (break even), au hata kuingia hasara.