Mfumuko Wa Bei Mwezi Huu

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wapendwa wana JF,

Najua kuna threads mbili zimo humu kuhusiana na Mfumuko wa Bei moja ikiwa imeanzishwa na Invicible na nyingine ikiwa imeanzishwa na Invisible. Hata hivyo nimeona ziko very general kwa hiyo nimefikiria kuwa ni vema tukawa na Thread ya kudumu kwa jina la "MFUMUKO WA BEI MWEZI HUU" ambayo kwayo tunaweza kufanya updates kila siku/wiki/mwezi na kila baada ya nusu mwaka tufanye tathmini ili tuweze kuangalia wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda.

Mwezi huu (Desemba 2007) vitu vifuatavyo vimepanda bei na nimegundua baada ya kufanya shopping wiki hii. Mimi mkazi wa Arusha nimegundua haya:-

1. Bei ya Gesi (LPG) ya kilo 40 imepanda kutoka shilingi 64,000/ (mwezi Julai) hadi shilingi 73,000/- mwezi huu wa Desemba!

2. Betri kubwa za Panasonic (Made in Tz) zimepanda kutoka shilingi 400/- kwa betri (Novemba) hadi shilingi 450/- mwezi huu wa Desemba.

3. Balbu za umeme za kawaida zimepanda kutoka shilingi 300/-kwa balbu (mwezi Novembea) hadi shiliongi 400/- kwa balbu mwezi huu wa Desemba.

4. Bei ya Mkate mdogo wa "Super loaf" imepanda kiasi cha kutisha kutoka shilingi 500/- mwanzoni mwa mwaka hadi 550/- katikati ya mwaka na sasa mwezi huu wa Desemba imefikia shilingi 600/-!
 
Ni kweli tunahitaji kitu kama hiki, maana watu wengi wanaishi blindly bila kupata concern ya mfumuko wa bei kwa sababu kunakuwa hamna uwanja wa kujadili suala hili. Wengi wanaona ni sawa kama ikiongezeka tshs 50 lakini hawajui athari zake kwasababu tunashindwa ku keep track of those things. I think its about time we knw tunaathirika vipi na hali yetu ya uchumi
 
..tunaelekea kwenye kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka!je?hii ndio inayochangia mfumuko wa bei?...kwa wale mtakao safiri kwenda makwenu,vipi nauli zitapanda?kuna wenye mabasi wamesema hawatapandisha nauli,tusubiri tuone!
 
Wapendwa wana JF,

Najua kuna threads mbili zimo humu kuhusiana na Mfumuko wa Bei moja ikiwa imeanzishwa na Invicible na nyingine ikiwa imeanzishwa na Invisible. Hata hivyo nimeona ziko very general kwa hiyo nimefikiria kuwa ni vema tukawa na Thread ya kudumu kwa jina la "MFUMUKO WA BEI MWEZI HUU" ambayo kwayo tunaweza kufanya updates kila siku/wiki/mwezi na kila baada ya nusu mwaka tufanye tathmini ili tuweze kuangalia wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda.

Mwezi huu (Desemba 2007) vitu vifuatavyo vimepanda bei na nimegundua baada ya kufanya shopping wiki hii. Mimi mkazi wa Arusha nimegundua haya:-

1. Bei ya Gesi (LPG) ya kilo 40 imepanda kutoka shilingi 64,000/ (mwezi Julai) hadi shilingi 73,000/- mwezi huu wa Desemba!

2. Betri kubwa za Panasonic (Made in Tz) zimepanda kutoka shilingi 400/- kwa betri (Novemba) hadi shilingi 450/- mwezi huu wa Desemba.

3. Balbu za umeme za kawaida zimepanda kutoka shilingi 300/-kwa balbu (mwezi Novembea) hadi shiliongi 400/- kwa balbu mwezi huu wa Desemba.

4. Bei ya Mkate mdogo wa "Super loaf" imepanda kiasi cha kutisha kutoka shilingi 500/- mwanzoni mwa mwaka hadi 550/- katikati ya mwaka na sasa mwezi huu wa Desemba imefikia shilingi 600/-!

Ibrah,
Thanks- tupe source ya data. Je tunanaweza kupata % increse pia kwa kila mwezi au miazi mitatu?

N:B Vipi bei ya cement? Ni kweli Dar ni 16,000 na Mwanza ni 25,000 hadi 30,000?
 
Ibrah,
Thanks- tupe source ya data. Je tunanaweza kupata % increse pia kwa kila mwezi au miazi mitatu?

N:B Vipi bei ya cement? Ni kweli Dar ni 16,000 na Mwanza ni 25,000 hadi 30,000?

Asante mkuu,

Source ya data zangu ni madukani ambapo nanunua bidhaa mara kwa mara. KWa mfano LPG (gesi) ya kilo 40 nimenunua juzi tu baada ya gesi yangu ya nyumbani kuisha, mara yangu ya mwisho kununua ilikuwa Julai ambapo nilinunua 64,000/-. Mkate ndiyo kitafunwa changu cha kifungua kinywa; betri kubwa natumia kwa ajili ya tochi (kila betri zikisha nguvu nanunua nyingine.

Kuhusu bei ya cement sina jibu lakini kesho nitawapostia hapa bei ya cement kwa hapa Arusha.
 
Nadhani tukitengeneza utaratibu mzuri kuhusu hii thread tunaweza kupata actual inflation rate in TZ na ku-compare na ya BOT. hapo tutajua kama kuna siasa kwenye data zao.
 
Asante mkuu,

Source ya data zangu ni madukani ambapo nanunua bidhaa mara kwa mara. KWa mfano LPG (gesi) ya kilo 40 nimenunua juzi tu baada ya gesi yangu ya nyumbani kuisha, mara yangu ya mwisho kununua ilikuwa Julai ambapo nilinunua 64,000/-. Mkate ndiyo kitafunwa changu cha kifungua kinywa; betri kubwa natumia kwa ajili ya tochi (kila betri zikisha nguvu nanunua nyingine.

Kuhusu bei ya cement sina jibu lakini kesho nitawapostia hapa bei ya cement kwa hapa Arusha.

This is the most credible raw data you can get. Achana na hizo za wapikaji wa BoT
 
Bravo Ibrah,
Ni kweli kabisa tunaweza kabisa kukusanya data nzuri sana kwa ajili ya inflation.
Nilijaribu kufuatilia bei ya bidhaa mbali mbali Tanzania 2003 hadi 2005 sikuweza kupata hizo taarifa cha aajabu ukisoma BOT Economic Bulletin utakuta zimekuwa reported wakati wa kukokotoa inflation. Ukijaribu koanisha na zile ambazo nilikusanya hazioani hata kidogo hata ukijaribu kutafuta average bado Its far from the truth.

Naamini thread hii itasaidi lakini cha msingi ni kudefine type ya commodities ambazo ni muhimu kwa kila mwanajamii ndio tuziangalie kwa makini zaidi
 
Do you mean as in

Vyakula
1)Staple foodstuff kama unga na mchele pamoja na vitoweo na matunda kama maharage, samaki na maembe etc

2)Fuel kama petroli, gesi, mafuta ya taa, mkaa etc

3)Vifaa na bidhaa za ujenzi kama mchanga, cement, kokoto

4) Mazao ya biashara kama kahawa, pamba, korosho

5) Huduma kama usafiri (nauli) basic fees za daktari etc

6)Highest/Lowest exchange rates
?

We may spot some interesting trends that cannot be easily seen from the ground.
 
N:B Vipi bei ya cement? Ni kweli Dar ni 16,000 na Mwanza ni 25,000 hadi 30,000?

..bei ya cement nchi nzima inacheza kati ya 15500 hadi 25000. hii inatokana na umbali toka kiwandani[gharama za usafirishaji]na kanda ya ziwa ndo wanakoma zaidi na hii bei!kama kule bukoba!

..tatizo liko kwenye miundombinu choka ya usafirishaji[reli bomu,barabara hovyo!]ambayo inaongeza gharama!
 
Inasikitisha kuona such a huge difference due to transportation costs.

Tutaendelea kujenga kwa muda mrefu sana.Kama raw materials za simenti zinaweza kupatikana locally tuwekwe investors wakujenga kiwanda kila kanda, hii itachochea ujenzi sana.

Tuna Dar for the east Tanga for the north east na Mbeya for the south, the west/ziwa needs one. Overtime kinaweza kujilipia kutokana na kupunguza gharama za usafirishaji.
 
Inasikitisha kuona such a huge difference due to transportation costs.

..hii imechochewa zaidi na viwanda kuacha kuwa na depots mikoa ya mbali,badala yake wanakuwa na agents,distributors,et al. hawa nao wanaweka profit margin yao....ndo mambo yanakuwa hivyo!

Tutaendelea kujenga kwa muda mrefu sana.Kama raw materials za simenti zinaweza kupatikana locally tuwekwe investors wakujenga kiwanda kila kanda, hii itachochea ujenzi sana.

..wazo muafaka kwa long term,short term ni kununua toka ug au kq. musoma saruji ya bamburi ni kama 17500 or so!

Tuna Dar for the east Tanga for the north east na Mbeya for the south, the west/ziwa needs one. Overtime kinaweza kujilipia kutokana na kupunguza gharama za usafirishaji.

..kweli,ila usafirishaji lazima uwe bora!ama sivyo itakuwa yaleyale!
 
Mfuko wa cement Dar kwa sasa ni Tshs 14,500; Kigoma-ni kati ya 25,000 na 27,000; Tabora ni 23,000.

Wazo la kuanzisha viwanda in strategic areas ni muafaka.
 
Nadhani suala sio kiwanda maana kusafirisha contena mfano 20Ft kutoka dar hadi Mwanza ni Ghali kuliko kusafirisha same contena kutoka Japan hadi Dar Tatizo nini?

1. Barabara Mbaya so magari waer and tear ni kubwa anf uel consumption kubwa.
2. Mfumo wa Reli sio imara na wa kuaminika kwani ungeweza kupunguza hiyo gharama almost kwa nusu ( nenda railway uone utakachoombiwa toa kitu kidogo ili usafirishiwe mapema mwishoni gharama zinakuwa zilezile za truck) na mzigo wako unaweza ibiwa ukisafirisha kwa Train.

Ukisema ujenge kiwanda cha cement huko
1. bado gharama za kusafirisha raw material kutoka same Kilimanjaro na sehemu ingine yanakopatikana madini hayo gharama inakuwa almost the same.

2. Sina kumbukumbu nzuri lakini nadhani sehemu kubwa ya Kando ya ziwa haijaunganishwa na umeme wa grid ya Taifa pamoja na gharama ya kusafirisha Fuel kwa ajili ya ku-run mitambo yao naona gharam bado itakuwa almost same.

Swali la kujiuliza
kama kutoka dar hadi Dom mfuko mmoja unacost 900 kuusafirisha which is almost 600Km na kutoka Dom hadi Mwanza is almost 600Km iweje ighrimu more than 5,000?

Je kwa nini serikali isifikirie kuruhusu cement kutoka Uganda, Ruanda, Burundi au Congo kwa wakazi wa mipakani kama inaweza kupatikana kwa bei nafuu zaidi katika maeneo hayo? Ili miundombinu ikikamilika naamini kila kitu kitakuwa shwari
 
ni hatari, sijui huyu kiongozi mwema lini itatunga mimba yake?. wakunga ndio sisi , lakini nadhani kazi ya kuzalisha kiongozi mwema imetushinda. kule kwetu zenji mpaka miguu ya kuku inauzwa kwa kilo sasa.wengi wamechoshwa na hii hali.natamani huyu rais naye tungekuwa tunapanga foleni pamoja pale darajani kununua mkate ili na yeye akaonja yale wanyonge wanayoyaonja.
 
Ni kweli bei ya cement Dar imepanda. Mimi nina shuguli ya ujenzi kwa wiki tatu sasa nilianza kununua mfuko kwa shs 15000/=. lakini kuanzia wiki iliyopita mpaka jana mchana nimekuwa nikinunua mfuko kwa shs 16000/= maeneo ya Yombo Vituka (karibu na Airport. Na bei hii ya shs 16000/= ilibadilika siku moja kutoka shs 15000/=.
 
BowBow, et al:
Simenti imepanda bei kwa sababu inauzwa nje - Afrika Kusini kuliko na ujenzi wa viwanja, n.k; na DRCongo inapendwa sana kwa ubora wake.
Na kwa wenye viwanda, of course ni priority kwao ku-export kuliko kuuza kwa madafu, and there is nothing you and I can do about it!
 
Bei ya Soda jamii ya Coca cola nayo imepanda, jana nimenunua soda Sprite kwa shiling 350/- nikashituka maana wiki ilopita ilikuwa 300/- nikamuuliza muuzaji kwa nini ametupandishia akasema kuwa Soda imepanda!Leo asubuhi nimempa lifti jirani yangu ambaye ana duka nikamuuliza akanithibitishia kuwa bei ya Soda imepanda tangu Jumanne wiki hii.

So, bei ya Soda jamii ya Coca cola hapa Arusha ni Shilingi 350/- kwa chupa badala ya shilingi 300/-!
 
Kufa hatutakufa ila cha moto tutakiona. Aga khan gharama za kujifungua ni laki tano! sasa tunashangaa nini wakinamama wanavyokufa huko muhimbiri na vijijini? tatizo Si mfumuko wa bei tu bali na ugawanyaji wa hali ya juu wa huduma za walio na fedha na za wasionazo hakuna minimum quality standard.
 
Bei ya Soda jamii ya Coca cola nayo imepanda, jana nimenunua soda Sprite kwa shiling 350/- nikashituka maana wiki ilopita ilikuwa 300/- nikamuuliza muuzaji kwa nini ametupandishia akasema kuwa Soda imepanda!Leo asubuhi nimempa lifti jirani yangu ambaye ana duka nikamuuliza akanithibitishia kuwa bei ya Soda imepanda tangu Jumanne wiki hii.

So, bei ya Soda jamii ya Coca cola hapa Arusha ni Shilingi 350/- kwa chupa badala ya shilingi 300/-!

..bei ya chupa ya 350 mls ya coke au pepsi ni kuanzia 350/= hadi 600/=. sehemu nyingi za manywaji[sebuleni] ni 500/=. bei hii inakama mwezi sasa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom