Mfumo wa utawala Malawi nimeupenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa utawala Malawi nimeupenda

Discussion in 'International Forum' started by Hemed Maronda, Apr 18, 2012.

 1. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfumo unaotumika katika vyama vya siasa na Serikali Malawi ni mzuri na unaheshimu sana wapiga kura,ningependa mfumo kama huo ungetumika hapa nchini kwetu,kwa mfano Marehemu Dr Bingu wa Mutharika alipogombea Uraisi kwa mara ya kwanza alisimama kwa tiketi ya UDF lakini baada ya kupata Uraisi akatofautiana na Mwenyekiti wake wa UDF Dr Bakili Muluzi,akaona isiwe taabu akajiondoa kwenye Chama na akaunda Chama chake DPP huku bado akiushikilia Uraisi wake,kwetu sisi Watanzania isingewezekana! Makamu wake Dr Kasim Chilumpha akabaki kwenye UDF.Dr Bingu alipogombea kipindi cha pili alisimama kwa tiketi ya DPP akiwa na runningmate wake Bibi Joyce Banda,baada tu ya muda mchache akakosana pia na Makamu wake Bibi Joyce Banda,nae akaona isiwe shida akajiondoa toka DPP akaunda Chama chake PP ambacho leo hii kinaongoza Serikali baada ya kufa Dr Bingu kikiwa na Wabunge wawili tu! Demokrasia hii nimeipenda tofauti na ilivyo hapa kwetu Mbunge tu akitolewa uanachama anapoteza pia na nafasi yake ya uwakilishi kama ilivyotokea kwa Hamad Rashid wa CUF.Ningependa swala hili liwekwe wazi kwenye Katiba yetu mpya inayokuja Wanabodi mnasemaje?
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapana. Huu utaratibu siyo mzuri kwa sababu una assume kwamba wapiga kura wanachagua mtu badala ya chama kitu ambacho si kweli. Alafu pia utaratibu huu una assume kwamba hao waliokuwa na vyeo walipata hivyo vyeo wakiwa wagombea binafsi kitu ambacho pia si kweli. Nina support utaratibu wetu uendelee.
   
 3. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa tatizo linalojitokeza kwenye mfumo wetu ni kuwa watu kumi tu wakiwa na visasi nawe kwenye Chama wanaweza kukuondoa uanachama na ukakosa nafasi yako ya uwakilishi ambayo umechaguliwa na watu 59,000 je ni Demokrasia yenye mshiko? Na mara nyingi tunapochagua huwa hatuangalii Chama kwa mfano kuna majimbo mengine ya uchaguzi kama la Mheshimiwa Shibuda yeye aligombea kwa tiketi ya CCM lakini huko hawakumtaka Viongozi wa juu matokeo amehama Chama na kuhamia Chadema na ameshinda hivyo inaonyesha dhahiri watu hawachagui Chama ila wanachagua mtu ambae anaweza kuwasaidia kuwaongoza kupata maendeleo hivyo bado mi naona mfumo wa Malawi ni mzuri zaidi kwakuwa wapo viongozi katika Vyama vya siasa kwa makusudi wanawabana wenzao kwa nafasi zao ili wasiwatumikie Wanainchi,angalia walivyokuwa wanataka kumvua uanachama wakati ule Spika Sitta eti tu alikuwa anawapa nafasi wapinzani kuibana Serikali kwenye mambo ya Ufisadi je ni sahihi?
   
 4. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huu mfumo wa Malawi ni mzuri kwa sababu kiongozi anakuwa hafungwi sana na chama chake. Yawezekana kabisa sasa hivi akawepo mbunge anayetamani kujiondoa ccm, lakini kwa hofu ya kupoteza ubunge wake anashindwa kufanya hivyo. Tunakihitaji kitu hiki kwenye katiba yetu ijayo.
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya chama si magumashi ya CCM. Ndio maana hawataki wagombea huru maana ili mambo yaende tunataka watu wenye uwezo ndo wawe viongozi na sio lazima watu wenye ushabiki na chama fulani cha siasa.
   
Loading...